Festus Makerubi wa TBC1 na Mbwembwe Zake

Baadhi yenu huyu Brother sio mgeni kwenu.Wale mnaofuatialia mziki huu wa kusifu na kumtukuza mungu nadhani mnamfaham zaidi.Jamaa anamudu vizuri sana kipindi chake hasa anapochombeza na zile mbwembwe zake za kuigiza nyimbo za waimbaji, ukijumlisha na kile kisauti chake kinacho enda sambamba na kicheko chake.Nampongeza kwa hilo.Ila kuna wakati flani nahisi kama anapitiliza,mikogo inakuwa mingi sana mpaka anaboa,akianza kusifia jambo atasifia mara mbili mbili mpaka inakuwa kero.akianza kucheka ndio usiseme atacheka weeeee....... anyways huo ni mtazamo wangu tuu sijui wa kwenu wadau.
Hivi Kumbe bado kuna watumnaangalia tbc mpaka Leo?
 
Hapo nadhani ndio anapokosea.anatakiwa kutoa haki sawa kwa madhehebu yote na sio kupendelea sana RC peke yake.BTW alikuwa ni mwanakwaya wa RC kanisa la Mwenge sijui kama bado anaendelea.
Rc mwenge, unamaanisha lile kanisa la mt maxmillian kolbe-mwenge ukivuka TRA kama unaelekea Afrika sana?
 
Mi nashauri atofautishe style ya kutangaza katika vipindi. Sioni tofauti anaposhika kipindi cha Tumwimbie Bwana na kile cha Zamadamu. Vicheko ni vilevile, mtiririko wa sauti ni uleule, mbwembwe na sifa ni za aina ileile. Mabadiliko ya style humvutia mtazamani, akawa na hamu ya kuendelea kuangalia/kusikiliza - bila kuchoka au kuwa bored. Nadhani inawezekana, au?
Hiyo ndio style yake.... Ndicho iamtofautisha yeye na wengine kwenye utangazaji......asingekuwa na kitu tofauti tusingekuwa twamjadii hapa
 
Baadhi yenu huyu Brother sio mgeni kwenu.Wale mnaofuatialia mziki huu wa kusifu na kumtukuza mungu nadhani mnamfaham zaidi.Jamaa anamudu vizuri sana kipindi chake hasa anapochombeza na zile mbwembwe zake za kuigiza nyimbo za waimbaji, ukijumlisha na kile kisauti chake kinacho enda sambamba na kicheko chake.Nampongeza kwa hilo.Ila kuna wakati flani nahisi kama anapitiliza,mikogo inakuwa mingi sana mpaka anaboa,akianza kusifia jambo atasifia mara mbili mbili mpaka inakuwa kero.akianza kucheka ndio usiseme atacheka weeeee....... anyways huo ni mtazamo wangu tuu sijui wa kwenu wadau.
Nyimbo nyingi za Wakatoliki Zinaboa. Awekw Gospel na hymn tofauti tofauti
 
Kile kipindi cha kumsifu Mungu nakiita Makerubi, napenda kuwaambia watoto wangu, njooni sebuleni mumsikilize Makerubi. Ama kweli anakimudi, big up!
 
Back
Top Bottom