Filamu ya Kijiji cha Tambua Haki.

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
1,002
274
Wakuu habari za mida hii natumai mko poa.Mimi huwa si mpenzi wa kuangalia filamu hasa za kibongo. Ila filamu hii aliyoicheza marehemu Stephen Kanumba enzi za uhai wake nimeipenda sana tena sana na nilitamani lait kama ningelikuwa na uwezo wa kununua nakala nyingi za filamu hiyo na kuzigawa kwa kila mtu aishie kijijini ningelifanya hivyo ili kuwaamusha kutoka katika uzingizi wa uonevu wanaofanyiwa.Na mwisho ni jinsi gani wanavyofanya na kuondokana na udhalimu huo.Nawasihi kama wewe sio mpenzi wa kuangalia filamu hebu itafute filamu hiyo uitazame kisha mtumie nduguyo anayeishi kijijini mwenye kauwezo kakumiliki tv na yeye aitazame pamoja na wanakijiji wenzake ili walitambue hili.Nawasilisha pia nawatakia utazamaji mwema.
 
Back
Top Bottom