Flaviana Matata Foundation, Marie Stopes Tanzania Watoa Elimu Usherekea Siku Ya Hedhi Duniani 28, Mei 2022

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
c4846182-f01a-4dfe-ac96-15cba6da60e2.jpg

Siku ya hedhi duniani huadhimishwa kila mwaka, siku ya tarehe 28 Mei ikiwa na lengo ya kuwakutanisha wadau mbalimbali kwa dhumuni la kuongeza uelewa kuhusu masula ya hedhi kwa msichana na kuhamaisha msichana kupata maji safi na taulo.

Hii hasa inawalenga wale walio katika mazingira ya hali ya chini ili wanapoingia katika siku zao za hedhi waweze kujisitiri na kuendelea na taratibu zingine kama kuhudhuria masomo na shughuli nyingine

Kauli Mbiu ya Siku ya Hedhi Mwaka 2022
Kauli mbiu ya mwaka huu ni Hedhi iwe kama ni moja ya Maisha ya kawaida kwa msichana na mwanamke (Making menstruation a normal fact of life by 2030) Hii ina maana tuwe na dunia ambayo hakuna mtu ataachwa nyuma au atashindwa kufikia malengo yake au kufanya shughuli zake za kila siku kwa sababu tu anaingia kwenye siku za hedhi.

Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Mkoa wa Mwanza
Katika kuadhimisha siku ya hedhi duniani, Shirika la Marie Stopes Tanzania kushirikiana na Flaviana Matata Foundation wametoa elimu ya masuala ya hedhi salama kwa wasichana na wavulana 987 katika Shule ya Sekondari ya Bukandwe ya Wilayani Magu Mkoa wa Mwanza.

Hata hivyo baada ya mafunzo mashirika hayo yaliwashika mkono wanafunzi hao kwa kutoa Zawadi mbalimbali ikiwemo taulo za kike kwa wasichana.

Marie Stopes imetoa wito kwa mashirika binafsi, Serikali na walimu kusisitiza utolewaji wa elimu ya masuala ya hedhi kwa Vijana wa kiume na wa kike, ikiwa na Elimu hio itamsaidia msichana kutambua mabadiliko ya mwili na kukabiliana nayo pamoja na kufahamu namna ya kujisitiri kipindi anachoingia kwenye hedhi, na kwa mvulana kuelewa mabadiliko hayo kama mshiriki mwenza ili kuondoa unyanyapaa pale msichana anapokuwa kwenye hedhi .

Kwa mashirika ya afya, mashirika ya maendeleo na taasisi mbalimbali kuzisaidia jamii kwa namna mbalimbali kuhakikisha wasichana hasa walio mashuleni wanakuwa na mazingira rafiki ili wanapoingia kwenye siku zao za hedhi wasikose mahitaji yao muhimu yatakayowasababisha kushindwa kushiriki kwenye masomo na masuala mengine ya jamii kutokana na hedhi .

Kuliangalia swala la utaratibu wa bei za taulo za kike, upatikanaji wa maji safi na salama katika shule , kusaidia maeneo yenye uhitaji ili wasichana waweze kupata taulo za kujisitiri kwa muda wa mwaka mzima ili wasiweze kukosa mahudhurio shuleni.

Hedhi ni nini ?
Ni kipindi maalumu katika mzunguko wa mwanamke mwenye umri wa kuzaa. Wakati huo, ambao kwa kawaida unarudi kila baada ya mwezi mmoja hivi, yeye hutokwa na damu kwenye uke.

Sababu ya damu kutoka ni kwamba, kijiyai kilichokomaa na kutoka nje ya kifuko cha vijiyai kisipopata mbegu ya mwanamume baada ya siku moja kinaharibika harakaharaka; hapo ngozi nyembamba ya tumbo la uzazi, iliyotanuka kwa damu ili kupokea na kulisha mimba, inajiengua na kutoa damu.

Kumbe mbegu ikikifikia kijiyai, mimba inapatikana na kujishikiza kwenye kuta za tumbo la uzazi ili iendelee kukua; hapo damu haitoki na mama anaweza kujihisi mja mzito. Mizunguko mingi ya hedhi huwa na siku kadhaa za mwanzo ambapo mimba haiwezi kupatikana (muda wa kutoshika mimba kabla ya kudondosha kijiyai), halafu siku ambazo mimba inaweza kutungika, na kisha siku kadhaa tu kabla ya hedhi ambazo mimba haiwezi kutungika (muda wa kutoshika mimba baada ya kijiyai kudondoshwa).

Kumbe mbegu ikikifikia kijiyai, mimba inapatikana na kujishikiza kwenye kuta za tumbo la uzazi ili iendelee kukua; hapo damu haitoki na mama anaweza kujihisi mja mzito. Mizunguko mingi ya hedhi huwa na siku kadhaa za mwanzo ambapo mimba haiwezi kupatikana (muda wa kutoshika mimba kabla ya kudondosha kijiyai), halafu siku ambazo mimba inaweza kutungika, na kisha siku kadhaa tu kabla ya hedhi ambazo mimba haiwezi kutungika (muda wa kutoshika mimba baada ya kijiyai kudondoshwa).
3c8a6a08-8ace-457d-9519-a9b12eddb492.jpg


Hedhi salama nini ?
Hedhi salama ni ile ambayo inahusisha mtoto wa kike kupata mahitaji yake yote muhimu akiwa kwenye siku zake za hedhi. Mahitaji hayo huhusisha taulo za kike ama pedi kama ijulikanavyo na wengi, maji safi na salama na sehemu ya kubadilishia. Wataalamu wa afya wanasema kuwa mtoto wa kike akipata hedhi salama basi ataweza kuondokana na matatizo mengi ya kiafya kama vile miwasho, fangasi, maumivu pamoja na hedhi bila kutokwa damu nyingi na hivyo huwa hedhi yenye amani na furaha.

Suala la hedhi halipaswi kuwa kero kwa mtoto wa kike. Hata hivyo, imekuwa tofauti kwa watoto wengi wa kike ambao wamekuwa wakipata wasiwasi na kukosa raha pindi wanapokaribia mzunguko wao. Hii inatokana na changamoto ambazo watoto hawa wa kike wanazopitia katika kupata hedhi salama.

Jambo la kusikitisha ni kwamba mara nyingi tumekuwa tukigusia tu masuala ya kiafya pindi tunapozungumzia hedhi salama na kusahau kuwa kukosekana kwa jambo hili kunaweza kuleta athari katika nyanja mbalimbali za maisha ya mwanamke huyu. Baadhi ya mazingira yanayoweza kumkwamisha mtoto wa kike ni pamoja na:

Mila potofu mfano: mwanamke au msichana aliye kwenye hedhi hapaswi kugusa maji, kupika, kushiriki sherehe za kidini au hata za kijami. Fikra hizo potofu husababisha ubaguzi na kuendeleza Imani potofu juu ya wanawake wanapokuwa katika siku zao za hedhi kuwa ni wachafu.

Kutojihusisha katika shughuli mbalimbali za jamii kutokana na kukosekana kwa nyenzo ambazo zitamsaidia mtoto wa kike katika kipindi aonapo hedhi basi mara nyingi watoto hawa hujitenga katika shughuli mbalimbali kama vile shule, michezo, mikutano mbalimbali kwani huona aibu na hofu ya kuonekana kwa watu akiwa na hali ile. Kutojihusisha na shughuli hizi huweza kuleta madhara makubwa sana kwa mtoto huyu wa kike na yanaweza kuwa ya papo kwa papo au ya muda mrefu.

Kukosa fursa kama mwanamke atakuwa wa kukaa tu nyumbani kipindi akiwa kwenye siku zake sababu tu amekosa vitu vya kumsaidia kupata hedhi salama basi ni wazi kuwa atakuwa anakosa fursa nyingi sana zinazoweza kujitokeza katika jamii yake kipindi yeye akiwa katika siku zake za hedhi
25ca0706-1a23-4168-842e-0d103ff2de45.jpg


Ushauri
Kwa wasichana wanaokutana na changamoto za hedhi ikiwemo maumivu yasiyo ya kawaida basi watembelee vituo vya afya vilivyo karibu nao kwa msaada zaidi. Lakini pia wanaweza kutupigia Marie stopes kwa namba bila malipo 0800 753 333 kwa ajili ya ushauri wa masuala ya hedhi na wanaweza pia kutembelea vituo vyetu vilivyopo Dar es Salaam, Zanzibar, Mwanza, Musoma, Kahama, Arusha , Iringa, Makambako na Kimara.
 
Siku ya hedhi duniani huadhimishwa kila mwaka, siku ya tarehe 28 Mei ikiwa na lengo ya kuwakutanisha wadau mbalimbali kwa dhumuni la kuongeza uelewa kuhusu masula ya hedhi kwa msichana na kuhamaisha msichana kupata maji safi na taulo.
Usishangae kuona men wana nyadhifa kibao humo kwenye mkutano
 
Back
Top Bottom