Flip flopping in Oil and Gas contracts

duh...na huyu naye keshawekwa mfukoni!!!kweli huwezi kushindana na boss aliyekuteua maana jk ana interest nyingi sana kwenye uwekezaji wa FDI's humu tz,.kama amelainika hivi basi tutegemee mgao soon na yeye kuwaomba msamaha TANESCO kama wale wachumia tumbo interns
 
Kuna sheria ya utafutaji mafuta ya mwaka 1980 ambayo ina mapungufu makubwa sana. Hatuna Sera ya Gesi Asilia. Hatuna Mkakati (natural gas masterplan) na hatuna sheria ya matumizi ya fedha zinazotokana na mafuta na gesi.

Ndio kwa sasa tunapinga kugawiwa kwa vitalu vipya mpaka tumalize nyaraka hizi muhimu sana kwa nchi yetu. Vile vile tunatakiwa kumaliza ukaguzi wa gharama za utafutaji zinazofanywa na haya makampuni.

Kimsingi ilipaswa kusimama kufanya lolote kwa sasa maana unafanyaje mambo haya bila sera na sheria madhubuti?
Mkuu wangu umemaliza..Hivyo sioni kabisa sababu ya uwazi, Usiri wala kutoa ahadi zisizowezekana isipokuwa kuzuia kabisa mikataba mipya hadi pale vitu hivi vitakapo wekwa sawa na wazi...
 
Kuna sheria ya utafutaji mafuta ya mwaka 1980 ambayo ina mapungufu makubwa sana. Hatuna Sera ya Gesi Asilia. Hatuna Mkakati (natural gas masterplan) na hatuna sheria ya matumizi ya fedha zinazotokana na mafuta na gesi.

Ndio kwa sasa tunapinga kugawiwa kwa vitalu vipya mpaka tumalize nyaraka hizi muhimu sana kwa nchi yetu. Vile vile tunatakiwa kumaliza ukaguzi wa gharama za utafutaji zinazofanywa na haya makampuni.

Kimsingi ilipaswa kusimama kufanya lolote kwa sasa maana unafanyaje mambo haya bila sera na sheria madhubuti?

Sasa mkuu unasema hizi hatua za Muhongo zita discourage direct investment(jambo ambalo ndo nadhani wamemchimba nalo biti Muhongo akabadili mawazo),na wakati huo huo unakiri hatuna sera ya gesi asilia wala "mkakati(natural gas masterplan)?Halafu unasema transparency ndo solution?

Na hilo la kutokuwa na sheria ya matumizi ya pesa zinazopatikana kutoka kwenye mauzo ya mafuta na gesi,kama sijakosea,Muhongo alilizungumzia na akasema pesa hizo zisipelekwe hazina kwasababu zinachanganywa na pesa nyingine na kuchakachuliwa.

Hayo ni baadhi tu ya matatizo aliyoyaona,nina imani transparency siyo solution,maybe just a part of it,kama hatuna hata sera zinazosimamia hayo mambo,then transparency is realy a "none issue"
 
Kuna sheria ya utafutaji mafuta ya mwaka 1980 ambayo ina mapungufu makubwa sana. Hatuna Sera ya Gesi Asilia. Hatuna Mkakati (natural gas masterplan) na hatuna sheria ya matumizi ya fedha zinazotokana na mafuta na gesi.Ndio kwa sasa tunapinga kugawiwa kwa vitalu vipya mpaka tumalize nyaraka hizi muhimu sana kwa nchi yetu. Vile vile tunatakiwa kumaliza ukaguzi wa gharama za utafutaji zinazofanywa na haya makampuni.Kimsingi ilipaswa kusimama kufanya lolote kwa sasa maana unafanyaje mambo haya bila sera na sheria madhubuti?


hivi watanzania bado mnaamini kuwa tatizo kubwa la tz ni sera mbovu??.......la hasha....mi bado naamini kuwa tatizo kubwa la tz ni watu wake......hata tukiwa na sera nzuri namna gani....kama watanzania hawatabadilika bado haitasaidia kitu.......maana wanaosimamia sera ni watu....hata kama sera ni nzuri namna gani....watu wabovu watapindisha sera....na hili ndo tatizo namba moja la tz.....Infact..tz kuna baadhi ya sera wala hazina shida(on paper)..lakini utekelezaji wake ndio umekua tatizo kubwa....mfano.....chukua master plan ya mji wa dodoma.....ile ndo iliyotumika kuijenga Abuja.....lakini hapa tz...mijamaa wa ccm wanaipiga danadana....na bado wanang'an'ngania kubaki madarakani....

