Fikra Pevu: Lowassa alipwa mamilioni na Wasomali

Hii habari ni ya siku nyingi sana. Nyie ndio mnaishushia hadhi JF. Hebu mod ondoeni huu uzi!!!
 
Enyi mliokua mnabishia UFISADI wa Ndugu Lowassa bila huruma kwa taifa lake, na wallahoi tulio wengi kila kona ya nchi hii na ugumu wa maisha, hebu sasa semeni tena!!!
 
Hakuna ubishi kwamba Mgombea mtarajiwa wa magamba ni fisadi. Huu ni uthibitisho mwingine wa ufisadi wake. Sijui fisadi Lowassa alilipa kodi kiasi gani kutokana na bulungutu lake hilo.
 
Kama ni pesa yao halali kutokana na jasho lao kama wafanyabiashara na wawekezaji acheni walipane kwani kuna mtu amelalamika kuhusu malipo hayo???
 
Hakuna ubishi kwamba Mgombea mtarajiwa wa magamba ni fisadi. Huu ni uthibitisho mwingine wa ufisadi wake. Sijui fisadi Lowassa alilipa kodi kiasi gani kutokana na bulungutu lake hilo.

Haujui alilipa kodi kiasi gani af unadai kafanya ufisadi, labda utuambie kamuibia nani kwenye hiyo biashara?
 
Hii habari ni ya siku nyingi sana. Nyie ndio mnaishushia hadhi JF. Hebu mod ondoeni huu uzi!!!

aiseeee baba yangu we ni gamba nini unataka mood autowe uzi aupeleke wapi mi ndio kwanza najua leo

ngoja nishushie na mbege
 
Hivi hapo kuna ufisadi gani jamani, au kuuza kitu chako kwa shea ni ufisadi. Sibishi kuwa mamvi ni fisadi ila hivi kwani nani sio fisadi? Bora fisadi mfanyakazi na mtafutaji au fisadi pumbafu anaetuibia na hatuoni anachofanya wala hatusaidii?
 
Hii kampuni ya kisomali ilipata mtaji wapi wa kuweza kuwekeza nchini? Isije kuwa ni wasomali ambao walikuwa wanateka meli za makampuni mbali mbali duniani na kisha kuomba mapesa chungu nzima ili kuziachia meli hizo. Na mapesa yao hayo yaliyopatikana kwa njia za haramu ndio sasa wanakuja kuzitakaza Tanzania.
 
But the guy is a businesman na wote tunajua hivyo so nashindwa kuthibitisha ufisadi hapa maana barua hiyo imesema tu anazotudai labda tungejua zilikuwa ni zanini otherwise inaweza ikawa ni clean money!
 
Hivi hapo kuna ufisadi gani
jamani, au kuuza kitu chako kwa shea ni ufisadi. Sibishi kuwa mamvi ni
fisadi ila hivi kwani nani sio fisadi? Bora fisadi mfanyakazi na
mtafutaji au fisadi pumbafu anaetuibia na hatuoni anachofanya wala
hatusaidii?
kwa hakika inashangaza kwa kumuona Lowassa kuwa ni fisadi kwa dili hili. Kinachoonekana hapa ni kuwa alifanya biashara halali na hao wasomali na ndio maana walikubali kumlipa. Labda kama alivyosema BAK, kama hakulipa kodi ya mapato kutokana na kipato hicho, hapo ndipo penye tatizo
 
Kwa kuzingatia dhana inaoitwa 'QUID PRO QUO' au NOTHING GOES FOR NOTHING kimsingi tunapata kung'amua kwamba chini ya jua hakuna chema (na katika thread hii ni Milioni 450) kinachoweza kuvuka juu ya meza ya biashara (counter) kutoka upande mmoja kwenda upande wa pili pasipo kutarajia chema sawa yake au kubwa zaidi kupata kupishana njiani kikirudisha hisani kiaina.

Mpaka hapo ni kwamba WaTanzania hadi sasa tunajiuliza Mzee Lowassa kapokea hizo Milioni 450 ikiwa ni kipato 'halali' kilichotokana na biashara gani hasa?

