FFU wamezunguka Ikulu. Kuna tishio la kuvamia Ikulu?

Status
Not open for further replies.
Sio Nchi tuu, hata Chama Cha Mapinduzi chenyewe hakitawaliki. Tuliambiwa Gamba - limeshindikana, Tukaambiwa Wajipime Wenyewe - Imeshindikana. Makundi yamepamba moto, sumu wanatiliana na bunduki kuonyeshana. mwaka wa kufa CCM miti yote huteleza

GAmba limekwama kiunoni!! ha ha ha ha !!! by Chenge
 
Rais wao, Chadema wakiandamana wanasema eti kwa vile Rais ni mwislamu.
Maandamano yaliyotokea toka jamaa awe Rais yanalingana na idadi ya safari zake za kwenda nje, inaeleweka
 
tz kila siku burudani, jk aliaambiwa kichakachua nchi haitatawalika, ndivyo inavyotokea, si mmeona
 
Unajua sehemu yenye joto kubwa tayari na vitu vinavyoweza kuwaka moto, hata ukisugua chuma tu, cheche zinaweza kuwasha moto.

Haya mambo ya sensa na nini kama maisha yangekuwa mazuri kidogo tu watu wasingeshiriki sana kuyapinga, lakini sasa hivi huhitaji hata kuwahubiria sana watu wajiunge na maandamano ya kuipinga serikali, kwa sababu serikali yenyewe inaonekana haijali wananchi na haitumii akili.

Hivi serikali ingekubali hilo swali la dini kwenye sensa hawa waliodai wangefanya nini baada ya kuhesabiwa na kuambiwa waislamu wako asilimia fulani?
Wangesema sensa ni ya uongo, kuna watu hawakuhesabiwa.
 
Wewe hakika ni kiranga. Hivi kipengele cha kidini kinatusaidia nini zaidi ya ndoto za alinacha za kufikiri kwamba idadi ikionyesha waislamu ni wengi siku moja nchi hii itakuwa ya kiislamu!!!!!!!!!!!!!! Kama mnataka idadi ya waislamu kwa sababu tofauti na niliyokueleza, kaitafuteni misikitini na kwenye taasisi zenu za kiislamu. Hii nchi haijawahi kuwa, haiwi na haitakaa iwe ya kiislamu mpaka Yesu atakaporudi.
 
Mkuu acha utani. Usogelee "kitu kizito" ukipige picha? Nilipita fasta nikawa na wasiwasi labda kuna uasi umetokea ikulu nisijepigwa na "kitu kizito"
Mbona Picha zinawezekana kabisa Mkuu. Ningefanya hili sema tu nipo eneo lina connection slow sana leo. Nenda Google Earth, tafuta kitufe cha picha za satellite ya wale majamaa zenu vichwa ngumu CIA, tafuta Dar es Salaam, kisha scroll hadi Magogoni Ikulu. Gari la washawasha litaonekana. FFU nina hakika hawataonekana kwa sana ila nadhani wangekuwa wamejipanga katika formation zingeweza onekana. Gari la washawasha litaonekana bila tabu. Kama upo eneo lenye Internet fast speed hebu tuwekee picha humu mwana wani.
 
Wamalize ishu tu, ili huyu ****** awe historia. He's has been a MASSIVE LIABILITY to Tanzania
 
Kwa nini wakalinde ikulu hawa coward wakati wanaotishia wanajulikana kwani ni rahisi kuwakamata kwa kutumia nguvu ndogo kuliko wanayoweka hapo Ikulu. Hivi hawa wakija na yale mabomu ya Alshababu mpaka pale Ikulu mabomu ya machozi na maji washa si yatatelekezwa huku kila mtu akiokoa maisha yake. Ningefikiri Polisi wangewafuata huko huko wanakopangia kuja Ikulu wawasambaratishe.
 
Wangesema sensa ni ya uongo, kuna watu hawakuhesabiwa.

Unajua mtu unapoingia katika malumbano na mtu mchokozi, kama wewe ni muungwana, huna budi kumpa nafasi mchokozi audhihirishie ulimwengu kwamba yeye ni mchokozi. La sivyo wewe unaweza kuonekana ndiye mchokozi.

Na kuna sehemu ambapo hili jambo lingefika, kama hawa waislamu kweli wana nia ya uchokozi, serikali ingeweza kuthibitisha kwa ulimwengu kwamba hawa watu ni wachochezi tu.

Kwa mfano.

Wameanza kwa kutaka swali la dini liwe katika sensa, mmewaambia kuhesabu watu kidini katika sensa si sawa kwa mujibu wa serikali yetu. Wakakazania, mkawaambia jihesabuni wenyewe kama mnataka, wakakazania kuhesabiwa kisensa, mkakubali.

Mkawapa figures, wakazikataa.

Hapo wenye kuangalia mambo wataona kuna jingine.

Serikali itakuwa na mwanya wa kuwaambia "kama hamzikubali figures zetu fanyeni hesabu wenyewe, in fact tuliwaambia tangu mwanzo mjihesabu wenyewe".

