Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 118,265
- 219,500
Kuwa wa kwanza kufahamu kwamba, Viongozi wakuu wa CHADEMA, Tundu Lissu na Freeman Mbowe leo 06/12/2023 Wamebahatika kuwa miongoni mwa watu waliohudhuria Ibada ya mazishi ya Askofu Kweka .
Akizungumza kwa Taabu kwenye ibada hiyo kutokana na kujawa na Majonzi makubwa, Freeman Mbowe amemtaja Askofu Kweka kama sehemu ya familia yake, kutokana na kuwa karibu mno na Wazazi wake, huku akimtaja kwamba ndiye aliyemfungisha ndoa na ndiye aliyeongoza Mazishi ya Mama yake na Baba yake.
Mbowe amemtaja Baba Askofu Dr Kweka kuwa mfano wa kuigwa na kwamba matendo yake yatadumu milele.
Pia soma: TANZIA - Askofu Mstaafu wa Dayosisi ya Kaskazini ( KKKT) Dkt. Erasto Kweka afariki Dunia