Francis Cheka amchekesha Nyilawila ulingoni

Bumpkin Billionare

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
1,332
621
Huu mchezo wa kupenda kupiga domo kwenye vyombo vya habari unaofanywa na mabondia wa hapa nyumbani pindi wanapoomba pambano na dume la milima ya Uluguru utaisha lini?

Jana, Karama Nyilawila amepata zawadi ya kuropoka baada ya kukong'otwa TKO ya round ya 6 katkia pambano la masumbwi lililofanyika kwenye ukumbi wa PTA kurasini DSM dhidi ya Francis Cheka.

Awali Karama Nyilawila alijigamba (kama ilivyo ada ya mabondia wote wenye njaa) kuwa Cheka hana ubavu wa kumshinda na hata pambano alilopigwa Moro Cheka alipendelewa tu na majaji.

Sasa jana ndio alijua kwa nini mfuko wa Rambo haubebewi kaa la moto. Round ya 6 kalamba sakafu, refa kahesabu mpk mia, hajaamka.

Chezea CHEKA wee, waulize ukoo wa Matumla, mpk wakastaafu ngumi.

Promota Bumpkin Billionare nataka orodha ya mabondia uchwara wote wanaotaka kupigwa (na sio kupigana, Cheka hapigani) na Cheka wajiandikishe ili niweze kuandaa ratiba ya wao kupigwa.

Cheka hoyeeeeeee!

cheka.JPG cheka3.JPG

Madam Maugo asijiandikishe, ameshapigwa vya kutosha awaachie na wenzake nao wapigwe
 
Last edited by a moderator:
Cheka akawanie mikanda mikubwa tumuone anajua otherwise hata ampige Matumla mara ngapi Matumla atabaki kuwa Legendary! Kila siku ngumi na mateja! akitoka nje ya nchi anakula kibano!
 
Huyu Cheka ana kama miaka kumi hivi mfululizo sijasikia amepigwa!
Kama Tanzania ingekuwa inajali kila mchezo, bila shaka huyu Cheka angeipa sifa nchi yetu!
 
chezea cheka ww Halafuuuuuuuuuu....kaka...ww Mbayaaaaaaaaaaaaaaaaaa............................
 
sasa cheka anajisifu kwa kupiga vilema....atoke nje sasa tuone kama ana huo ubavu.
Matumla ni legend wa ngumi hapa nchini....sasa kajichokea bado cheka anampiga matumla kwa shida....
 
Hivi huyo cheka nae mbna hapganagi na watu wa nje.. Yeye daily anaishia kuwaonea vijana wa keko

Ashapigana mapambano kadhaa huko nje na yote kapigwa....huyu jamaa sio bondia aisee...jaribu kuangalia mapambano yake utakubaliana na mimi.....kamkimbia rasta kaseba wakamfuata huyu muuza karanga ili kumuongezea point cheka...boxing tanzania iliishia na akina matumla basi......
 
mkuu una maanisha anaweza kuwa anatumia mambo ya wahenga kushinda mapambano!!!huenda eeee!!
 
Huyu Cheka ana kama miaka kumi hivi mfululizo sijasikia amepigwa!
Kama Tanzania ingekuwa inajali kila mchezo, bila shaka huyu Cheka angeipa sifa nchi yetu!

Haya ndio ya kuongea mkuu! Lkn kudhani cheka anaweza kwenda mwenye tu njea ya nchi na kuanza kupigana, ni wazimu!
 
Tatizo hakuna anayekubali kufanya kwa maslahi ya Taifa, kila mtu anachunguliwa maslahi binafsi kwa kila jambo! Hawataki kumuunga mkono Cheka kwa sababu hawaoni namna ya kumnyonya, kwa hiyo wanamuacha tu amalize kipaji chake hapa hapa hadi atakapozeeka na kufa maskini.
 
Kaka ndondi sio kucheza marede....cheka sio bondia ...period...yeye na mchumia tumbo wote wabeba viazi sokoni....ndondi tanzania inabakwa na viongozi wa vyama vya ndondi ....wanafanya kama miradi yao....ukiona mtu anapigana kibongobongo jua kuwa kakosa kazi nyingine ya kufanya....vijana wadogo hawaandaliwi kama matumla alivyoandaliwa na baba yake toka utotoni ndio maana mpaka kesho ndio bondia pekee aliyekuwa na ubavu wa kucheza mapambano makubwa nje na kurudi na mikanda...cheka hata umri ushamtupa nje....miaka 30 ni umri wa kustaafu
 
Kwa bahati nzuri nilipata bahati ya kushuhudia mapambano yote waliyowakutanisha Cheka na Matumla, kiasi kwamba unanipa wasiwasi ndugu yangu kwa unavyosema kuwa Cheka sio Bondia, ila Matumla ndio Bondia.
Cheka ni mmoja wa Mabondia wachache nchini wanaopigana kwa kutumia akili sana wawapo ulingoni, na kubwa zaidi ana ngumi kali, na hili suala la Cheka ngumi kali hata Matumla amekiri mara nyingi ninapozungumza naye.
Labda tatizo lililopo ni kuwezeshwa tu kwa Cheka (au mchezo mzima wa ngumi nchini), ukiwa ni uwezeshaji ambao ungemfanya Cheka azidi kuwa bondia mkali na kuipa sifa Tanzania katika medani ya michezo.
Niweke wazi kwamba, sikuwahi kufurahia mapambano ya ngumi nchini kama nilivyofurahia mapambano yaliyowakutanisha Cheka na Matumla, hasa lile lililopigwa pale Luxury Pub, Tandika!

Omba Mungu, Matumla awe fiti tena halafu liwepo pambano lake na Cheka, nitataka sana mimi na wewe tukae kwenye viti vilivyo jirani tukishuhudia pambano, ukumbi huwa kimya wakati fulani na sauti pekee inayosikika huwa ni ngumi tu.
 
mkubwa sasa mbona unachekesha....cheka alipigwa na matumla enzi hizo matumla wa ukweli kabla hajazeeka na kuchoka....cheki rekodi ya cheka utaona pambano lake la kwanza kupigwa....matumla sasa hivi kachoka vibaya sana hata wewe unaweza kumpiga....ni kama tyson alivyochoka sasa ......mimi nataka cheka akapigane nje sio kuchagua wauza karanga kujiongezea pointi.......nitamkubali akishinda angalau mapambano matatu tu ya nje na sijui itakuwa lini maana jamaa na yeye umri ushamtupa mkono....
 
Hivi huyo cheka nae mbna hapganagi na watu wa nje.. Yeye daily anaishia kuwaonea vijana wa keko

Mikanda anayo yeye, kama kuna mtu anautaka ajilete aje kupigwa. We kama unaye bondia wako hajapigwa siku nyingi mwili unamuwasha we mlete aje kuchakaa
 
mkubwa sasa mbona unachekesha....cheka alipigwa na matumla enzi hizo matumla wa ukweli kabla hajazeeka na kuchoka....cheki rekodi ya cheka utaona pambano lake la kwanza kupigwa....matumla sasa hivi kachoka vibaya sana hata wewe unaweza kumpiga....ni kama tyson alivyochoka sasa ......mimi nataka cheka akapigane nje sio kuchagua wauza karanga kujiongezea pointi.......nitamkubali akishinda angalau mapambano matatu tu ya nje na sijui itakuwa lini maana jamaa na yeye umri ushamtupa mkono....

Acha ubwege na jealous wewe, bondia hachagui anachaguliwa na promoters. Wewe andaa pambano uone kama hupigwi wewe na huyo bondia wako. Hawa wachonga mdomo wenyewe wametaka kupigwa. Na kama mabondia wa nje angalia vizuri hiyo list yako, labda tu kwa kuwa ukoo wa Matumla ulipigwapigwa na huyu jamaa ndio inakuuma
 
Back
Top Bottom