Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,372
Wana body, amani iwe kwenu.
Taarifa za kuaminika ambazo intelijensia ya Lizaboni imepata ndani ya CHADEMA ni kwambaFreeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA na Katibu Mkuu Dr Slaa wanahujumu pesa ambazo zilitengwa kwa ajili ya kuendeshea Website ya chama ambayo ni Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo – Chadema. Kwamba, kiasi cha shilingi milioni 25 kilitengwa kila mwezi na mfadhili mkuu wa chama, taasisi ya Ujerumani ya CAS kwa ajili ya kuboresha mfumo wa kusambaza taarifa za chama kupitia website hiyo. Kwamba fedha hizo zimeingizwa kwenye akaunti ya chama na zinatolewa kila mwezi kwa maelezo eti zinatumika kulipa mishahara waandishi wa mtandao huo, kugharamia gharaza za simu, tozo mbalimbali na matumizi mengine.
Cha kushangaza ni kwamba, hakuna hata mwandishi mmoja ambaye anapokea mshahara kutokana na kazi ya kuandika kwenye mtandao huo. Inaelezwa pia kuwa kwa sasa mtandao huo hauna msimamizi maalum na inaelezwa kuwa Dr Slaa alisitisha ajira za vijana waliokuwa wanaandika taarifa kwenye mtandao huo mwishoni mwa Oktoba 2014 kwa maelezo kuwa mtandao unafanyiwa ukarabati. Miongoni mwa vijana ambao ajira zao zilisitishwa ni pamoja na Ben Saanane, Yeriko Nyerere, Michael Aweda na wengineo.
Intelijensia ya Lizaboni baada ya kupata taarifa hiyo ilijiridhisha kwa kutembelea mtandao huo. Ilichokikuta ni aibu tupu. Pamoja na mtandao kupambwa kwa rangi mbalimbali za CHADEMA, hauna taarifa mpya hata moja licha ya matukio mengi kutokea ndani ya nchi yetu. Tukio la karibuni ni sakata la AKAUNTI ya ESCROW ambalo lilipamba vyombo vyote vya habari hapa nchini. Cha kushangaza ni kwamba, kwenye mtandao huo wa Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo – Chadema hakuna mada yoyote inayohusu sakata la ESCOW. Uchunguzi wa Intelijensia ya Lizaboni umegundua kuwa taarifa tatu za mwisho ambazo zimewekwa kwenye mtandao huo ni hizi zifuatazo;
Kutokana na hali hiyo, fedha hizo wanagawana Mwenyekiti, FREEMAN MBOWE ambaye anapata mgawo wa shilingi milioni 8, Katibu Mkuu, Dr Slaa anapata shilingi milioni 7, Mkurugenzi wa Fedha wa chama, Anthony Komu anachukua shilingi milioni 5 na kiasi kinachobaki kinatumika kuendeshea blog ya chama ambayo ni chademablog.blogspot.com ambayo pia gharama za uendeshaji ni ndogo.
Hakika hii inatisha. Ni ajabu kubwa kwa watu wanaojifanya kuwa wanapinga ufisadi kumbe wao ni mafisadi wakubwa.
Bado tuna safari ndefu katika kupambana na ufisadi.
Nawasilisha

- SIRI ZA CCM KUHUJUMU KATIBA YA WANANCHI ZAFICHUKA ( Iliyowekwa tarehe 5/11/2014)
- TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA( Imewekwa tarehe 9/10/2014) na
- MKUTANO MKUU WA CHAMA KUMCHAGUA MWENYEKITI TAIFA LEO (imewekwa tarehe 14/9/2014)