Fisadi mwingine huyu





- Kwanza mbunge anasema kwamba complaints hazina facts! Halafu anakuja chini hapa anasema sio sawa kumshambulia Rais Kikwete peke yake, badala yake iwe ni viongozi wote:-



- Halafu anabadilika tena na kusema Rais alichaguliwa na viongozi wengine pia, ona hapa chini:-



- Sasa unakaa na kujiuliza hivi hili taifa tulimkosea nini Mungu? Sisi wananchi wa Tanzania tumlimchagua Rais kuongoza taifa, yaani sisi wananchi na tukampa nafasi kikatiba kuchagua washauri wake na wasaidizi wa kutimiza lengo letu kwenye taifa, sasa leo tunaposema ameshindwa kazi tuliyompa, Mzindakaya anasema nini tena? eti tuwashambulie viongozi wote, wakati kamati ya bunge imeshasema wazi kwa kuwataja kwa majina wahusika wa Richimonduli na hata ikatoa ushauri wa nini kifanywe kisheria kuwaadhibu majambazi wakubwa kina Lowassa, Rostam, Msabaha, Karamagi, Mwakapugi, mpaka Hosea, sasa tulitegemea our Chief Law-Enforcement Officer, Rais wa jamhuri Kikwete awashughulikie haraka inavyotakiwa, sasa kama ameshindwa ashambuliwe nani madiwani?

- I mean wabunge wamefanya kazi yao, kuanzia kamati ya Mwakyembe, mpaka bunge zima limeipitisha ile ripoti, sasa Mzindakaya anataka tuwalaumu madiwani kwamba kwa nini ripoti haijfanyiwa kazi badala ya kiongozi tuliyemchagua kusimamia sheria za jamhuri yaani Rais wa jamhuri! Sasa kama huyu ni mbunge tena wa toka enzi za Mwalimu, sasa tutegemee nini kutoka kwa Rais? Maana hawa kina Mzindakaya ndio washauri wenyewe wa Rais, na believe me anawawakilisha wengi sana na hizi nonsense!

- Kwanza anasema hakuna facts, halafu anasema asishambuliwe Rais peke yake maana makosa sio yake peke yake na wengine pia, mweeee! Mungu mweeee! hivi tulikukosea nini hili taifa? Wa-Tanzania inabidi tuendelee kushambulia hapo hapo maana inaonekana this time message imefika, tulisema huko nyuma kuwa iko siku the buck itafikishwa inapotakiwa, yaani mezani kwa Rais na sasa imefika!

- I mean Rais wa jamhuri anaulizwa na kina Butiku na Quaresi, kwamba yeye kama Chief Law Enforcer wa Jamhuri hii, kwa nini majambazi wa Richimonduli wapo nje, yeye anajibu kwamba eti ni wivu na chuki, Sophia aliposema ni wivu na chuki kule kwenye kamati ya Mwinyi, tulidhani amepagawa kumbe sasa inaonekana kuwa huenda ndiyo lugha ya huko Ikulu, kwamba kila anayekosoa ana wivu na chuki ya kukosa Urais na u-First Lady, pleeease tulijua tu kuna siku yatawafika shingoni kuhadaa wanachi, kununua media, kuwatumia kina Tido Mhando na polls fake, kuwatumia waalimu wa mlimani, mihela ya Iran, kuwachafua kina Salim, yote haya ya yalikuwa ya nini kama kweli mlikuwa na uwezo wa kuongoza?

- Sasa saa imefika ya kuhesabiwa mnalia wivu na chuki, mkatishia weee kwamba Mtandao msipopewa uongozi basi taifa halitakalika wala halitaongozeka garademiti, sasa uongozi umewashinda mnalilia wivu na chuki, maana Quaresi naye aligombea urais sasa ana chuki za kuukosa na mkewe kukosa u-First Lady pure nonsense!, unajua inafurahisha sana mnavyoumbuka ingawa on the other hand pia inasikitisha sana kwa sababu mnaumbuka kwa ghrama ya migongo ya umasikini wa wanachi walalahoi!

Mungu Aibariki Tanzania!


Respect.


FMEs!





FEMS,
Usisahau kuwa mganga huyu ni kambi tofauti kabisa na ile ya mtandao!, wapi na wapi makatapila na mtandao?? na hata JK mwenyewe anaelewa hilo... na iweje kumpaka mwenzio mafuta kwa mgongo wa chupa? eti asilaumiwe peke yake kwa hiyo tayari unam-discredit yeye na system nzima lol what a strategy!!,

Amani.
 
Back
Top Bottom