Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

SOMA MAJINA YA WALIOKULA FEDHA ZA AKAUNTI YA ESCROW KATIKA RIPOTI YA PAC INAYOSOMWA SASA BUNGENI.

Zitto: Upande wa viongozi wa kisiasa ambao waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mhe.
Andrew Chenge (Mb)

Zitto: Andrew Chenge aliingiziwa shilingi bilioni 1.6.

Zitto: Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa 62
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6.

Zitto: Mhe.William Ngeleja (Mb) na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4

Zitto: Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4.

Zitto: Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga
alipewa shilingi milioni 40.4

Zitto: Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7.

Zitto: Upande wa Majaji Prof. Eudes Ruhangisa, aliingiziwa milioni 404.25 na J.A.K Mujulizi aliingiziwa shilingi milioni 40.4

Zitto: kwa upande wa Watumishi wa umma,Ndg. Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa
shilingi milioni 40.4

Zitto: Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye
alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TIC) aliingiziwa shilingi milioni 40.4

Zitto: Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi wa TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8.

Zitto: Viongozi wa Madhehebu ya
Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu 63
Methodius Kilaini shilingi 80.9

Zitto: Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4 na Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4.

Zitto: Watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi,
mabox, magunia na lumbesa TegetaEscrow

Zitto: Bilioni 73.5
zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha
Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya 2006

Zitto: Taarifa
ya benki (bank statements) yenye majina na akaunti zote
zilizoingiziwa fedha zimeambatishwa.

Zitto: Kamati imebaini mawasiliano kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
 
Mi niko kwenye kampain ya kumbadilisha mama angu... maana anaipenda hiyo ccm sana......

na kama yupo dini hyo mpaka askofu ni kibaka nakushauri mbadilishe aisee unless otherwise. hii ni too much kwa kanisa na ni aibu though vatican ndo michezo yao.
cc ikhwaan
 
Last edited by a moderator:
Waziri na Naibu Waziri wa Nishati na Madini nao kitanzini...

Muhongo alikuwa dalali kati ya Sethi na JR...
 
Wakari tunaelekea 2015 chadema itafakari namna ya kuziba mianya yote inayoweza kuikosesha kura hâta moja wakati wa uchaguzi wa 2015. Miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na Zitto kurudishwa kundini kwa garama yoyote. Kwa muonekano wa dhahiri zitto ni mwana cdm halisi anayeipenda cdm kwa moyo wake wote. Zitto amejifunza na chadema imejifunza kitu Pia kutokana na yaliyototokea ndani ya cdm. Kwenye mkakati huo CUF imrudishe Hamadi Rashid Pia ili kulinda kura za hamadi na zitto zisipotee kwenye UKAWA. Kufanya hivyo ni sehemu ya mpango mkakati wa kukamata dola 2015. Nikimuangalia zitto ataisaidia sana cdm mbele ya safari. Chama kitumie its uncommon sensé kufanya uwamuzi huu mzito wa kikomavu
 
Back
Top Bottom