Furahia muda ulionao na yule unayempenda. Kila mtu tuliyenaye kwenye maisha yetu hatadumu milele

totoadela

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
350
1,075
Furahia MUDA ulioanao na yule unayempenda. Kila mtu tuliyenaye kwenye maisha yetu hatadumu milele.

Wengine tutakuwa nao kwa muda mrefu sana na wengine tutakuwa nao kwa muda mfupi.

Mungu hutupa watu kwa MAJIRA fulani na kwa MAKUSUDI fulani

Ni rahisi sana kujikuta ukisubiria ufike kiwango fulani Au upate kitu fulani ndipo uweze kufurahia maisha, Ila utagundua kadri siku zinavyoenda ndivyo unavyozidi kusogeza mbele FURAHA.

Usisahau kuwa kila ULIYENAYE, lazima kuna MADHAIFU na MAPUNGUFU anayo.

Unachotakiwa ni kuamua kuwa, katika muda ambao uko naye uangalie yale mazuri ambayo yatakupa FURAHA kwa wakati huo,Kama hajaja kukupa FURAHA, basi atakuwa amekuja KUKUFUNDISHA Au atakuwa amekuja.

KUKUUNGANISHA na mtu.Hakuna mtu ambaye hana FAIDA, hata yule ambaye amekusababishia MAUMIVU naye pia kuna SOMO AMEKUPA.
 
Ukipata nafasi mwambie akupendae kwa dhati ahsante kwa kunipenda.
Kuna watu mapenzi yanawafanya vitu sio
 
Nilimpenda sana
Nilimpenda sana
Nilimpenda sana.

Upendo unasamehe
Upendo unavumilia
Upendo unatunza

Mungu amfanyie wepesi huko aliko kwangu nilifanya na kujitoa kadri nilivyoweza tena kwa upendo mkubwa.
Nimejifunza mengi mazuri na mabaya katika upendo. Hamida
 
Nilimpenda sana
Nilimpenda sana
Nilimpenda sana.

Upendo unasamehe
Upendo unavumilia
Upendo unatunza

Mungu amfanyie wepesi huko aliko kwangu nilifanya na kujitoa kadri nilivyoweza tena kwa upendo mkubwa.
Nimejifunza mengi mazuri na mabaya katika upendo. Hamida
Hamida kwanini umeiacha hamida.
Hamidaaaaa.
Pole mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom