Fredrick Mwakalebela aula, aitwa kuanza kazi shirika la makumbusho ya taifa

Shibalanga

Senior Member
Mar 1, 2011
178
93
Fredrick Mwakalebela aliyewahi kuwa katibu mkuu wa TFF na Mgombea ubunge wa Iringa mjini (CCM) kabla hajawekewa mizengwe ya rushwa, amepata kazi shirika la makumbusho ya Taifa (National museum of Tanzania) kuwa AFISA UTUMISHI NA UTAWALA MKUU, ama kweli kama wasemavyo waungwana Mungu akifunga mlango moja hufungua mlango mwingine cha muhimu ni kutokukata tamaa. kila la kheri Mwakalebela katika majukumu yako mapya.

Source: Mwananchi
 
Kwa nchi hii hilo lilitegemewa maana baada ya kuchakachuliwa aliombwa ajumuike kwenye Kampeni na ili baadaye apate kijikeki na Mungu siyo Jaxx kapata kakeki kidogo angalau apunguze machungu; Tunasubiri wengine hata wale wa Mwanza maana watapewa ubunge viti vya rais....jiulize kwanini mpaka leo wakuu wa mikoa hawajateuliwa then ujiongeze....tunajipanga kulipa fadhili kwa umakini kabisa maana hii ndiyo kete yetu ya mwisho
 
Maajabu ya kikwete na ajira za mafisadi wenzie hayaishi
huyu naye ni gamba gumu maslahi binafsi
kumbe zile kesi ilikuwa ni kupoteza muda wa mahakimu na TAKURUKU
kutudanganya wananchi kwamba wanafanya kazi,

mbona kesi kashinda fasta na kazi kubwa tena kitengo muhimu
 
Ikiwa TAKUKURU walimpeleka mahakamani kwa tuhuma za rushwa basi wao ndo walikurupuka na hawakuwa na ushahidi wa kutosha au basi wakubali walitumiwa ili kumdhoofisha ili asiweze kugombea tena, nadhani CCM makao makuu na yule mama Monica Mbega ndo wa kulaumiwa kwa hili kwani wao ndo watakuwa walichora mchoro huu, lakini mimi nasema malipo ni hapa hapa Duniani, ndo maana hata yule mama naye hakupata hata huo ubunge wenyewe.
 
Maajabu ya kikwete na ajira za mafisadi wenzie hayaishi
huyu naye ni gamba gumu maslahi binafsi
kumbe zile kesi ilikuwa ni kupoteza muda wa mahakimu na TAKURUKU
kutudanganya wananchi kwamba wanafanya kazi,

mbona kesi kashinda fasta na kazi kubwa tena kitengo muhimu
Kwani unafikiri kapewa hiyo kazi bila usaili, msimwtike kila zigo Mzee JK, hilo nadhani ni suala la kazi ilitangazwa, na akaomba aka sailiwa na kuonekana nibora miongoni mwa wasailiwa. Ingekuwa kateuliwa na rais, labda tungeweka shaka lakini kwa hili acha umbea!!!
 
Acha kupotosha bana.........

Mwakalebela alishinda kesi ya TAKUKURU kihalali na si fasta kama unavyodai,kesi imechukua karibu miezi 8 wewe unasema kashinda fasta?,kesi yenyewe ya kudaiwa kutia rushwa ya Tshs.100,000/=!!!!!!!!!!...

Kuhus ajira,usiseme kwamba Mwakalebela amepewa,huu ni upotoshaji pia,Makumbusho walitangaza ajira kwenye magazeti na sehemu nyingine na watu wakaomba(akiwemo Mwakalebela),usaili ulifanyika na Mwakalebela akashinda.Kumbuka kwamba Mwakalebela ni msomi kwa kiwango cha shahada ya pili ya uzamili ya utawala wa biashara(MBA) na kabla hajawa Katibu mkuu wa TFF alikuwa ni Afisa utawala wa kiwanda cha mtibwa kule Manungu kwa kipindi kirefu tu so anazo sifa za kutosha kupewa nafasi hiyo na si kwamba kapewa kama unavyodai wewe.....

Bala.
 
Hongera Mwakalebela unastahili kutokana na ujuzi wako na shule yako....fanya kazi jipange upya 2015 iringa yako tu
 
Kwani unafikiri kapewa hiyo kazi bila usaili, msimwtike kila zigo Mzee JK, hilo nadhani ni suala la kazi ilitangazwa, na akaomba aka sailiwa na kuonekana nibora miongoni mwa wasailiwa. Ingekuwa kateuliwa na rais, labda tungeweka shaka lakini kwa hili acha umbea!!!

mkuu nami naungana na wengi kumpongeza kwa kupata ajira mpya. Tangu mwez wa 4 alipoitwa kwa usaili niliwai kuandika apa jf kuwa lazima akwae icho kitengo kutokana na sifa alizonazo mwakalebela. Ila sikusita kutoa dukuduku pia kuwa iyo nafasi kawekwa,haijalishi kaombaje. Hii ni kwa kuwa haiwezekani mtu alikuwa ana kesi ya kujibu dhidi ya uyo mwajili mpya ila apo apo anatoka mahakamani kujibu kesi anaenda usaili National museums. Jina lake lilipitisha hata kabla hajashinda kesi,kitu kilichozua hisia kali kwa watu makini. Yani ni sawa na Jerry Muro sasa ivi alivo na kesi ila anaitwa kwenye interview mfano kuwa mkurugenzi wa Tbc1 shirika la uyo uyo anayekushtaki. Hapa watu makini walijadili hapa hapa jf kuwa kesi ya rushwa ya uchaguz ilikuwa usanii,pili walijua lazma awe huru alaf aende pale national museum. Siipingi ajira ya ndugu mwakalebela ila skeptical senses zilishajionesha mapema. Hongera ndugu Fred Mwaka.
 
