FEMI (play boy)

paartey

Member
Jun 26, 2023
39
53
FEMI (play boy)

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 01

MAWASILIANO: 0783642467

Anza nayo.....

Femi kijana fulani hivi machachali ambaye shida anaisikia tu kwa wengine wanavyosema maisha ya shida maisha sijui hivi, Femi amezaliwa kwenye familia yenye pesa sana ambapo baba yake na mama yake mzazi wamekuwa wakiishi Marekani miaka na miaka, ila femi alibaki Tanzania akiwa na bibi yake yaani bibi alimtaka mjukuu wake bibi pia yuko vizuri sana kwenye mambo ya pesa lakini hakuwa bibi yule mzee watu wangu wa nguvu wanasemaga wabibi wa mjini bibi amekuwa akimuacha mjukuu wake afanye kile anachokisikia bibi anahakikisha account ya mjukuu wake iko full mda wote anafanyiwa anachokitaka picha linaanza nyumbani kuna wadada wa kazi wawili na mkaka wa garden mmoja

Femi amekuwa mtu wa kulala na kuamka tu agusi kitu chochote zaidi ya simu yake na kula tu sio mtu wa kufanya kazi ata kufua anafuliwa na wadada wake na kama wewe ni mfanyakazi wa ndani halafu ukamfanya femi kuchukia basi vita itaama kutoka kwa femi mpaka kwa bibi yake.

SONGA NAYO....

Ilikuwa siku ya jumanne kama kawaida shughuli za hapa na pale ziliendelea kijana femi majila ya saa nne (4) asubuhi ndio alikuwa anatoka usingizini yaani ndio anaamka

"Brandina nani anatakiwa kufanya usafi ndani kwangu ?"

Aliuliza femi baada tu ya kutoka chumbani kwake na kwenda sebuleni, brandina ni mmoja kati ya wafanyakazi wao

"Ni mimi nilikuwa nikisubili uamke...."

"Kafanye chap nina mgeni wangu anakuja muda sio mrefu nisingependa apakute vile....."

"Sawa kaka...."

"Wewe hivi hayo mambo ya kuniita kaka nimekuambiaje ?? Eeeh mimi sio kaka ako halafu unataka nikose nini kutoka kwako ?? Usije ukaru......."

Kabla hajamaliza kuzungumza simu yake ya mkononi iliita

"Hallow..."

Alizungumza femi baada tu ya kupokea simu akakaa kimya kwa muda akisikiliza sauti ya upande wa pili kisha akaendelea

"Aaah ndo hivyo fanya kweli kwenye presentation me siji leo subira anakuja nyumbani nitakuwa nae....."

Waliongea sana baada ya muda akarudi chumbani kwake

"Mbona mashuka ubadilishi sasa ??"

"Eeeh....."

Alimuuliza brandina ambaye kwa kumtazama tu unajua kuwa alikuwa akimuogopa sana femi

"Nikuulize kitu brandina wewe uwa ausikii vizuri au mtu akizungumza unakuwa na mawazo yako mengine ??"

"Nakuelewa kaka "

"Sasa unaniuliza mara mbili mbili ili iweje ??

"Samahani, naomba nibadilishe na nimalize kufanya usafi nitakuita "

"Unataka nikakae nje ?? Una akili wewe ? Halafu embu njo....."

Femi alimuita brandina kwa dharau sana brandina alizidisha uoga na kubaki akiwa ameganda tu na kumtazama femi kwa wasiwasi

"Njoo basi..
."

Alizungumza femi na alipoona kuwa brandina amfati akainuka alipokuwa amekaa na kumsogelea zaidi

"Hivi ujawai kufikilia kuwa na mimi ?? Yaani na uzuri wangu huu unakubalije kutandika kitanda kwaajili ya wenzio.??"

Alizungumza femi uku akijaribu kumshika shika brandika

"Kaka femi niachie nimalize kazi natakiwa kwenda sokoni pia "

Alilalamika brandina lakini malalamiko yake hayakufua dafu femi alionesha kudhamilia kufanya jambo baya kwa brandina wa watu ambaye alionekana kuwa msichana mpole na mtulivu sana

"Kaka femi......"

Ilisikika sauti ya juu sana ikiita kutokea sebuleni hapo femi alistuka na kutoka ili kujua nani alikuwa akiita hakuwa mwingine Bali ni mdada wa kazi mwingine aliyejulikana kama zuhura

"Kuna mgeni wako huyu sijui unamafahamu"

Alizungumza zuhura uku akioneshea mkono mlangoni

"Oooh subira wangu jamani karibi kipenzi "

Alizungumza femi na kumfata subira na kumkumbatia

"Karibu sana nimefurahi kukuona "

Alizungumza femi kwa furaha sana muda wote huo zuhura alikuwa ameganda akimshangaa femi

"Kaendelee na kazi zako "

Alizungumza femi na zuhura hakuwa na namna zaidi aligeuka na kutoka kuelekea jikoni

"Oooh utamletea juice chumbani na sambusa "

Alitoa oda femi na msichana yule alifanya kama ambavyo aliagizwa....

"Ujamaliza tu kufanya usafi ??"

Alifoka femi akimfokea brandina kuwa amechelewa kufanya usafi

"Baby ongea nae taratibu ata hivyo mimi nipo leo nafikili kilichobaki ni mimi kushika majukumu yangu "

Alizungumza subira akiamini kuwa kuletwa kwenye nyumba hiyo ni kweli anapendwa eeeh hayo mawazo kwa mwanaume huyu yaani huyu femi ondoa kabisa anachojua yeye ni shwaaaaah..... kupita na wadada yaani hakuna mdada mzuri anayepita kwenye macho yake bila yeye kummezea mate lakini pia michezo yake amekuwa akiicheza kwa akili sana anaweza akatembea na wasichana kama watatu tena marafiki na wasijuane yuko vizuri sana femi ni kijana wa ovyo hakuna mjadala.

Basi mwaya subira wa watu pasi na kujua kuwa chumba iko ni kama dangulo alifanya usafi ulioenda shule alifanya kila kitu kama mwanamke aliyeolewa na kujali familia yake, hakuishia hapo tu alitoka nje na kwenda kuungana na wafanya kazi kwajili ya kuandaa chakula

"Leo nipo kwaajili yenu jamani msinionee huruma ni wajibu wangu "

Hayo maongezi kwa muda huo yalikuwa yakifanyika jikoni ambapo subira alikuwa bize na mapishi na kila kitu alifanya mwenyewe hakuitaji ata kusaidiwa

"Lakini madamu akikukuta unafanya kazi kama hivi tutagombezwa sana "

"Wasiwasi wenu nini ?? Wifi yenu na nusu nishafika kila kitu kitakuwa sawa...."

Ila subira mbwa huyu atakuja kulia vibaya akija kujua kuwa anapitiwa tu maana daaah ameamua kujiveka majukumu makubwa mno.....

"Demu mazinguo huyu tangu amefika anaangaika na kufanya kazi za ndani ananikera hatari can you imagine tangu amefika yuko bize na kazi za ndani kama roboti wala hayuko romantic "

Alilalamika femi akiwa kitandani kwake na alikuwa akiongea na rafiki yake ambaye walionekana kuwa na karibu sana....

Baada ya muda subira alipakua chakula na bila kupoteza muda alichukua chakula na kumpelekea femi na sio tu kumpelekea alimlisha kabisa ila mbwa huyu namuonea huruma femi sio wa hivyo kabisa..I.......

Majila ya saa 2 usiku bi femi alikuwa amesharudi nyumbani alimkuta subira na walika kwa muda wakazungumza mawili matatu, sasa baada ya yote muda subila kuondoka uliwadia femi hakuwa na budi kumuaga ile wanatoka tu nje ya geti waka.....Waka......

ITAENDELEA
 
FEMI (play boy)

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 02

MAWASILIANO: 0783642467

SONGA NAYO.......

