Funzo kwa CHADEMA: Huwezi kwenda Ikulu kwa kutumia njia ya mkato

Andiko zuri sana.Ila kwenye hili ..........lakini ukawa na presha za ndugu zako, presha za jamaa zako presha za marafiki zako.

Je Rais ataweza kupambana na hiyo pressure?
 
Tuliiba nini?

Fafanua!

Bichwa lako sijui limejaa nini.... Pole sana MsemajiUkweli ila nahisi si mda utakuwa msema uongo... Fikra zako unazigeuza za watanzania? Aliewekwa atawatumikia kina flani. Siku zaja watu waanze kupiga dili kama kawa, CCM ni ile ile wamebadili chupa tu, dili zitapigwa na watanzania tutaisoma namba😃😃😃😃
 
Last edited by a moderator:
Kweli nyani haoni kundule lake hivi yule alikuwa anaanguka anguka wakati wa kampeni kwenye uchaguzi wa 2010 alikuwa nani vile? Watanzania sio wajinga wanajua mlichofanya.

Kikwete hakuanguka anguka, Kikwete alianguka tena mwishoni mwa kampeni. na alichunguzwa na madaktari na ripoti kutolewa kuwa ni FATIKI za kampeni. Kumbuka alichaongoza miaka 5.

Huyu wenu anashikiliwa toka day one, anapotezaza kumbukumbu, anadungwa masindano mpaka anakuwa zezeta
 
Mwaka 1995, Mwl. Nyerere aliwahi kusikika akisema, ''I can't let my country go to the dogs''. Hii ni sentensi fupi lakini umebeba ujumbe ambao mpaka sasa watanzania .........

But contrary to what Mwalimu vowed to keep to his dying bed, he didn't infact let the country ony to the dogs, but to thje viscious JACKALS!!
 
Kwa nini vituo ya chadema viwe vya ukweli lkn vya Serikali visiwe vya ukweli? Na kama NEC waliiba kura una uhakika gani kama vituo vya chadema vilikuwa haviibi?

Na kama chadema wana ushahidi wa kuibiwa kura ni kwa nini hawauonyeshi mpaka leo hii mpaka Raisi ameshaapishwa, wabunge wao wameshaapishwa na kupiga kura ya kumchagua Spika wa Bunge na sasa Waziri Mkuu anatangazwa na watampgia kura au kama hawaamini mfumo wetu ili kutafuta haki ni kwanini hawaupeleki kwenye vyombo vya Kimataifa kushitaki kama vile Umoja wa Afrika, SADC, UN ?
Je, tunapaswa kuamini kwamba chadema waliibiwa kura kwa sababu tu wanasema hivyo na kwa kuwa chadema wao ni watakatifu?
Viongozi wakuu wa CHADEMA wameamua kujificha kwenye hoja ya kuibiwa kura ili kuyakimbia maneno yao ambayo yaliwaamisha baadhi ya watu eti watashinda uchaguzi mkuu wa Rais kwa zaidi ya 80% ya kura.

Wanapiga kelele za kuibiwa kura bila kuwa na ushahidi kamili.
 
Wakati naweza kukubaliana nawe kwa mengi, zingatia matumizi mazuri ya maneno.
Nukuu yako haiko sawa; Mwl Nyerere hakutumia neno "dogs" kumaanisha kile alichosema kwa mantiki/maudhui ya lugha ya kiingereza (hapa usitafsiri kwenda kiswahili neno kwa neno).
Mwl Nyerere alitumia neno "underdogs" ambalo lina maana tofauti kabisa na neno 'dogs' ingawa yote yana herufi zenye kufanana.
Kipindi hicho upinzani ukiwa unaongozwa na Mh Augustine Lyatonga Mrema, na ukiwa karibu kuchukua dola, Mwl akawa makini kutoruhusu upinzani kuchukua utawala, ndio akatamka sentensi hii, "I can't let my country go to underdogs" kwa maana ya kutoruhusu nchi yake iwe mikononi mwa watu wasio na uzoefu, wasio na uwezo mkubwa wa kutosha kuongoza nchi.
Ref: https://en.wikipedia.org/wiki/Underdog_(term)
Mfano mzuri:
Katika mechi ya TZ na Algeria, TZ, ikilinganishwa na Algeria ambayo imeshashiriki mara kadhaa katika fainali za kombe la dunia bado TZ ni UNDERDOGS.
Naomba kuwasilisha
 
