Fikra za Mwalimu: Hizi hapa.. mzikubali au mzipinge!

Hii mada ya Nyerere imekuwa na mvuto wa wachangiaji wengi sana!Mimi naomba kuuliza swali moja kwa wachangaiji wa mada hii HIVI KWAN NINI NYERERE ALITAKA KUPINDULIWA MWAKA 1982?
 
Hii mada ya Nyerere imekuwa na mvuto wa wachangiaji wengi sana!Mimi naomba kuuliza swali moja kwa wachangaiji wa mada hii HIVI KWAN NINI NYERERE ALITAKA KUPINDULIWA MWAKA 1982?

Kawatafute kina Hatibu McGhee, Metusela Kamando, Kadego na Otto waliotaka mpindua uwaulize!
 
Sisi Waafrika ni watu wa pumba (maneno) sana na ndio maana sishangai kuwa bara zima limelosti! Tunaongea mno lakini kutenda hatujui.
 
jibu gani sasa hili!!? maswali mangapi ambayo wewe ushawahi kujibu hapa wakati kuna wenyewe ambao wangewezwa tafutwa na kuulizwa? kama huna jibu unachuna tu na sio kuleta........ngoja niishie hapo!!.

Heheheheheee...this is a good one. And boy you're up early today...
 
Naomba kuuliza kitu kimoja hapa...
Tunazungumzia fikira za Mwalimu na uwezekano wake kufanya kazi ktk mazingira yetu?.. ama tunazungumzia vitendo vilivyofuatia baada ya fikra hizo kutofanya kazi!..
Maana kwanza lazima nikubali kwamba sisi wengine hapa maneno mingiii kama mwalimu mwenyewe, unajua tena yeye alikuwa reflection ya kina sisi hapa..nanyi ndio za kina Mkapa na JK!

Nachojaribu kuelewa huu ubishi unatokana na kitu gani haswa maanake FIKIRA na BUSARA sio vitu vinavyosomwa mashuleni ila ni kipaji, na kichwa cha mada hii kinajieleza vya kutosha....

Je, mnachojaribu kusema hapa ni kwamba hizo itikadi za mwalimu na Ujamaa hazikuweza kufanya kazi na hazitaweza fanya kazi?...Je, kinachoongelewa hapa ni katiba ya TANU na CCM? maanake naona focus nzima ya mjadala huu inahusu siasa zake za Ujamaa. Je, maandishi mengine aliwahi kuyaandika nje ya kiti chake cha wenyekiti na Urais!.. mathlan vitabu vyake havina mpango vile vile!
Is it to say watu kama MLK waliosema sanaaa na wakafa bila kuwepo mabadiliko ya hali za wananchi weusi, walikuwa wakilolonga ovyo hakuna busara kabisa ktk maneno yao?..
Nashindwa kufuatilia mada hii kuelewa haswa kitu gani kinachodaiwa toka upande wa pili kwani FIKIRA na UTEKELEZAJI wake ni vitu viwili tofauti kabisa pamoja na kwamba hoja kubwa ya fikra hizo ni ufunuo wa kufika pale palipo kusudiwa..

Hata msomi aliyeandika kitabu cha kujifunza hesabati hawezi kuhukumiwa elimu yake ya utunzi kwa sababu ya matokeo ya wanafunzi wengi kushindwa mitihani ya hesabu...
I mean jamani nifungueni macho nashindwa kabisa kelewa wapi tunakwenda... Je, mnachotaka ni kuziona hizo FIKIRA ktk maandishi kisha zichambuliwe maana sioni uchumbuzi wa fikira hizo isipokuwa kile kilichotokea.

Ni aibu kubwa kwa vijana wa Kitanzania hakika kufikia kusema hali ya Tanzania ilikuwa sawa na Zimbabwe wakati mwalimu anang'atuka hali mwalimu aliondoka fedha yetu ikiwa na thamani kubwa hivyo mali zetu kuonekana aghali ktk masoko...Uchumi wetu uliporomoka kinyume cha kile kinachotokea Zimbabwe..
 
.....
Ni aibu kubwa kwa vijana wa Kitanzania hakika kufikia kusema hali ya Tanzania ilikuwa sawa na Zimbabwe wakati mwalimu anang'atuka hali mwalimu aliondoka fedha yetu ikiwa na thamani kubwa hivyo mali zetu kuonekana aghali ktk masoko...Uchumi wetu uliporomoka kinyume cha kile kinachotokea Zimbabwe..

Wakati nikiendelea kutafakali bandiko lako napenda kushukuru kwa aya hii yako ya mwisho. Ni muhimu watu kukumbuka hilo!
 
Bob you are right on ya kulinganisha bongo na zimbabwe, no hiyo ni a big joke, jana nimesikia kuwa bank ya Zimbabwe iameanza kuchapisha noti za shillingi millioni 15, maana hiyo ni good kwa mikate mitatu ya boflo!

Bongo mwaka 1986, Mwalimu akiwa sio rais tena kwa kutmia kibali cha Bank Kuu, nilinunua tiketi ya ndege kutoka Dar-Brussells-Montreal, kwa shillingi laki moja na ishirini za bongo, halafu nilinunua dola bank of commerce, hapa foreign branch kwa shillingi kumi na sita kwa dola moja, yaaani $ 1.00 kwa TSH. 16.00, risiti ninazo mapaka leo sijazitupa,

Sasa pamoja na yote tuliyoyapitia ya waya na nini, lakini zimbabwe bado hatujawafikia na sidhani kama tutakuja kuwafikia. Maneno yako mengine ni mazito sana ninahitaji kuya-diggest kwanza!
 
jibu gani sasa hili!!? maswali mangapi ambayo wewe ushawahi kujibu hapa wakati kuna wenyewe ambao wangewezwa tafutwa na kuulizwa? kama huna jibu unachuna tu na sio kuleta........ngoja niishie hapo!!.

This was a figure of speech, my outlook on the issue was already spelled.
 
...........fikra na matendo bega kwa bega, bila matendo fikra zinakuwa maneno mingi na hivyo ni bure tu!!!.

This nafikiri ni very strong point, kwa sababu mimi binafsi huwa ninamuaminia sana nabii Issa, au Yesu Kristo, kuwa kama ni change au mageuzi, basi huyu jama alikuwa ndio mambo yote, na anasema kwamba alikuwa siku zote inspired na maneno au fikra, kama sio sera za baba yake, yaaani mkulu God,

Na ukisoma vizuri maneno ya Mungu, yaliyokuwa ndio hasa kiini cha motivation ya Yesu kufanya mageuzi an change za ajabu, basi Mungu anasema kuwa fikra au imani bila vitendo kufuatia, ni kazi bure, nionyeshe mtu mwenye maneno bila matendo aliyefanikiwa, ukweli ni hakuna, maneno au fikra ambazo haziwezi kufanyiwa kazi ninajiuliza kwamba ni za nini na kama ni worthy hata kuwa nazo, licha ya kuzichambua?
 
Field Marshall ES,
Mkuu wangu hata Yesu alipoondoka alikuwa na wafuasi sio zaidi ya 100 tena kati yao walikuwepo wabaya. Hali na matendo ya Wayahudi ndio yalikuwa mabaya zaidi hata ikabidi wafuasi wake wakimbie nchi wengine kwenda hadi Roma, Ugiriki na kadhalika..
Hadi leo hii tukitazama vitendo vyetu wote dunia nzima basi naweza sema Yesu hakuwa na fikra kwani hakuna mafanikio kabisa zaidi ya watu kuwa na imani JINA. Leo hii vitendo vyetu ni viovu zaidi ya wakati wowote ule ktk mafundisho yake..
Na hata upande wa waislaam vile vile leo hii sisi wafuasi ni washenzi kuliko wakati wowote ule na tunahalalisha mengi kutokana na mazingira yetu (hizo change zenu)..sometimes huwa nashindwa kuwalaumu wale wanaoweka madai kupindisha Kuran kutokana na matendo ya Waislaam wa leo, lakini hata hivyo ni muhimu wabadilishe mbinu za kuvutia wale wasioamini badala ya kujenga uadui..
Hawa wote (Yesu na Muhammad) hawakufanikiwa then na hawajafanikiwa leo ukitaka kutazama matokeo ya vitendo vyetu sisi tuliokusudiwa.

Hivyo basi kuhalalalisha kwetu maovu kama ya kina Mwinyi, Mkapa, JK kwa sababu ya mazingira tuliyokuwa nayo na mkono wa binadamu ktk kitangaza fikra chafu zinazopingana na Biblia yetu.... inaashiria ndivyo tulivyo na kuwa hawa viongozi ni reflection yetu sisi. Hawana makosa wala hakuna haja ya kuwakaumu hata kidogo.
Mkuu ebu pitia hii story nzima google neno hili kisha isome taarifa nzima nakumbuka nilisha iweka mahala siku za nyuma - The power and the vainglory!
Utamkumbuka baba wa Taifa mkuu...
 
Hadi leo hii tukitazama vitendo vyetu wote dunia nzima basi naweza sema Yesu hakuwa na fikra kwani hakuna mafanikio kabisa zaidi ya watu kuwa na imani JINA. Leo hii vitendo vyetu ni viovu zaidi ya wakati wowote ule ktk mafundisho yake..

Mkuu wangu Bob,

Mimi sina tatizo kabisa na Mwalimu, ninachojali ni ukweli wa anything, kuanzia fikra mpaka sera za itikadi, vitendo vyetu viovu dhidi ya mafundisho ya nabii Issa au Yesu, ambaye alikuwa akifuata maneno ya baba yake, yaaani Mungu, haibadili ukweli kwamba bado kuna bin-adam wanaofuatilia hayo hayo mafundisho ya Yesu na kufanikiwa hadi leo hii tunapoandika hapa,

lakini leo hakuna mahali bongo au Afrika, unapoweza ku-practice fikra au sera za itikadi za Mwalimu, ukafanikiwa sasa to me hizo fikra zina matatizo, Yesu alizi-practice mwenyewe fikra za baba yake na bina-adam wakamuaona akifanikiwa kwa muelekeo wa zile fikra, sasa fikra za Mwalimu, hata kina Kingunge wamezikimbia maana ni un-realistic, mimi kwangu ndio hoja ya muhimu, sasa kwa sababu hiyo basi tuyachambue kwa kina mapungufu ya either fikra hizo za Mwalimu, au Mwalimu mwenyewe, cha muhimu ni kupata an idea of why tumefika hapa tulipo as a nation!

The ishu sio kumlaumu Mwalimu tu, hapana we have our responsibility too kwenye this mess, lakini tunahitaji kujua how tumefika hapa, ni lazima kuchimba hekima na busara za Mwalimu, kisiasa.
 
Mjadara huu wa Fikra za Mwalimu Nyerere ni lazima uzingatie matukio yote makubwa katika Historia ya Tanzania.

Mapinduzi ya Zanzibar 1964 yaliyoongozwa na John Okello.

Mwafaka wa siri kati ya Nyerere na Marekani ili kuzuia Zanzibar isivamiwe na Warusi kueneza Ukommunist.

Jaribio la mapinduzi la mwaka 1964 likiongozwa na wanajeshi waliosoma Israel.
Nyerere kuvaa Baibui na kujificha St Joseph, wakati Kambona anapita akiendesha Gari mitaani hadi ikulu kuwatuliza Askari walio asi.
Bibi Titi Mohamed na maanguko ya kisiasa.

Kuzaliwa kwa ugomvi wa kisiasa wa Nyerere na kambona.
Ikumbukwe kwamba Nyerere ndiye Bestman wa Kambona wakati akioa huko London.

Kumtimua John Okello kama mbwa koko Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Mauaji ya Zanzibar chini ya Rais Karume na kuwanyamazisha kabisa washiriki halisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, na kuingia rasmi kwa Dhambi ya dhurma huko Zanzibar

Kifo cha JFK Best friend wa Nyerere.

Urafiki na Mao wa China

Azimio la Arusha.

Karume kushindiliwa Risasi na Mlinzi wake.

Pata shika Mpya Zanzibar baada ya kifo cha karume.

Upinzani wa wazi wa KNCU na KCU dhidi ya Siasa ya Ujamaa ya Nyerere.
 
Ingekuwa hili swali la Fikra za Mwalimu ni swali katika mtihani, wengi wangefeli kutokana na majibu yaliyotolewa humu ndani.

Swali lililenga Fikra na si Sera (Vision not Policy)! Majibu ya knee jerk reaction yamekuwa kuhusiana na policy na si Vision.

Hata bandiko la awali la kumnukuu Mwalimu lilikuwa ni kuhusiana na theme ya maneno yale na uwiano wake katika mazingira tuliyomo.

Kama kawaida, ndivyo tulivyo que sera sera, tumekimbilia kuwa subjective kutokana na hisia zetu hasi kuhusiana na Mwalimu Nyerere na kushindwa kuwa objective na kujibu swali kuhusu Fikra zilizobandikwa.

Naungana na Bob Mkandara kuwa hii ni aibu sana kwa sisi ambao tunajiita "Wasomi" na "Elite" kama tunashindwa kujibu masali na hoja kama zilivyoulizwa na kukimbilia kutoa majibu ya hisia zetu na chuki juu ya Nyerere.

Hivyo basi, wengi wetu tumeshindwa jibu ama kuzikubali Fikra zilizoletwa au kuzipinga kwa kuonyesha ni vipi zinaweza tumika au haziwezekani kabisa. Kama tulifikiri tumepata Msonge, tujiangalie tena tumezungusha Sifuri hivyo pepa ni F (FAIL)!
 
..Sifa ya kiongozi haipaswi itokane na maneno, au fikra zake. inapaswa itokane na rekodi na matokeo ya utendaji wake.

..Nyerere alikuwa na tabia ya kumsukumizia lawama Mzee Rashidi Kawawa.

..Watanzania tuliaminishwa kwamba aliyekuwa akiharibu ni Kawawa na siyo Nyerere.

..Hata kama Kawawa alikuwa yuko mstari wa mbele, je kuna wakati wowote alikiuka maagizo ya utekelezaji toka kwa Baba wa Taifa?

..Kuna waliojaribu kututofautisha na Zimbabwe. wanafikiri Nyerere hakulikoroga kuliko Mugabe.

..Baba wa Taifa angeendelea madarakani miaka 5 zaidi mnafikiri tungefika wapi?

..hivi mumejaribu kulinganisha sekta ya elimu ya Zimbabwe sasa hivi, na sekta ya elimu wakati Mwalimu anaondoka madarakani?

..nakumbuka wakati Mwalimu anaondoka madarakani nilikuwa nakalia TOFALI darasani. vitabu vya kiada tulikuwa tunasoma watoto watano kitabu kimoja. tena ilikuwa haiwezekani kuchukua kitabu kwenda nacho nyumbani.

..hivi tulitaka nchi iharibike namna gani mpaka tuelewe kwamba Mwalimu alishindwa uongozi?

..mnaosisitiza umuhimu wa fikra za Baba wa Taifa, naomba mueleze kama mko tayari turudie hali ya maisha ya miaka ile wakati anaondoka madarakani.

..Kwa mataifa ya dunia ya tatu, Kiongozi bora ni yule atakayewezesha wananchi wake kuwa na MLO wa uhakika, KAZI za uhakika, ELIMU bora na ya uhakika, HUDUMA ZA AFYA za uhakika. Kinyume cha hapo amefeli.

NB:

..wasomi wazima tunapumbazwa na maneno matamu, halafu tunashangaa ndugu zetu kule vijijini wanavyoikumbatia CCM.
 
..

..Watanzania tuliaminishwa kwamba aliyekuwa akiharibu ni Kawawa na siyo Nyerere.