Hapo sasa wakileta fyokofyoko na maandamano, hata kama serikali ikiwapiga risasi kwa jina la "usalama wa taifa" watu tunaoangalia reason na logic, hatuwezi kuilaumu serikali.

Lakini leo serikali imewapa hawa watu msemo, ikiwapiga risasi kwenye maandamano itaonekana serikali dhalili inayoogopa watu wake yenyewe.
 
Unajua mtu unapoingia katika malumbano na mtu mchokozi, kama wewe ni muungwana, huna budi kumpa nafasi mchokozi audhihirishie ulimwengu kwamba yeye ni mchokozi.

Wakatoliki hujihesabu wenyewe kupitia vigango majimbo na parokia, nazani na wenzetu wangetumia utaratibu huu ingekuwa rahisi sana.
Lakini mie binafsi sioni kama kuna tatizo kuingiza kipengele cha dini ili vile vile wale wachache wajue walenge wapi kupata wafuasi na wenye waumini wengi wajue wapi kwa kujenga nyumba zaidi za ibada
 
Unajua mtu unapoingia katika malumbano na mtu mchokozi, kama wewe ni muungwana, huna budi kumpa nafasi mchokozi audhihirishie ulimwengu kwamba yeye ni mchokozi.
Give then a Yard they Take a Mile....

Mkuu haya yote yameletwa na hii serikali kuwa lege lege, na kukosa msimamo (na hapa wamesha-open a pandora box) hivi kwanini tusiendelee na kwamba serikali haina dini.., mambo yoyote kuhusu dini hayawahusu after all hizi data za sensa zipo pale kuleta huduma sasa kujua tuna wa-Hindustan wangani ili iweje ?, kwani tunajenga mahekalu hapa ?
 
Wewe hakika ni kiranga.

Naam, cha Ngeda Sangala Kandumbwa

Hivi kipengele cha kidini kinatusaidia nini zaidi ya ndoto za alinacha za kufikiri kwamba idadi ikionyesha waislamu ni wengi siku moja nchi hii itakuwa ya kiislamu!!!!!!!!!!!!!!

This is what I call jumping the gun, guilty until proven innocent mentality.

Hata kama kuna watu wanataka kuifanya nchi hii iwe ya kiislamu kwa namna hiyo uliyoisema, watu hawa si peke yao wanaotaka kujua idadi ya watu kwa dini Tanzania.

Kuna demographers wasomi wanaoinfluence public policy wanahitaji habari hizi (nishaongea sana kuhusu umuhimu wa hizi demographics katika public policy, kuanzia birth control issues, HIV/AIDS fight mpaka elimu na afya kwa ujumla)

Hii dhana ya kwamba "yeyote anayetaka kujua breakdown ya idadi ya watu kidini ni uamsho" ni intellectual lazyness.

Na kama vile ambavyo serikali haiwezi kukataza watu kuendesha magari kwa sababu baadhi ya magari hupata ajali, serikali haitakiwi kukataza swali la dini kwa sababu kuna uamsho wachache wanaotaka kutumia hizi figures kuleta mgawanyiko wa kisiasa.

Sipendi mtego wa panya unasao waliokusudiwa na wasiokusudiwa. Hii habari inawapunja wasomi wanaotaka kujua mgawanyiko wa watu kidini kwa sababu genuine za research. Kama kuna watu wanataka kuleta vurugu, tuende na sheria, tuwaaache wapange, tunase ushahidi, mkondo wa sheria ufuatwe.

Sio kuhukumu mtu kwa sababu "huyu atakuja kuwa mwizi baadaye" kabla hata wizi haujafanyika.

Kama mnataka idadi ya waislamu kwa sababu tofauti na niliyokueleza, kaitafuteni misikitini na kwenye taasisi zenu za kiislamu. Hii nchi haijawahi kuwa, haiwi na haitakaa iwe ya kiislamu mpaka Yesu atakaporudi.

Demographers wenyewe wanasema figures zinazokubalika kabisa ni za sensa za serikali.

Ushasema uamsho wanataka kutumia sensa kwa sababu ya kisiasa kuifanya nchi iwe ya kiislamu, sasa utawaaminije wafanye hesabu ya kweli wakati wana a political agenda? Huoni kwamba una ji contradict hapo?

Hebu msikilize msomi huyu anavyo endorse figures za sensa kama ni the most reliable.

Bila figures za sensa presentation ya kisomi kama hii haiwezi kuwapo.

[video]http://www.ted.com/talks/hans_rosling_religions_and_bab ies.html[/video]
 
Wakatoliki hujihesabu wenyewe kupitia vigango majimbo na parokia, nazani na wenzetu wangetumia utaratibu huu ingekuwa rahisi sana.
Lakini mie binafsi sioni kama kuna tatizo kuingiza kipengele cha dini ili vile vile wale wachache wajue walenge wapi kupata wafuasi na wenye waumini wengi wajue wapi kwa kujenga nyumba zaidi za ibada

Sawa, waingize hicho kipengele lakini isiwe lazima kukijibu.

Kwa hiyo wanaotaka kujibu rukhsa, wasiotaka nao rukhsa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom