Kabwela
Member
- Feb 11, 2008
- 76
- 5
Juzi mchani nikiwa natoka kibaha kwenda mjini Dar nilikwama njiani eneo la kibamba CCM kwa muda wa saa 3. Jana jioni nikiwa natoka kibaha kwenda kiluvya madukani imenichukua saa 2 (mita 800) kwa gari kutokana na msongamano wa magari. Inaanza kuzoeleka kuwa kukitokea tatizo lolote maeneo hayo inakuwa na usumbufu kwa kila anayetumia barabara ya morogoro. Nauliza haya maandamano (foleni) ndio mazoezi ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru au ndio maisha bora yenyewe. Ukiuliza hivi kina.... Watasema mmetumwa na.... wengine watasema mnamsakama JK. Nashauri wanaohusika na barabara hii kuu ya nchi watengeneze njia za kuchepuka (service roads) kukitokea matatizo na hii inatuaibisha pia kwa majirani zetu wanaotumia bandari zetu. Nawasilisha