Anasema wanafanya mambo kwa - funika kombe mwanaharamu apite. Anasema Waziri Mkuu aliapa kuilinda katiba lakini sasa wanachokifanya ni kulindana tu.
Anasema bungeni kuna mawaziri 30 lakini wanaowajibika ni kama 10 na anaweza kuwataja.
Anasema tusifanye kazi za Nape Nnauye bungeni. Anasema tusiwabeze wapinzani kwa kila kitu.
Huyu jamaa anaonekana moyo wake hauko tena CCM.
Source: Bungeni leo asubuhi
kama unatafuta wenye akili CCM huyu ndio pekee ana akili timamu wengine ni mbofu mbofu tu
ndani ya ccm hakuna uhuru wa kutoa maoni hata hayo aliyosema tayari yameshamuweka matatani,. wewe hukumbuki alivosaini kumuondoa waziri mkuu aliitwa na kuhojiwa??akiwa nje ya ccm atatoa mchango mpana zaidi kwa maendeleo ya taifa letu!aa hapana kaka punguza mkari basi ss kama wapenda maendeleo ungepaswa umpongeze kisha umwombe aongeze kazi, nguvu na ari mpya ktk kuikosea serikali pale inapokosea si lazima aje ila afanye wajibu wake kama mbunge hicho ndo tunataka si lazima uwe mbunge wa cdm hata hao waccm kama alivyoonyesha njia MHESHIMIWA DEO
Rangi, Umeeleweka.Awataka wabunge CCM waache kufanya kazi za NAPE na wawajibike badala ya kufanya SIASA BUNGENI. WASIPOPATA meli katika jimbo lake wataandamana muda wowote na mahala popote, amekataa kuunga mkono hoja ya waziri mkuu hadi mambo ayatakayo yatimizwe.
Njano5.
Hawa ndiyo wazalendo wanaotakiwa ................... tatizo kubwa la nchi yetu wasafi na wazuri CCM wameamua kukaa kimya kitu ambacho hakitusaidii wote!!
Nampomgeza na kumkubali sana Filikunjombe. Huyu ni mbunge aliye makini na mwenye mawazo huru yenye taswira ya maslahi ya taifa: si mnafiki. Wenzake wa chama chake wanamuona kwa jicho baya: Nadhani hakufaa kuwa CCM maana mawazo yake hayafanani na ya wao.Yaani kweli Bungeni ukuwasema wapinzani kwa lugha mbaya unasifiwa, kama jana Mkamia alivyoendelea baada ya kumtukana Sugu, leo Filikunjombe kalazimishwa kutoa neno miwani ya Mbao, ila ndo hivyo Waziri Mkuu hapo anapata machungu na kukumbuka yale majina ya wabunge waliosaini kutokuwa na imani naye, Filikunjombe alikuwa muwazi na si mnafiki kama wengine:rockon: