Fumanizi la Pasaka

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
Na Dustan Shekidele, Morogoro
GUMZO wikiendi iliyopita ya shamrashamra za Sikukuu ya Pasaka mjini hapa, ni lile la bosi wa kiwanda cha maturubai aliyetajwa kwa jina la Daudi, kufumwa gesti akiwa na mfanyakazi wake ambaye ni mke wa mtu aliyetajwa kwa jina la Aisha.
Tukio hilo la aibu kwa bosi huyo lililoshuhudiwa na paparazi wetu, lilitokea muda mfupi kabla ya Pasaka majira ya saa 1:00 usiku ndani ya gesti maarufu iliyopo maeneo ya Sabasaba mjini hapa.
Habari zilizopatika eneo la tukio zilidai kuwa mzee huyo ana mazoea ya kufika mahali hapo na mwanamke huyo anayefanya kazi chini ya usimamizi wake ambapo huwa wanajiachia sehemu ya baa kabla ya kuingia ndani.
Siku ya tukio, 40 yao ilitimia baada ya wawili hao kutinga kwenye gesti hiyo na kujianika wakiponda raha.
Ilidaiwa kuwa wakiwa mahali hapo, kuna mtu alimuona Aisha ‘akidendeka' na mzee huyo hivyo akamjulisha mumewe aliyetajwa kwa jina la Mwinshehe.
Ilisemekana kuwa, baada ya kupokea taarifa hizo, Mwinshehe alipanga mikakati ya fumanizi ambapo alitinga kwenye gesti hiyo na kuhakikishiwa kuwa mkewe yupo ndani katika chumba chenye jina la Uganda ndipo alipoingia vitani.
Akiwa kwenye mvutano na wenye gesti waliomkataza kuingia, ghafla alimuona mkewe akitokea msalani akiingia ndani na ndipo alipovamia kwenye chumba na kumkuta mgoni wake ameshamaliza mchezo.
Baada ya kumuona mumewe, mwanamke huyo alianza kuangua kilio huku akisikika akisema, ‘Baba Nassoro nisamehe, makosa wamewekewa binadamu, sitarudia tena'.
Hata hivyo, Mwinshehe ambaye alikuwa na hasira hakumsikiliza zaidi ya kuwashushia kipigo ambapo yule mzee alishindwa kumudu mashambulizi baada ya kuzidiwa na kujikuta akichanika paji la uso, wenye gesti waliingilia kati na kuwatoa nje kisha wakafunga geti.
Baada ya hapo, timbwili zito lilihamia kwenye kituo kidogo cha polisi cha Kiwanja Cha Ndege ambapo baada ya kufika, Mwinshehe aliangua kilio alipowaona wakwe zake (baba na mama wa mkewe Aisha).
Aidha, wawili hao walitoa maelezo yao kituoni lakini hawakuelewana hivyo polisi waliingilia kati, wakaita gari la kuwapeleka kituo kikuu.
Katika hali ya kushangaza, wakiwa njiani, wahusika hao walielewana na kurudi tena kituoni hapo ambapo Mwinshehe aliwaeleza polisi hao kuwa ameamua kumsamehe mkewe hivyo ametaka mgoni wake, Daudi alipe faini ya shilingi elfu 70.
Mzee Daudi aligoma kulipa kiasi hicho akidai kuwa ni kikubwa na alipoulizwa ana uwezo wa kulipa fidia ya kiasi gani alidai
atalipa elefu 50
. Mwishehe alichukua kiasi hicho cha fedha na kuondoka na mkewe nyumbani.
fumanizi4.jpg

FUMANIZI.jpg

fumanizi21.jpg

fumanizi6.jpg
 
Ama kweli maisha magumu kweli mkeo anabanduliwa halafu una lipwa 50000 unalizika kabisa ni afadhali nimsamehe bure kuliko kupewa pesa.....
 
Nilichogundua ni kwamba mume ameonyesha udhaifu mkubwa sana.
Nadhani wakati anaenda kufumania alikuwa anawaza pesa, na wala hakuwa na wivu wala nini!
Ama kweli maisha magumu kweli mkeo anabanduliwa halafu una lipwa 50000 unalizika kabisa ni afadhali nimsamehe bure kuliko kupewa pesa.....
 
Ndoa zimekuwa bure kabisa siku hizi.

Siku akiishiwa anaweza mtuma mkewe kwa yule bwana ili mamfumanie tena.
 
DU!jamaa kaonyesha udhaifu mkubwa mno,kama ni mimi pesa sichukui naondoka na wife,au namuachia mke aendelee nae.kecho na keshokutwa akimfumania atapewa elfu kumi na kuambiwa leo sina kitu kabisa.
 
Au ilikuwa ni mchezo wa kuigiza tangu hapo awali (yaani jamaa ametegeshewa na mke anafahamu mchezo mzima)
 
mbona hio picha haioneshi kama ni wafumaniwa?? watu wako relaxed kabisaaa embu mcheki huyo mama ?lol
 
daah huyu mwanaume kiboko aisee. Kweli hivi ni vituko uswahilini.
Isijekuwa vijana wa mtaani kwake wakawa wamepata formula, wanamla mkewe akiwafumania wanampa 50000 anakaa kimya maana kaonesha kwamba anahusudu pesa kuliko mke.
 
Huyo hajakaa kimeneja wa kiwanda. Meneja anakuwa hivyo?
 
Ha ha ha haa, kuna mkuu hapo juu kanifanya mpaka nimepaliwa kwa kicheko..!! Eti kwamba kuna siku mkewe "atakatwa" afu jamaa atampa 10000/= na kumwambia kua leo sina kitu kabisa.!
 
Jamaa nimempenda katizama mambo ya msingi kwanza kajua mke kaishabanduliwa hakuna chakuzuia,pili kajua akunakilichopungua,tatu kaonakuleta vurugu asije akaozea jela bure mtu anakiwanda cha maturubai utashinda naye??Nne kaona nibora achukue mshiko kuliko kuuacha akaenda kulala njaa wakati walicha mtenda!!
 
na mashaka sana na hiyo picha,hamna sura ya kufumaniwa hapo zaidi ya ulevi..hembu muone huyo mzee ni kama mlevi anayejitahidi kuamka!!
 
Na kweli jamaa kachungulia mbali. Ameona akimwachia mwanamke wake aende tena rumande, atakuwa amewapelekea maafande mke wake wakam'banjue tena kwa upya. Umetumia akili ndugu yangu, wanaokucheka ni wale tu ambao hawakuona mbali, Big up man...
 
Ha Ha huyu jamaa kweli hajatulia mi naona angekomba fedha halafu anamwachia mke yeye anenda kusaka mwingine. inapunguza hasira bana kuliko kuendelea nae.
 
Back
Top Bottom