Fid-Q azindua kampeni ya kuhamasisha vijana kushiriki mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa Taifa letu

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
01.jpg

Msanii nguli wa miondoko ya Hip-hop Fareed Kubanda – Fid Q amekutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sports Lounge katikakati ya jiji la Dar es Salaam, kujadili maswala ya msingi yenye mustakabali chanya kwa maendelo ya taifa hili.

Ameitisha mkutano huu akiwa kama kijana na mwenye nafasi na ushawishi kwa vijana wenzie katika ushiriki wa kuleta mabadiliko chanya na maendeleo ya nchi yetu.

Fid Q amesukumwa kuzungumza na waandishi wa habari baada ya kutanabai kwamba vijana japo ni asilimia 80 ya taifa lakini hawana mwamko na msukumo wa kujitokeza kushiriki mchakato wa uchaguzi wa viongozi waowataka na wanaowaamini wanauwezo wa kuleta mabadiliko ya ki nidhamu kwenye masuala ya msingi ya taifa letu.

"Kuna kitu kimoja ambacho watu wengi hasa hasa vijana wenzangu hawakifahamu, Nchi yetu ni changa sana. Vijana nchi hii chini ya umri wa miaka 35 ni zaidi ya asilimia 80 ya idadi ya watu, wakati watu wazima zaidi ya miaka 60 ni asilimia chini ya 5 ya watanzania wote. Hizi ni takwimu za sensa iliyopita. Nimetanguliza takwimu mapema kwa sababu, twakimu huwa hazisemi uwongo.

Changamoto zinalolikumba taifa hili kwa kiasi kikubwa zinatuathiri sisi vijana wa nchi hii ambao ndio wengi wetu. Madhara yanayotokana na uongozi mbovu, vile vile yanatuathiri sana sisi vijana kwa wingi wetu. Tutake tusitake, ustawi na kunawiri kwa vijana ndio kutaamua mustakabali wa Tanzania, vijana tukilala basi na Tanzania pia italala." Alisema Fid Q.

Bado kuna changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa vijana. Vijana wengi wamezagaa mitaani bila shughuli za kufanya. Hata wale wenye degree hawana kazi. Vijana wanakata tama na kuona kwamba wao sio sehemu ya taifa hili.

Kuna changamoto ya viongozi waadilifu watakaosimamia kuhakikisha kwamba keki ya taifa inagawanywa kwa Watanzania wote na hailiwi na wachache.

Baada ya utangulizi huo, ni dhahiri kwamba kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa unaoendelea, na uchaguzi mkuu wa 2015 lazima vijana tuamke na tushiriki kikamilifu. Kwanza, vijana wenye uwezo na sifa za kugombea nafasi za uongozi ni lazima wafanye hivyo, pili vijana wenye vigezo vya kupiga kura pia ni lazima wafanye hivyo maana ni wajibu wetu, tatu, vijana ni lazima tushiriki kikamilifu katika mchakato wa kampeni ili kuhakikisha ishu zetu za msingi zinajadiliwa na wagombea na zinapewa kipaumbele.

Kama vijana wanakuwa na hofu basi niwakumbushe kwamba, Mwalimu Nyerere alikabidhiwa nchi hii akiwa na miaka 39 tu na kuanza harakati za kupigania Uhuru ambao tumeuenzi jana. Alikuwa ni kijana mdogo tu.

Mzee wetu Dr. Salim Ahmed Salim alianza kuwa mwanadiplomasia mahiri akiwa na rika dogo tu, akiwa na umri wa miaka 22 alikuwa Balozi wa Tanzania, nchini Misri. Mifano ipo mingi, hivyo vijana tusipate woga – Tumechangia kupatikana kwa Uhuru na kujenga nchi hii, na sasa ni wakati mwingine tena wa kuibadilisha nchi yetu.

"Hivyo mimi Fareed Kubanda, nimeamua kufanya matamasha ili kusimamia haya niliyoyasema hapo juu. Kwa kutumia nafasi zenu ndugu wana habari naomba mnisaidie kutangaza azma yangu hii pamoja na nitawapigia baadhi ya wasanii wenzangu kuwaomba waniunge mkono ili tufanikishe hili na tushiriki katika kuleta uongozi utako leta mabadiliko tunayoyataka na kwa kasi yetu sisi vijana."