Mimi naona mh Zitto..kuliko ubaki kujibu hoja za mawaziri wa ccm....ni bora nyie chadema mpambane na juhudi za kuwaamsha watanzania wajue jinsi wanavyoibiwa na watawala.....ili itakapofika wakati wa uchaguzi watanzania wafanye maamuzi magumu ya kuwatoa watawala hawa...ili hata mkija na sera nzuri muweze kuzisimamia......maana kilio chenu chadema dhidi ya watwala wala hakiwanyimi usingizi........Fanyeni hima piteni nchi nzima tangazeni ukombozi wa mtanzania...watu wabadilike kifikra ili waweze kujua na kudai sera nzuri.....maana haki ya mtanzania inaporwa kuanzia hata kwenye utekelezaji wa katiba.....watanzania leo wanaambiwa watoe maoni kuhusu katiba mpya...lakini ukweli ni kwamba hata katiba ya zamani hawaijui......kwanini hawaijui?????

wakati nchi imetawaliwa kwa miaka 50!!!....Kwa hiyo hii maneno ya flip flopping itaendelea nchi hii mpaka pale ambapo hawa watawala wataondoka madarakani.......Shime shime zitto.....nyie kama viongozi wa chadema kuweni pamoja.....tena kama mnatofauti zenu...ondoeni.....toeni elimu kwa watanzania wajue haki yao ya uwazi kwenye mikataba n.k n.k.......hii ndio italeta ukombozi wa kweli kwa mtanzania..otherwise..it will also just look like flip flopping with the rulers......Just my thinking.......
 
Ha ha ha!! Our leaders say one thing to their 'people', and completely another thing to their 'masters/mistresses'. We go by context, not by principle. There is no shortcut to change. If we need change we should work towards it in a comprehensive manner. If we think change will come by having a few vocal ministers in a few ministries, we are doomed. It is the system that is failing us, not necessarily individuals. Tuamke na kuacha kushangilia mafanikio hewa!!
 
Naona watu wameshtuka kusikia "rafiki" yangu sana ana mafuta huko L. TANGANYIKA. Inabidi mrudi kidogo nyuma kwrnye ile Executive Outcome na offshoot zake. Kuna thread iko kwenye Intelligence itawasaidia.
 
Mheshimiwa sometimes as a politician its not very nice to take things so personal and you are very much expected to control emotions....I am not him but this is character assassination and has nothing to do with the existing discussion kwani he is not the subject matter ingekuwa Mhongo it could have been right....

Pole dada hakumaanisha kwa ubaya. Ali assume watu wanafahamu issue ya Heritage Gas and Oil...
 
Zitto
Jibu lako ni rahisi mno. Mwekezaji kwanza mmempa mgodi and 80%; halafu anaenda kukopa Pesa Bank ya China. At what interest rate? we don't know.

Investment yake ni USD 2 billion; that is big money. Machimbo hayana infrastructure yoyote ile, mie navyoona hawa jamaa wanaweza kumiliki mgodi huu hadi mwisho wa Dunia kwa kuwa kama Mwekezaji atashindwa kulipa basi ile ardhi itanyang'anywa na Bank ya China kwa sababu siyo mwekezaji ndiye ame-guarantee, bali ni ule mgodi ndiyo ume-guarantee huo mkopo.

Kwa maana nyingine ni kuwa sisi waTanzania mabwege, ardhi yetu, guarantee ni yetu, risk yote ipo kwetu.

Zitto hebu twambie shipment kiasi gani za iron ore hiyo itachimbwa na kuwa exported na kurudisha fedha zote hizo? Mie naona hata feasebility study hiyo ingewekwa ioneshe uwazi. Ule mradi kurudisha pesa ni ndoto. Tazara hadi leo haijalipa.

