Forbes Yatoa Orodha ya Mabilonea 50 wa Afrika...Rostam Aziz aibeba Tanzania

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Jarida maarufu la Forbes limetoa orodha ya mabilionea 50 (matajiri) wa Afrika wakiongozwa na Aliko Dangote.

Katika Tanzania,Rostam Aziz anashika nafasi ya 27 kwa Afrika na nafasi ya kwanza Tz akiwa na utajili wa thamani ya dola bilioni moja,akifuatiwa na Reginald Mengi aliye wa 34 Afrika na utajili wa Milioni 550;Mohamed Dewji na Said Bakheresa wanashika nafasi ya 38 Afrika wakiwa na utajili wa dola milion 500.

Mo Dewji amevunja rekodi ya kuwa bilionea kijana kuliko wote,akiwa na miaka 38 tu. Ajabu ni kuwa hata Forbes wameshindwa kupata picha ya Said Salim Bakheresa ili kuiweka ktk kumtambulisha,na wameishia kuweka picha kivuli tu
 
Siwezi kamwe kujisifia kwa kuwa na tajiri mwizi, zulumati na fisadi kuu la nchi ya Tanzania ROSTAM.

Uporaji na ufisaji wake kwa jicho la tatu umechangia maafa na mateso makubwa kwa watanzania kadhaa kuikosa huduma bora za elimu na afya.
 
Rostam Ana utajili wa USD Billion 1.1 mkuu. Rudia pale Forbes utaona. Kwa sasa anapunguza kiasi cha share zake pale Vodacom na kuwauzia Vodafone ya Uingereza kwa bei ya juu zaidi,kitu ambacho kinaweza ongeza utajiri wake.
 
Hamna transparency kwenye utajiri wa wa-Tanzania ndio maana utaona Mengi kampita Bakhresa, lakini kiukweli hela za majini zinalipa kuliko hela za unga
 
hapa kuna kitu ambacho sijui sikielewi ama ni uvivu wangu wa kufikiri???

eti mimi naona ni sahihi kabaisa kwa Rostam kuwa bilionea wa kwanza Tanzania kwasababu ya aina ya bishara zake, kama aliweza kufilisi tanganyika packers na mpaka leo wewe mbuzi wako ukimchinja kijijini yeye ndo anaye nunua ngozi yako kwa sh 200 na kiuza sh 6000 kwa kg unafkiri ataacha kuwa tajiri??

mwache aende mbali zaidi mtanzania gani anayesafirisha pamba na kahawa nje ya tanzania zaid yake?? Mengi katokea Moshi kahawa inayozunguka nyumba yake mwenyewe inasafirishwa na rostam.

bakhressa naye kateka soko la vyakula na kiukweli kati ya wote hawa anayefanya bishara inayomgusa mtanzania per se ni yeye lkn hawez kumpiku rostam manake yy hadin akusanye sh 1000 zifike billion ni leo??
 
Hamna transparency kwenye utajiri wa wa-Tanzania ndio maana utaona Mengi kampita Bakhresa, lakini kiukweli hela za majini zinalipa kuliko hela za unga

cjakuelewa kiongoz hapa. ila nachojua Mengi hapo juz kat alinunua migodi halafu imetema mbaya. hapo ndipo alipompiku Bakheresa
 
Hv wanasiasa huwa hawaesabiki au? Kwa maana mimi ninaamini hao wote hamzidi m2 anaitwa NIMROD MKONO mbunge wa musoma vijijini pamoja na EDWARD LOWASA!
 
Back
Top Bottom