Kwani unafikiri kapewa hiyo kazi bila usaili, msimwtike kila zigo Mzee JK, hilo nadhani ni suala la kazi ilitangazwa, na akaomba aka sailiwa na kuonekana nibora miongoni mwa wasailiwa. Ingekuwa kateuliwa na rais, labda tungeweka shaka lakini kwa hili acha umbea!!!

Acha kutuzuga nani asiye ijua serikali ya nchii unaitwa kwenye interview just kutimiza wajibu lakini mtu anakuwa ameishapangwa the same tu huyo mwakalebela kuna mkono wa jk hapo no doubt. Siku zinakuja mambo ya kulipana fadhila yatakomeshwa shame on you magambaz
 
Fredrick Mwakalebela aliyewahi kuwa katibu mkuu wa TFF na Mgombea ubunge wa Iringa mjini (CCM) kabla hajawekewa mizengwe ya rushwa, amepata kazi shirika la makumbusho ya Taifa (National museum of Tanzania) kuwa AFISA UTUMISHI NA UTAWALA MKUU, ama kweli kama wasemavyo waungwana Mungu akifunga mlango moja hufungua mlango mwingine cha muhimu ni kutokukata tamaa. kila la kheri Mwakalebela katika majukumu yako mapya.Source: Mwananchi
Hakuna cha kufunga wala kufungua mlango hapo. Huyo bwana amepewa hiyo kazi na chama chake. Hana proffesion yakumuweka hapo. Kabebwa!
 
Nchi hii fedha zinachezewa, kila siku kesi zinaendeshwa halafu mwisho wake serikali inashindwa
Maajabu ya kikwete na ajira za mafisadi wenzie hayaishi
huyu naye ni gamba gumu maslahi binafsi
kumbe zile kesi ilikuwa ni kupoteza muda wa mahakimu na TAKURUKU
kutudanganya wananchi kwamba wanafanya kazi,

mbona kesi kashinda fasta na kazi kubwa tena kitengo muhimu
 
Hii ndio bongo bana, kwa chama cha magamba huwezi kukurupuka tu na kusema nagombea ubunge, lazima upitie hatua fulani fulani kufikia kwenye kugombea ubunge, haya apige kazi huko tutasikia tena ni wapi atapelekwa baada ya hapo safari ya ubunge ndio hiyo iko njiani kwa huyu jamaa
Fredrick Mwakalebela aliyewahi kuwa katibu mkuu wa TFF na Mgombea ubunge wa Iringa mjini (CCM) kabla hajawekewa mizengwe ya rushwa, amepata kazi shirika la makumbusho ya Taifa (National museum of Tanzania) kuwa AFISA UTUMISHI NA UTAWALA MKUU, ama kweli kama wasemavyo waungwana Mungu akifunga mlango moja hufungua mlango mwingine cha muhimu ni kutokukata tamaa. kila la kheri Mwakalebela katika majukumu yako mapya.

Source: Mwananchi
 
Mwakalebela na ujuzu gani na mambo ya kale/makumbusho? Yeye ni curator? Amesoma anathropology? or histrory? or anything close na makumbusho? Nahisi hii nafasi anaweza akawa amepewa kwa utashi wa kiasi, na hofu yangu ni kwamba Serikali achalia mbali Mwakalebela haiwaelewi fani hii ya makumbusho, na mbaya zaidi hawatambui 'potentials' za makumbusho kwenye uchumi wa Taifa!

Nasema haya kwa sababu kubwa moja, ukitembelea jumba la makumbusho ya Taifa Dar es Salaam utaona how 'shallow it is' kuna vitu vingi sana bado hajikuwepo, na hata mazingira yake yamekaa hovyo hovyo pamoja na kwamba hela za misaada zimekuwa zinatolewa. Balozi wa EU hapa nchini (Tim Clarke) kwa muda alijitahidi sana kuonana na aliyekuwa mkuu wa makumbusho (Dr somebody) lakini kwa maajab ya musa kila walipopanga meeting huyu bwana mkubwa wa makumbusho akawa hatokezi na akipigiwa simu anasema 'kasahau'!!! Balozi Clarke alitaka ku-discuss namna ya KUSAIDIA kuinua hadhi ya jumba la makumbusho na kwa bahati nzuri mke wa Balozi (Mrs Clarke) kasomea mambo ya kale.

Lile jumba pale mjini limekuwa na uzio wa mabati for years, ni marekebisho gani hayo yasiyoisha. Ukiingia ndani mambo hayajaa vizuri both presentation & contents wise. Ukitembelea mikoani suala zima la makumbusho ni kama hakuna kabisa. Sasa Mwakalebela anaweza akawa na jibu la kuridhisha kuhusu 'neglect' ya makumbusho Tanzania? tusubiri.
 
Back
Top Bottom