Please we need more explanation, especially those numbers. In China Sichuan Hongda is not a professional Iron and Steel maker neither iron ore mining company. Is really not known in steel Industry. They are professional Non Ferrous zinc miners (Zinc). How you were duped there? Discarding away offers from BHP Billiton and Rio Tinto?
Mkuu umepotea sana lakini tunashukuru umerudi kuchangia,usipotee sana mkuu.

Hayo hapo juu uliyoyasema yamekuwa possible only kwasababu kuna waliopokea mlungula.Hizo dola bilioni 2,kuna waliowekewa kwenye akaunti mkuu,na ndiyo maana ni siasa tuu!

Very sad kwakweli!
 
We are learning,"Muhongo said.

Ebo, sasa huyu mtu anaitwa profesa na anasema bado anasoma! Heri amwachie mwingine aliyehitiumu badala ya kuflip flop katika mambo haya!
Kusoma na kujifunza hakuna mwisho,dont be that shallow minded.Umesharudi kule nilipokuwekea zile links?
 
As long as CCM itaendelea kuwa madarakani, hatuna budi kusimamisha shughuli zote za kuingia mikataba mipya ya uchimbaji madini, gesi na uvunaji maliasili nyingine in large scale. Udhaifu wa kiuongozi tuliokuwa nao aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya, ume-create kundi la wapigaji kwenye sekta zetu zote za maliasili. Kundi hili la wapigaji, kwa makusudi kabisa na wakiwa na akili zao timamu, huingia mikataba famfa na wawekezaji huku wao wakipewa mafungu yao ilhali wakijua kabisa kwamba nchi yetu haitafaidika lolote na uwekezaji huu.

Ni mabadiliko ya kimfumo wa uongozi tu, toka ngazi ya juu kabisa ya Urais mpaka ngazi ya chini ya watendaji wa serikali, ndio yatawezesha rasilimali zetu kutumika kwa manufaa ya watanzania wote. Lakini kwa hali iliyowekwa na mfumo uliopo ya 'everybody for himself' hata tukiwa na sera, sheria na hata masterplan, hawa hawa papasi waliotawala kwenye mfumo uliopo wataendelea kuwanyonya watanzania na kuneemesha matumbo yao. Mambo mengi mabaya yanayotokea dhidi ya maslahi ya nchi yetu, si ya bahati mbaya bali ni ya kupangwa kwa makusudi maalumu ya kinyonyaji na wapigaji waliojaa kwenye mfumo wetu wa sasa. Dawa ni ku-overhaul huu mfumo.
 
Kwenye kuhakikisha tunawekeza kwenye makaa ya mawe na chuma kule Ludewa kamati yangu ilitoa pendekezo kwamba mwekezaji akisharudisha mtaji wake anaoweka basi umiliki utakuwa 49% kwa Tanzania na 51% kwa mwekezaji na kwamba kampuni pia itakuwa listed kwa kila upande kutoa 10% kuingia sokoni. Haya ndio makubaliano na yamo kwenye mkataba. Tulifanya intervention at the right time na tukafanikiwa.

Hata hivyo ni vizuri mkataba huu ukawa wazi pia wananchi waweze kuuona ili kuondokana na hisia kama hizi.

Na makisio ya muda wa kurudisha Mtaji wake ni miaka mingapi? Kwa sababu hivyo ni vitu lazima viwe vimekisiwa kuanzia Mwanzo.
 

Ushauri wangu kwa mh. Zito,
Kwa kweli aidha kwa kujua au kutokujua, tumechonganisha serikali na wawekezaji ili waone TZ sio mahali sahihi pa kuwekeza.
Zito unaongea sana, usipodhibitiwa utaicost nchi. Lazima mambo nyeti kama haya yawe na mipaka. Busara inahitajika ktk jambo hili. Binafsi nadhani kuna haja ya Mh. Rais wetu J.M Kikwete kuliangalia suala hili objectively. Kwa Jinsi inavyoonekana prof akiamua kitu unamzunguka kwa wawekezaji wanakuja juu na unatumia sana media. Nina Hakika wazungu WANATUCHEKA.

Ushauri wangu, wizara hii ndio imeshikilia uchumi wa nchi, hivyo basi kuna haja CDM bila kujali itikadi yenu, Kama mlivyofanya Wakati wa issue ya mabadiliko ya Katiba mkamuone raisi. Please address this issue in the right forums kwa kuzingatia unyeti wake, it is not one man show, kamwe Hilo halijengi na watz hatulitaki tunataka kutoka hapa tulipo.

