Fundi simu leo nusu nichezee kipigo kutoka kwa mteja

LA7

JF-Expert Member
Aug 26, 2019
457
1,736
Leo nikiwa zangu ofisini kwangu jua la mchana hivi nikiwa napiga tu miayo kwa njaa ya pesa,

Akaja mdada mmoja akiwa na simu ya batani imevujia kioo, sasa kwa bahati mbaya nikawa sina kioo cha aina hiyo, kwa haraka haraka nikapiga hesabu kuna simu moja ya mteja nilimtengenezeaga spika akawa hajaja kuchukua mwezi na kitu umepita,

Nikaona nitoe kioo nimuwekee huyu mteja ili hii ridhiki isinipite, kweli nikamuwekea mteja akaniachia changu hapo miayo ikapungua, huku nikiamini kesho nikienda mjini nirudishie kioo cha yule mteja,

Hamad! Usiku wa saambili mteja wa simu huyu hapa na anaikuta simu yake mezani ikiwa haina kioo, nikajaribu kumuelewesha lakini wapi, alikuwa ametupia halafu, akanipa hela nilokuwa namdai 3000 akaniambia nimpe simu yake aondoke duh! Kusema ukweli mtaani mm naaminika sana lakini kwa hili tukio lingeniharibia mambo yangu, japo sikutoa kwa nia mbaya hicho kioo, nilikuwa naipambania familia isilale njaa siku ipite,

Baasi bhana akili ikiwa imeshavurugika nikaingia kwenye masimu mabovu kuna kioo ambacho niliamini ni kibovu siku zote leo ndo kimeniokoa na sekseke hili,
 
Kumbe hata wanaume wa mjini wana tamaa kama wadada wa bongo muvi?
 
Back
Top Bottom