Sana sana tunachokiona hadi hivi sasa ni mauaji ya ndugu zetu Wamasai ili taifa la UARABUNI lipate kutengemaa huko Loliondo kwa namna yoyote ile, tata nayo kufyonza malighafi yetu bila mkataba wowote wenye maslahi kwa taifa ila tu kwa wajanja wachache tu - lakini mpaka leo hii hatujawahi kusikia kauli ya Lowassa akikemea mambo haya hadharani.

Huu ukimya wake wala si ajali kitu bali hasa ndio wizi uliolipiwa na Waarabu kupitia mkono wa 'Wasomali' wa Ki-Bongo ambao na wewe unawafahamu vema tu na mmojawapo hivi karibuni anatarajiwa kuukwa rasmi uongozi wa juu CCM ili mambo yote yawe shwari kwa mahesabu ya MAFISADI wote nchini.

Mkuu, swali la pili???

Kamuibia nani hapo?
 
Haujui alilipa kodi kiasi gani af unadai kafanya ufisadi, labda utuambie kamuibia nani kwenye hiyo biashara?

Kuna uwezekano mkubwa hizi ni pesa haramu. TAKUKURU wangekuwa wanatenda kazi kama ambavyo inastahili na kuifuatilia kampuni hii ya wasomali basi ingendulika tu kwamba pesa hizo si pesa halali ama zimepatikana kwa kuteka nyara meli za makampuni mbali mbali duniani, biashara ya madawa ya kulevya au kuuza nyara mbali mbali za Taifa ambazo walizipata kwa njia za haramu. Kama ni pesa halali na Lowassa anajua hilo basi kuna ubaya wowote wa Lowassa kutamka hilo hadharani? Si atakuwa anaisafisha kampuni hiyo na pia kusafisha jina lake?

Mafisadi wana njia mbali mbali za kutakasa pesa zao. Wanaweza kujifanya kuchukua mkopo ili kuonyesha kwamba chanzo cha biashara yao ni mkopo, kumbe tayari walikuwa na mapesa yao chungu nzima ambayo ni haramu.

Kwanini waende kukopa kwa Lowassa badala ya kwenda kwenye mabenki mbali mbali nchini? Ni lini Lowassa ameanza kujishughulisha na utoaji wa mikopo? ameshatoa mikopo kwa makampuni gani mengine nchini/duniani? Anatoza riba kiasi gani? Je faida anayoipata analipia kodi? Kishalipia kodi kiasi gani kutokana na faida hiyo aliyoipata kwa kutoa mikopo?

Haya ni mambo ambayo yanapaswa kuwekwa bayana ili kuondoa utata wowote uliokuwepo katika mkopo huo uliotolewa na Lowassa.
 
Kuna tatizo lipi Lowassa akifanya biashara na Wasomali, mlitaka afanye nao Mbowe pekee?

Umeshaenda Bilicanas? mpaka machangu wa kisomali wanafanyia biashara zao hapo, pitia ukaone.
 
Hii kampuni ya kisomali ilipata mtaji wapi wa kuweza kuwekeza nchini? Isije kuwa ni wasomali ambao walikuwa wanateka meli za makampuni mbali mbali duniani na kisha kuomba mapesa chungu nzima ili kuziachia meli hizo. Na mapesa yao hayo yaliyopatikana kwa njia za haramu ndio sasa wanakuja kuzitakaza Tanzania.

kwani wasomali wanashindwa kuwa na uwezo wa kuwa na kampuni kwa njia halali hapa nchini mkuu! mbona wapo wasomali kibao nnchi za watu huko ulaya na marekani na wanamakampuni pia! mbona hata watz wapo wengi wanaekeza huko nje na kwa hela za haramu na wengine za halali pia! yani nnchi kama somalia ikose watu wa uhalali wa kumiliki cumpini amabay ianaweza kulipa deni la mil 450 tu mkuu! skatai wapo wale wa haramu na wa halali, tuangalie pande zote mbili mkuu wangu
 
Mkuu Zomba hebu funguka kidogo, wenzako tunachokihoji tena kwa nguvu zote hapa ni kwamba wewe na wenzako wote humu MKATUTAJIE AMA AINA YA BIDHAA AU HUDUMA ambayo Mzee Lowasa alipata kuwauzia WaSomali kwa hiyo thamani kubwa ya Milioni 450 ili ubishi na mshaka uishe.