Tatizo la uchaguzi kwa Chadema na Tanzania yote ni kwamba kwa mfumo tulio nao upinzani hauwezi kushinda mpaka pale tutakapokuwa na tume huru ya uchaguzi. Tume tuliyo nayo si huru, ya haki na iliyo wazi. Tungekuwa na tume huru CCM isingelazimika kutumia vyombo vya dola kuzuia Chadema isikusanye matokeo ya uchaguzi kwa sababu kama tungekuwa huru matokeo yaliyokusanywa na Chadema yasingetofautiana na yale yaliyotolewa na tume ya uchaguzi. Chadema hata kama wangesimamisha malaika au Yesu matokeo yangekuwa yale yale madhali tume ya uchaguzi ina kauli ya mwisho katika utangazaji wa matokeo ya kura. Lakini kwa bahati nzuri kule Zanzibar CCM imeumbuka vibaya.
Jasusi, kuna tofauti kubwa ya kushinda na kutangazwa mshindi, kwa uchaguzi huu 2015, Lowasa hajashinda na wala hajatangazwa mshindi kwa sababu HAJASHINDA. Hamuitaji ku sugar-coat na kudanganya watu kuwa EL alishinda ila matokea yakabadilshwa, ebu wewe tusaidie hata jimbo moja tu ambalo matokeo yaliyotangazwa na TUME ni tofauti na yaliyobandikwa kituoni. Magufuli ameshinda viti 218 kati 264, Magufuli ameshinda mikoa yote Tz bara kasoro Arusha, Kilimanjaro na Dar, achane propaganda zisizo na mashiko.
Kuhusu Tallying center ya CDM, tar 26 kwenye press conference yao baada ya Tallying center yao kufungwa, John Mrema alisema wazi kabisa mbele ya waandishi wa habari, tayari wana Tallying centers nyingine, sasa hii sababu ya kushindwa sababu ya Tallying center mbona hamueleweki. Vilevile tangu lini ujumlisha wa kura tu ukahitaji foreigners ?
CDM wawe wawazi tu hao foreigners wataalam wa IT walikuwa wanafanya nini kwenye Tallying center zao ?
Sheria za nchi zinakataza foreigners kushiriki kwenye siasa za Tz isipokuwa kama mgeni au observer tu, hauwezi kulalamika kufungwa hizi Tallying center.
Jasusi, nakuheshimu kutokana na historia ya mambandiko yako, ila inashangaza kwa mtu kama wewe kuendekeza "Unyumbu", tatizo ina tatizo kubwa kama watu wake wanaamini wanajielewa wanaendekeza ushabiki na mihemko tu.
 
Last edited by a moderator:
Ccm ingemsimamisha Lowassa na Ukawa ikawa na Sr.Slaa na wakazunguka na Lipumba nchi nzima kama Manager wa Kampeni basi Ccm ingepoteza viti zaidi na Urais ingeshinda ila kwa Margin ndogo sana

Isingeshinda hata kwa kuiba..chadema wangechukua nchii tena bila hata kujiunga kama ukawa
 
Kweli nyani haoni kundule lake hivi yule alikuwa anaanguka anguka wakati wa kampeni kwenye uchaguzi wa 2010 alikuwa nani vile? Watanzania sio wajinga wanajua mlichofanya.
kuna tofauti ya kuanguka kwa udhaifu wa mwili na kushindwa kuhutubia kwa udhaifu mwingine
Unaweza kuanguka jukwaani lakini kumbukumbu ziko sahihi na unakukimbuka unachokisema
 
Kura za Tunduma mlisema Lowasa amepata elufu 6 tu hizo hapo ngapi? Kama siyo wizi?
Musitake tuongee mengi wakati nyinyi Ni majizi.
Masanduku ya kura feki yote yaliyokamatwa kesi ziko wapi?
Wapi NEC walisema amepata kura 6,000?