..

Kama ambavyo sasa watu wameaminishwa kwamba aliyekuwa anamharibia Kikwete ni Lowasa. Maskini Lowasa wa watu kashambuliwa tena hata kuongea sasa haruhusiwa na "pundits" wa Tanzania. Tuna shida kubwa sana katika fikra as a country-ukubwa wa shida hii unaongeza pale ambapo wenye shida ni wale ambao wanadhaniwa ndio wasomi wa nchi hiyo. Kazi tunayo!
 
..

NB:

..wasomi wazima tunapumbazwa na maneno matamu, halafu tunashangaa ndugu zetu kule vijijini wanavyoikumbatia CCM.


In fact ndugu zetu vijijini ni wajanja kuliko sisi wa mijini tunaofikiri tumesoma. Tazama Dar nzima haina diwani wala mbunge wa upinzani, lakini Mpanda, Kigoma, Tarime, etc wanao. Sasa utasema sisi wa Dar ni wajanja kuliko huko Mpanda? Only in Tanzania ambapo upinzani unakubalika vijijini kuliko mijini. The problem: there is something terribly wrong and dangerous with our education system to the extent that those who go to school are more morally corrupted and intellectually sterilized than those who don't! Otherwise, how can we explain the level of zombiness that is constantly displayed by the so called "wasomi"?
 
Mimi sikubaliani na usemi kwamba wasomi tumeshindwa kujadiri hoja kuhusu Fikra za Nyerere.

Tuchukue kipengera kimoja baada ya kingine na kukichambua kwa undani.
Kwa mfano.

Fikra zilizo ibua hoja ya Kutaifisha Mashule.
Fikra zilizo ibua hoja Kutaifisha Hospitali.
Fikra zilizo ibua hoja Kuua Vyama vya ushirika.
Fikra zilizo ibua hoja ya kufuta unyapala.
Fikra zilizo ibua hoja ya kufuta Kiingereza kama somo la kufundishia Primary.
Fikra zilizo ibua hoja ya kuua mfumo wa elimu ya kikoloni na kuandaa mfumo mpya wa elimu usiozingatia soma la Utaifa.

Kujadiri Fikra za MWalimu Nyerere kijumla jumla kunaleta hali ya kuona watu tunamsimangaMWalimu Nyerere bila sababu za msingi.
 
..mara nyingine dawa hutoa matokeo mazuri inapojaribiwa kwenye test-tubes au kwa panya wa majaribio.

..lakini dawa hiyo ikijaribiwa kwa wanadamu inaweza kuwa na madhara makubwa.

..Wataalamu wakigundua hilo huamua kusitisha mara moja matumizi ya dawa hiyo.

..mara nyingine wataalamu hufikia hata kuifunga au kuifanyia uchunguzi maabara iliyotoa dawa yenye madhara.

..mimi nafikiri mfumo huohuo utumike ktk kujadili hizo "fikra" na "njozi" za Mwalimu.

..kama zilikuwa na madhara wakati wa utekelezaji wake, kwanini tuziamini kama zilivyo?

..ningewaelewa kama baadhi yenu mngekuja hapa na at-leat marekebisho ya fikra hizo.

..katika mazingira yetu kwanini tusiifungie CCM at-least kwa muda? kwanini tusikiangalie chama hiki with suspicious eyes? kwanini tunachezea maisha yetu kwa kuwarudisha madarakani?
 
Kitila,

..ukiangalia, across the board, CCM inapata ushindi wa tsunami ktk maeneo yale yaliothirika zaidi na uongozi mbaya wa CCM.
 
..Sifa ya kiongozi haipaswi itokane na maneno, au fikra zake. inapaswa itokane na rekodi na matokeo ya utendaji wake.

Mkuu Joka, hiii ni safi sana, swali langu kwa Bob mkandara na Mkuu wangu Kishoka, eti mankuabliana na ile hadithi ya "...Zidumu fikra za mwenyekiti..."?
 
Back
Top Bottom