1. Mzee Lowassa, kwa kuwa ni mwenyekiti wa kamati ya Usalama nchini, je aliwauzia Wasomali HAKI YA KUPITA nchini hadi Dodoma bila kustukiwa na vyombo vyetu vya usalama?

2. Je, aliwauzia WaSomali au watu walioko nyuma ya WaSomali ardhi ya ndugu zetu WaMasai na kufanywa kuwa Taifa la Uarabuni ndani ya mipaka yetu ya Tanzania?

Toa jibu la moja kwa moja bila kuzunguka buyu hapa.

Kuna tatizo lipi Lowassa akifanya biashara na Wasomali, mlitaka afanye nao Mbowe pekee?

Umeshaenda Bilicanas? mpaka machangu wa kisomali wanafanyia biashara zao hapo, pitia ukaone.
 
Mkuu Zomba hebu funguka kidogo, wenzako tunachokihoji tena kwa nguvu zote hapa ni kwamba wewe na wenzako wote humu MKATUTAJIE AMA AINA YA BIDHAA AU HUDUMA ambayo Mzee Lowasa alipata kuwauzia WaSomali kwa hiyo thamani kubwa ya Milioni 450 ili ubishi na mshaka uishe.

1. Mzee Lowassa, kwa kuwa ni mwenyekiti wa kamati ya Usalama nchini, je aliwauzia Wasomali HAKI YA KUPITA nchini hadi Dodoma bila kustukiwa na vyombo vyetu vya usalama?

2. Je, aliwauzia WaSomali au watu walioko nyuma ya WaSomali ardhi ya ndugu zetu WaMasai na kufanywa kuwa Taifa la Uarabuni ndani ya mipaka yetu ya Tanzania?

Toa jibu la moja kwa moja bila kuzunguka buyu hapa.

Watanzania bado mko nyuma kibiashara. Hivi uwekewe wazi biashara za watu humu? unaakili sawa sawa wewe?

Hivi unajuwa kitu inaitwa "Industrial espionage and trade secrets"?

Ikiwa watu wanapoteza mabillioni kufanya ujasusi ili wajuwe mbinu za biashara za wenzao, wewe unataka uwekewe bure hapa? una matatizo ya uelewa.

Kwanza Lowassa hapo ilipotolewa hiyo habari hajapastukia, huyo jamaa alioanika hizo habari anaweza kushtakiwa akaishia kuhenyeshwa mahakamani kwa ujasusi. Ni kosa la jina kutangaza habari za biashara ya watu isiyo kuhusu. Tena tushtuwe ngoja swappable wa Lowassa.:

Hoyaa, Pasco. mshtuwe mzee huko ampelekeshe huyu jamaa wa fikra pevu mahakamani ndio atapokoma kucheza na moto. Zamani tulipokuwa wadogo tukichezea moto wazee walituambia "msichezee moto mtajikojolea kitandani" huyu kijana wa fikra pevu naona hajapata hilo funzo.

Yetu macho maana Lowassa alishatangaza bayana, wanaomchafuwa wakae tayari kuburuzwa mahakamani.
 
Siku moja wala sitoshangaa kuja kusikia kwamba yale magorofa makubwa sana pale eneo kati ya Muhimbili na Diamond Jubilee ni mali ya AL-SHAABAB kwa hisani ya baadhi ya wakuu wetu hapa hapa nchini.

Kumbe ndio maaana utajiri wote huu wa ghafla madili yenyewe ndiyo kama haya halafu wengine bila hata ya aibu wanaelezea wazi wazi tu humu eti MBONA HUU WIZI NI WA ZAMANI SANA NDIO MNABANDIKA leo hapa JF eeeh ....!!!

Back
Top Bottom