Unapotoa tuhuma lazima pia ulete ushahidi kamili.
 
Jasusi, kuna tofauti kubwa ya kushinda na kutangazwa mshindi, kwa uchaguzi huu 2015, Lowasa hajashinda na wala hajatangazwa mshindi kwa sababu HAJASHINDA. Hamuitaji ku sugar-coat na kudanganya watu kuwa EL alishinda ila matokea yakabadilshwa, ebu wewe tusaidie hata jimbo moja tu ambalo matokeo yaliyotangazwa na TUME ni tofauti na yaliyobandikwa kituoni. Magufuli ameshinda viti 218 kati 264, Magufuli ameshinda mikoa yote Tz bara kasoro Arusha, Kilimanjaro na Dar, achane propaganda zisizo na mashiko.
Kuhusu Tallying center ya CDM, tar 26 kwenye press conference yao baada ya Tallying center yao kufungwa, John Mrema alisema wazi kabisa mbele ya waandishi wa habari, tayari wana Tallying centers nyingine, sasa hii sababu ya kushindwa sababu ya Tallying center mbona hamueleweki. Vilevile tangu lini ujumlisha wa kura tu ukahitaji foreigners ?
CDM wawe wawazi tu hao foreigners wataalam wa IT walikuwa wanafanya nini kwenye Tallying center zao ?
Sheria za nchi zinakataza foreigners kushiriki kwenye siasa za Tz isipokuwa kama mgeni au observer tu, hauwezi kulalamika kufungwa hizi Tallying center.
Jasusi, nakuheshimu kutokana na historia ya mambandiko yako, ila inashangaza kwa mtu kama wewe kuendekeza "Unyumbu", tatizo ina tatizo kubwa kama watu wake wanaamini wanajielewa wanaendekeza ushabiki na mihemko tu.
Kama ni foreign tallying experts mbona hata CCM walikuwa nao? Hukulisikia hilo? Unaiamini kweli NEC? Mwaka 1995 Mrema alimshinda Mkapa lakini Mkapa akatangazwa mshindi na NEC kwa kushirikiana na usalama wa taifa. Sina imani kabisa na NEC.
 
Swali ni kwamba una ushahidi wa kwamba kura ziliibiwa? Hicho ndicho muhimu hayo mengine yote hayana maana kwani kama swala ni kusema na kunukuu tu sijui Marekani kasema hivi au vile kila mtu anaweza, hata ACT nao wanaweza kusema kwamba wameshinda Mkoa wa KLM lkn wameibiwa kura na wakatafuta msemo ambao umesemwa na Mmarekani na unaendana na wanachokilalamikia, hivyo wanachoopaswa kufanya ukawa ni kuja na ushahidi mbele ya Dunia na walipaswa kufanya hivyo punde tu Tume walipotoa matokeo!
Barbarosa, ili kukata mzizi wa fitna tuwekee hapa matokeo yote ya uchaguzi yaliyobandikwa kwenye vituo zaidi ya elfu 65 vya kupiga kura Tanzania tuyalinganishe na matokeo yaliyotangazwa na NEC. Bila hivyo tutakuwa tunasaga unga kwenye kinu cha maji.
 
Siwezi kufanya hivyo kwa maana sina shida na Tume ya uchaguzi, nina Imani nayo na kwamba matokeo waliyoyatoa ndiyo sahihi, sasa ni jukumu la wale ambao wanasema matokeo siyo sahihi watoe ushahidi wao, lkn siyo mimi!
 
Sisi wengine hatuna imani na NEC iliyochaguliwa na CCM kusimamia mechi ambapo CCM ni mshindani pia. Zanzibar imethibitisha kuwa hofu zetu ni za msingi. Wewe endelea kuwa na imani na chombo kisicho huru na wazi. Matokeo ya MNEC hayawezi kuwa independently verified and that is where the problem lies. Zanzibar imefungua macho ya watu wengi.
 
Back
Top Bottom