Fid Q aliendelea "Ninatumaini kwamba wasanii wenzangu wataniunga mkono, ili kuanza kuwaamsha vijana wenzetu, tuweze kutimiza wajibu wetu wa kihistoria wa kufanya mabadiliko katika nchi yetu, hasa pale tunapokuwa tunahitajika sana na jamii.

Tayari nimefanya mazungumzo na Mkubwa Fela, Babu Tale, Mwana FA, Nick wa Pili, Lamar, P-Funk, Mwasiti, Barnaba, Ditto ambao wamekubali kuwa sehemu ya harakati hizi. Bado nahitaji wasanii wengine wengi washiriki ki mawazao, hali na mali kufikia lengo kuu la Tanzania mpya na bora zaidi".

Huu ni mwanzo wa harakati hizi, mwakani tutafanya amsha amsha kubwa ya vijana. Mwaka huu tunasema Tuonane January (#Tuo8January). Tutengeneze nchi yetu.

Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.

Chanzo:Bongo 5
 
kuna harufu chama flani kitajinasibisha hapo na hiyo ndio itavuruga mambo yote. Sababu tupo ambao hatuamin kwenye hio milengo yao

Yaaani hamna kitu hapo..Mtaniambia Mungu akitupa uzima... Hapo Lazima kuna [_______________] Nyuma nyuma yao.
 
Kwa ufupi ukishamtaja Barnaba,Mwasiti na Mwana FA kwa harakaharaka nachelea kusema watamezwa na mkondo wa chama fulani na itakuwa ndo mwisho wao
 
kama nia yao ni mbaya watashindwa na ndio utakuwa mwanzo wa poromoko lao. Bora wajiingize jumla waeleweke misimamo yao kama akina sugu na profesa J kuliko ku-beep, itawagharimu. Wachukue uzoefu wa yule mwenzao Marlow!!
 
Mara wao ndo wanatumika kuhamasisha watu wajae kwenye mikutano ya CCM ambayo washabikiwa wao hawaipendi. Je kutumika vibaya si ulimbukeni?? Je wasani wetu ni limbukeni sana kiasi kwamba ni zero brain??

Kuna mifano ya wasanii maarufu kutumika kwa kuitafutia wateja CCM, chama ambacho kimeua uchumi wa nchi hii, je msanii kioo cha jamii alipaswa hata kuwa na simu ya kiongozi wa CCM yoyote??? hata wa mtaa tu???

Juzi kati Jokate anadai eti January anafaa kuwa rais, anampenda Zitto eti vile anatetea na ni sauti ya wanyonge??

Huko nyuma tumeona Barnabas, Marooooo na wenzake eti wanaume wakifanya ujingaaa wa kupindukia kisa hela, kusaidia watu wake kuibiwa ni ni kushiriki wizi??? Marooo unaakili ulifanya haya hapa TZ na bado unataka upate mkate kutoka kwa hawa unaowapeleka wakaibiwe, kweli msanii TZ ni divisioon Zero yakufikia.

Yuko Kala Jeremaya eti naye akaja na singo EL awe rais, kweli umekosa kufikiria kazi safi unakuja na kumsifu mtu hopeless kabisa kama huyu? Nakaya naye alitegemewa kama Kala, muulize pengine aliishia kukaa uchi tu.

Yule mke wa wote naye pale kanisani, Flower Basha naye pamoja na Mungu aliyenaye, pamoja na ukaribu na mchungaji wake, amemuasi mumewe na Watz kwa kutumbuiza kwenye matamasha ya kualika watu waje kuibiwa na CCM, kweli ukiwa kanisani nakusimkia unaimba kwa kipaza sauti unaona ni sawa utumike na mungu hapo hapo ukitumika na shetani kama CCM??

Hongera Jo Makini, Hongera Mr. II, Hongera MwanaFA, Hongera Prof Jay, Hongera Lady JD, hongereni sana maana ktkt ya bahjari la wajinga, hakika mmeonesha kuwa kuna matumaini juu yenu.