Hivi vita vya Zito na Prof vinaicost nchi na watanzania kwa ujumla. Vita hii naifananisha na chupa ya coca cola kwenye sinema ya god must be crazy ilivyowagombanisha.
Mungu ibaraki Tanzania, Watu wote bila kujali dini tuiombeee nchi yetu, hapo ndipo ukombozi wa kuangamiza umasikini ulipo. Ardhi ndio Urithi wetu kamwe haitakuwa laana Bali itakuwa baraka kwetu.
Queen Esther
 
Huyu Waziri mimi sigombane naye nini? Sina jambo la kugombana naye. Mimi ni Mbunge wa upinzani na kazi yangu kubwa sana ni kuonyesha kuwa CCM na Mawaziri wake wote hawawezi kuongoza nchi yetu kwa manufaa ya wananchi. Pia sipendi mtu awafanye Watanzania mabwege. Anajua kabisa kwamba hawezi fanya asemacho lakini anasema tu ili kuonyesha kuwa Serikali ya CCM inafanya kazi wakati haifanyi kazi. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye sekta ya Madini na miaka kumi tukawa tunafanya kazi ya ku review tu lakini dhahabu inasombwa. Hili ndio ninalolikataa

Anachosema Zitto ni kweli tulikalia kulumbana kwa miaka kumi kwenye madini Barrick walipoona watz wameshtuka wanatuambia mali imeisha Tulawaka gold mine mara wanauza mgodi kwani tax heaven yao imeisha sasa wanamwachia Mchina aje apambane Barrick si walikuwa wanasema wanapata hasara migodi minne tu waliyoiuzia China wanakwambia ni one of the bigest deal in London top 250 stock exchange sasa hapa tutamwona Zitto mbaya kumbe anatuamsha kabla mikataba hawa majambazi ya ccm hawajaiseal.
 
ngoja nikamue kwanza sheria za mafuta na gesi ndio nije kuchangia.

lakini, unaweza sitisha utafiti?

Kwa nini utafiti usiendelee halafu uchimbaji ndio usubiri hiyo 'masterplan'?

Hivi kuna uchimbaji bila utafutaji?? Continuation itakuwaje?

Hivi utafutaji wa gas na mafuta unatumia muda gani kwa wastani kuanzia grass root projects hadi iwe advanced project??

Kama gharama za vitalu zimepanda kinyemela hivi karibuni, kwa nini hivyo vitalu visitolewe subject to mabadiliko ya sheria mpya??
 
hivi, unaweza revoke mikataba iliyo valid kisheria??

How? Gharama za ku-revoke zitakuwaje??

what is the impression? Does it mean we don't have lawyers who can draft a win win agreement? Or are they forced by whoever to draft shoddy contracts? Shule ya nini sasa kama mambo ni hovyohovyo tu ktk nchi hii?
 
zito, hivi tunahitaji kuipangia matumizi maalumu pesa inayotokana na gas?? Umuhimu wake nini??

Vyanzo vingine vya mapato mengine yanapangiwa matumizi??

Je, impact ya pesa za EPA zilizorudi zikiwa zimepangiwa matumizi, tumezifaidi??

Na matumizi hayo yatakuwa ndio kipaumbele au itakuwa madawati tena??

Sikubaliani na hili.
 
Last edited by a moderator:
pamoja na wanasheria wa Tanzania kuwa wazuri sana, bado wanapwaya sana ukilinganisha na wanasheria wa nje kwenye upande wa kuingia mikataba ya madini.

wenzetu wako mbele sana ya mchezo, kutokana na uzoefu wa muda mrefu.

Sasa hapa unakuta mtu anauza eneo lake kwa kutumia draft ya mkataba anaouzia nyumba.

Afu ujue nchi zingine wana bodi za wataalam wa kuingia mikataba ya madini, hapa kwetu hatujui hata kama tunahitaji, kwanza hatujatambua hata kama ni taaluma inayojitegemea.

We do have lawyer, and competent lawyers for that matter. But, our problems is that even those competent lawyers have either been compromised or have decided to also work for self interests. Only few of them thinks of wider public interests when dealing with such issues
 
Back
Top Bottom