Ni vema wasanii mkawa kioo cha jamii kwa kuonesha wapi twende, tena mpinge wizi wa CCM na serikali yake hadharani sio kugombea pesa zao harafu mnajifanya tuwaheshimu. Wasanii duniani hukomboa na kupigania haki za washabiki wao. Je wewe unafanya nini TZ???

Nawasilisha
 
Hongera Jo Makini, Hongera Mr. II, Hongera MwanaFA, Hongera Prof Jay, Hongera Lady JD, hongereni sana maana ktkt ya bahari la wajinga, hakika mmeonesha kuwa kuna matumaini juu yenu.

Hongera Afande Sele
 
wanatafuta promo tu....hao wasani...
vijana washaamka wenyewe kitambo tu....
 
Wanakampen hawa hapa. ..kuweka picha zao sina maana wanaenda kufanya waliofanya 2010 may be watakuwa wamejirekebisha labda kampeni ya sasa hivi ni ya mabadiliko ya vijana kiukweli. .ila sdhan
 

Attachments

  • 1418373588903.jpg
    1418373588903.jpg
    11.8 KB · Views: 1,035
  • 1418373639239.jpg
    1418373639239.jpg
    77.1 KB · Views: 207
Wanakampen hawa hapa. ..kuweka picha zao sina maana wanaenda kufanya waliofanya 2010 may be watakuwa wamejirekebisha labda kampeni ya sasa hivi ni ya mabadiliko ya vijana kiukweli. .ila sdhan

hao ni ccm maslahi......tu, mimi siamini eti msanii ana hamasisha kitu fulani sana sana hao watatumiwa na ccm tu
 
Hawo ni ccm kwani huyo fela ni gamba damu, na kwa habari za uhakika ccm ndio wako nyuma yao.

Hivi kweli waTanzania hatuwezi kuunga mkono juhudi zozote zilizo na mtazamo 'chanya' kwa ustawi wa nchi yetu bila kuweka 'politiki'!? Naanza kuchukia siasa...nawachukia CCM toka zamani, naanza kuwachukia CHADEMA, naanza kuchukia UKAWA...nachukia wanasiasa chama tawala na upinzani amabao wanatu'zeveza' waTanzania kiasi cha kuua harakati zozote zenye mrengo wa kukomboa nchi yetu!
 
Wanakampen hawa hapa. ..kuweka picha zao sina maana wanaenda kufanya waliofanya 2010 may be watakuwa wamejirekebisha labda kampeni ya sasa hivi ni ya mabadiliko ya vijana kiukweli. .ila sdhan
Hawajawahi kubadilika hao .
 
Hivi kweli waTanzania hatuwezi kuunga mkono juhudi zozote zilizo na mtazamo 'chanya' kwa ustawi wa nchi yetu bila kuweka 'politiki'!? Naanza kuchukia siasa...nawachukia CCM toka zamani, naanza kuwachukia CHADEMA, naanza kuchukia UKAWA...nachukia wanasiasa chama tawala na upinzani amabao wanatu'zeveza' waTanzania kiasi cha kuua harakati zozote zenye mrengo wa kukomboa nchi yetu!

Sio kwamba hatutaki kuunga mkuu tatizo wanazipanga harakati wenyewe sio wazalendo wala wanachotaka sio maendeleo chanya unayosema wewe. .mfano mzuri ni 2010 ngwear RIP.marlaw. fid q na mwana FA walitukusanya kwenye kampeni mwisho wa siku kumbe wanampigia debe jk na yakatukuta yaliyotukuta wakachukua Chao leo sisi ndo tunaumia. Kwa iyo tumewachoka..ila sina hakika hii kampen ya tuonane January inamalengo chanya au ndio yale yale ya 2010. ..hivyo ni sisi vijana kuwa makini kwenye izo kampeni tukikuta wanaongea pumba zao ni kuondoka na kuwaacha wenyew. ..but kama watarudia ya 2010 wanaiabisha HIP HOP saana maana hii sio misingi na utamaduni wa HIP HOP
 

Attachments

  • 1418375528551.jpg
    1418375528551.jpg
    62.3 KB · Views: 153
Back
Top Bottom