Ulikuwa ni muda ambao subira aliamua kurudi nyumbani kwao baada ya kutumia siku nzima akiwa kwa kina femi, sasa ile wanatoka tu getini walikutana na msichana fulani hivi mzuri mno akiwa anashuka kwenye bajaji femi alistuka baada ya kumuona lakini msichana yule akampungia mkono femi uku akiwa anatoa pesa kwenye wallet kwaajili ya kumlipa dereva bajaji, kwa wasiwasi femi alimkimbilia msichana huyo ambaye alikuwa hatua chache kutoka pale alikokuwa amesimama subira.....

"Nani yule....??"

Aliuliza msichana yule ambaye ndio kwanza alikuwa amefika

"Ona sasa unavyopaniki si nilikuambia kuwa leo nina mgeni, huyu ndiosichana ambaye nilisoma nae tangu shule ya awali tumelelewa wote lakini kwa sasa ana makazi yake namaanisha ameolewa amekuja leo kuniona kaka yake lakini pia na bibi si unajua tena "

"Dada nipe hiyo hela niondoke unanipotezea muda"

Alifoka dereva bajaji ambaye aliona kuwa anapotezewa muda wake kwa kusimama pale ikiwa wao wanapiga soga basi msichana yule aliyeonekana kuwa classic sana akatoa not ya sh. 10000 na kumpatia dereva bajaji

"Keep change broh "

Aliongea msichana huyo kwa dharau

"Actually, naomba umfikishe huyu nyumbani kwao "

Aliongea femi uku akioneshea mkono kwa subira ambaye aliganda akiwaangalia tu na asielewe nini kinaendelea....

"Oooh wifi yangu naona tunapishana tutaongea siku nyingine....."

Alizungumza msichana yule ambaye ndio kwanza alikuwa amefika, neno wifi lilimchanganya sana subira na kuhisi kuwa yule ni dada wa femi ila femi walahi mbingu ataisikia subira wa watu kwa mahaba mazito alimsogelea msichana huyo na kumkumbatia kisha akaaga na kuondoka

"Waoooooh dada yako anaonekana kuwa mtu pisi sana "

Alizungumza msichana huyo ambaye kwa majina anajulikana kama rose

"Let's go baby......."

Basi kwa siku hiyo moja femi alikuwa na wanawake wawili kwa muda tofauti na kila mtu aliamini kuwa yeye ndiye mchumba wa femi.....

"Oyaaaah mwanangu jana kuna demu alikuwa anakutafuta hatari alisema anasoma business bachelor "

"Mmmmh ni nani ??"

"Aaah sikumbuki jina lake lakini nilimwambia kuwa unaumwa umeshindwa kuja...."

"Aaah hapo nimekupata amenicheki huyo demu nilikutana nae kwenye geti la chuo hapo nje naona ameanza kuingia king....."

"Ila mzee baba punguza tutakuzika na kilo mbili (2) upitwi yaani "

"Weeeh najua kujilinda acha kabisa......"

Yalikuwa ni mazungumzo kati ya femi na rafiki yake ambaye alionekana kumjua sana femi na tabia zake za kubadilisha wanawake kama daladala au chakula maongezi yao yalikatishwa na lecture ambaye kwa muda huo ndio ilikuwa ni kipindi chake hivyo aliiingia kufundisha......

Tabia za femi ziliendelea kuwa hivyo kubadili wanawake na hakuna mwanamke ambaye aliweza kumkataa....

Hatimaye semester ziliisha na likizo iliwadia kama kawaida likizo zake uwa anaenda marekani kwa wazazi wake na likizo inapoisha uwa anarudi Tanzania.

Vyuo vilifunguliwa na ilikuwa mwaka mwingine tena kwa wanafunzi wa chuo ambapo yeye femi alikuwa anaingia mwaka wa pili, siku ya kwanza kama kawaida lazima ukutane na wale wanafunzi wa mwaka wakwanza femi alikuwa akimuangalia kila msichana na kuthaminisha kama anafaa kuwa na yeye au laah, orientation ziliendelea kwa wale wanafunzi wageni na week ya pili masomo yakaanza lakini femi hakuwai kubadilika kabisa....

"Weeeh kuna demu nimemuona nimefatilia taarifa zake nimembiwa anaitwa Mere, kaka huyo nikimpata tu basi femi mimi naachana na kila kitu, yaani naachana na hawa wanawake wa hovyo wanaonipendea uzuri na pesa "

"Broh bhana hizo story zako ongea na hao wasiokufahamu ila sio mimi, yaani me nakujua mpaka nakujua tena utazani nimekuzaa "

"Ubaya wako ujawai kuniamini na kwanza ujamuona huyo mere ukimuona tuwenyewe lazima utulize komwe lako na maneno utaweka pembeni na kubaki ukinisaidia kumpata "

"Sijui labda....."

Story za hapa na pale ziliendelea wakimjadili mere na kama atajwi hivi muda huo huo aliwasili huyo mere yaani alikuwa anapita kwenye eneo ilo walahi ata mwandishi wenu nawahakikishia kuwa mere ni chombo yaani mwanamke fulani hivi daaah me mwenyewe nilipomuona kwanza nilipagawa mtoto kirangi cha mtume mweupe peeeh tena sio weupe wenu wa mkorogo hapana yaani mweupe rangi yake ya kuzaliwa na hakuwa na doa, kwa muda huo mere alikuwa amevalia skin jeans yake nyeusi na t-shirt ndogo ndogo iliyoendana mwili wake, kipochi chake pambe mwenyewe, na miwani ya macho ile ya kisasa, halafu na wigi lake original kabisa, mere hakuwa peke yake alikuwa na rafiki zake lakini uwezi amini femi alikuwa akimuona mere tu huyu kaka jamani.

"Kaka umeona kitu iko ??"

Aliuliza femi akimpa taarifa rafiki yake kumbe sijawatajia jina la rafiki yake ni Frank jamani mkaka fulani mzuri sema hakuwa na pesa kama femi.

Femi alimuuliza rafiki yake kama amemuona mere lakini muda wote huo frank alikuwa ameachia mdomo wazi akimshangaa binti mere.....

"Kaka mbona unakodolea sana chombo yangu ??"

Aliuliza femi hapo sasa ndio aliweza kumstua mwenzio

"Mere sabiti "

Alizungumza frank akionesha wazi kuwa anamfamu mere maana alimtaja jina lake na kumalizia na jina la baba wa mere

"Unasema....??"

Femi aliuliza

"Aaah nasema chombo hatari "

"Broh si nilikuambia mimi yaani huyo ndo sitakuja kumchanganya nawanamke yeyote niamini mimi
...."

Alizungumza femi lakini frank hakujibu kitu zaidi alionekana kuwa mbali kimawazo....

Siku zilisonga uku femi akiweka mazingira safi kwaajili ya kumpata mere lakini kwa wakati huu frank aligoma kabisa kumsaidia mshikaji wake yaani alijitoa kabisa, na hakutaka kabisa mere awe na mahusiano na femi ingawaje hakuwa akifanya waziwazi lakini kwa mtu anayeelewa akiangalia mate matendo tu anaelewa....

"Nimemtumia maua na chocolate mere amepokea tena amenitumia na kimesaji cha Asante "

"Umetumaje umeenda au ?"

"Weeeh broh naweka mazingira sana kabla hajaniona, hii zawadi ya tatu anapokea pasi na kujua ni nani anampatia na anayenifanyia kazi hii yuko vizuri broh namuaminia jiandae kuwa shemeji wa mere....."

"Broh una uhakika kuwa unampenda kweli mere au ?? Kuna muda napata wasiwasi sana "

"Wasiwasi wa nini ?? "

"Unabadili sana wanawake, nawaza hao wanawake wakija kugundua kuwa unawadanganya na kuwachezea tu, broh tuachane na kila kitu turudi kwenye ukweli unatakiwa kuwaheshimu wanawake "

"Nimekuambia nataka kutulia kwa mere....."

Wakiwa wanaendelea na maongezi alikuja msichana fulani hivi wa kipemba aliyekuwa amevalia baibui nzuri ambayo kwa sasa hivi tunaita Abaya

"Kipenzi....."

Aliita mdada huyo na kumkiss femi

"Shem mambo...??"

Baada ya kumkisi femi akamgeukia frank na kumsalimia....

"Broh ngoja me niiingie library si bado uko na shem hapo ??"

"Poa poa....."

Frank aliwaaga na kuondoka....

ITAENDELEA
 
FEMI (play boy)

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 03

MAWASILIANO: 0783642467

SONGA NAYO.......

Frank aliondoka na kumuacha femi akiwa na mchumba wake huyo mwenye hasili ya kipemba maana rafudhi yake ilidhihilisha ilo....

"Siku ya nne leo upokei wala haujibu jumbe zangu una nini kwani ?"

Aliuliza msichana huyo...I..

"Aaah we acha tu sio wewe tu kila mtu kwa sasa siko sawa, yaani siko sawa ile ya kumaanisha kabisa nina mambo magumu napitia ndio maana ata simu uwa naweka kando "

"Niambie mpenzi wangu ni nini kina kusumbua ?? Niko tayali kusimama na wewe....."

Bhana weeeh femi zee la maigizo likaanza kuigiza sasa, yaani michozi tikatika mtoto wa kiume ila huyu kaka daaah apewe maua yake amejua kuchanganya wanawake na sio kuwachanganya tu amemfanya kila mwanamke ampende kwa dhati basi mwaya msichana wa watu hakuwa mbali na femi wake akamlaza kulifuani na kumbembeleza wadada wengine walikuwa wakiwaangalia tu wengine walikuwa ni wanawake wa femi walibaki wakishangaa na kujiuliza kuwa femi amepatwa na nini ?? Kama ujuavyo mazingira ya chuo....

Muda mfupi tu walikuja wakaka wawili ambao walikuwa ni marafiki wengine wa femi

"Broh nini shida ??"

Yaani kundi la kina femi walikuwa wamezoea kuitana broh uwezi kujua mkubwa nani mdogo nani kila mtu anamuita mwenzie broh

'Afadhali shemeji zangu mmekuja analia tu na kusema kuwa ana matatizo magumu anapitia....."

"Oooh femi....."

Mmoja kati ya rafiki zake alimsogelea na hapo femi alimkonyeza ilikuwa ni ishara tosha kabisa kwa lugha zao

"Shem huyu tuachie sisi atakuwa Sawa"

"Mmmh namuachaje mpenzi wangu katika hali kama hii ??"

"Hautuamini au ??? Tutaongea na mshikaji wetu then tutamaliza kila kitu....."

Msichana wa watu hakuwa na namna zaidi aliondoka akiwa na huzuni yaani alikuwa akimuonea huruma sana femi wake pasi na kujua kiwa alikuwa anaigiziwa

"Broh madrama mengi imekuwaje kwamba ujafika kwa lamatha mpaka mda huu ?? Saa hii tungekuwa tu akuona kwenye jua kali kulia unajua bhana...."

"Mnazingua mjue ? huyu demu king'ang'anizi sana yaani sina hisia zozote na yeye "

"Weeeh huyu si ndio demu alikua anakuendesha kinyama yaani ulikuwa kama chizi flesh....."

"Nimeshuka broh nimeshuka tena kwa kuruka kwenye tuta "

Ahaha alizungumza femi na wenzie wote walicheka story za hapa na hapa zilishika nafasi yake ila kundi la kina femi ukikaa nao usipocheka basi....

"Oy niaje ??"

"Safi....."

"Naweza nikaongea na Wewe ??"

"Hapana..."

Ni femi alikuwa kimuongelesha mkaka ambaye alijulikana kama Charles ambaye kwa historia fupi Charles ndio alikuwa mchumba wa yule binti wa kipemba, lakini femi alimlaghai msichana yule kwa pesa zake na kumfanya mkaka yule akataliwe adharani na yule binti, yaani aliachwa adharani na msichana yule alimchagua femi, hivyo basi takribani chuo kizima kinajua kuwa femi anadate na swaumu yaani msichana yule wa kipemba, ndio maana alikuwa na uhuru wa kuwa naye sehemu yoyote ile, ila sasa wenzangu na mimi tunafichaa kama bangi kila mtu tunapewa undugu mpya.....

"Nakuomba tuongee sisi ni wamaume na unajua ilo "

Femi siku hiyo alikuwa mpole sana na alikuwa akitamani sana kuzungumza na Charles

"Achana na mimi femi me na wewe hatuna kitu cha kuongea labda kama unataka kunidhalilisha kwa mara ya pili sawa "

Charles alionekana kuwa na hasira sana na femi na hakuweza kusahau kabisa matukio yaliyomkuta kwenye mwaka wa pili pale chuoni, Charles hakuweza kumsikiliza femi zaidi aliondoka na kumuacha femi akiwa amekaa pale peke yake hana cha kufanya mwaya

Siku zilienda kila siku akili ya femi ilikuwa ikimuwaza mere msichana aliyeonekana kuiteka zaidi akili ya femi kuliko kitu chochote

"Brothers kuna kitu nataka kuwambia....."

Muds huo femi na kundi lake walikuwa wamekaa darasani na lecture alikuwa mbele akiendelea kufundisha lakini femi akaanzisha story, wote wakageukia

"Kuna msichana anatesa sana akili yangu mafikili yeye ndio ameumbwa kwaajili yangu"

"Ni kuhusu mere tena jamani ?"

Alilalamika frank na kugeukia mbele hakutaka tena kumsikiliza mwenzie, na kwakuwa kelele ziliongezeka lecture aliwafukuza wote na kumuacha Frank tu ambaye alionekana kuwa bize na kumsikiliza mwalimu.....

"Halafu sasa hivi mbona kama wewe na frank amko sawa? Maana ulipo wewe ataki kabisa kukaa "

"Ata me sijui "

Yaani wamefukuzwa darasani ata awasikitiki ndio kwanza story zinanogaz waliongea mengi sana na baada ya muda femi akarudi nyumbani akiwa nawanamke

"Mmmmh kaka femi umezidi sasa "

Alizungumza brandina yaani msichana wa kazi

"Inakuhusu nini ?? Tena funga mdomo wako, sasa niharibie kwa huyu kama ulivyoharibu juzi uone kama sijakunyoosha "

"Unawapotezea muda wadada wa watu, hivi wengine una wakumbuka kweli ??"

"Brandina sio bure unanitaka....."

Yalikuwa ni Mabishano ya hapa na pale kati ya femi na mdada wao wa kazi ambaye hakupendezwa kabisa na tabia ya femi...

"Baby......."

Ilisikika sauti ya ukali kutokea chumbani kwa femi na msichana aliyekuwa ndani akatoka nje akiwa ameshika underwear yawanamke mkononi

"Hii ni ya nani.....??"

Aliuliza msichana huyo kwa hasira sana....

"Ya mwanamke wake aliyeondoka leo asubuhi "

Alidakia brandina ila huyu dada jamani kikorofi lakini kikishikwq kidogo tu na femi anatetemeka kama kifaranga cha kuku

"Baby nitakueleza...."

"Utanieleza nini ?? Tena umeweka chini ya mto na imevaliwa bora ingekuwa mpya ningesema ni zawadi lakini imevaliwa ??"

"Baby ni mimi niliivaa nikiwa naigiza kwamba ukija kuvaa utaonekanaje "

Kwanza hata msichana mwenyewe alicheka maana hakutegemea jibu kama ilo kutoka kwa femi yaani femi ndio alibajaribisha nguo ya kike kweli huyu kaka sio kabisa brandina alicheka mpaka akalala chini....

"Naondoka halafu mimi na wewe basi....."

Alifoka mdada huyo akaingia chumbani akachukua pochi yake na kuanza kuondoka alipofika mlangoni aligeuka nyuma na kukuta femi akiwa amekaa kwenye kochi akimusngalia tu anavyoondoka....

"Kwahiyo hata uniombi msamaha ?? Yaani ata unizuii unaniacha niondoke ?? "

Alilalamika msichana huyo ila girls bhana kuna Muda tunashindwa kujua mnataka nini kwani si niwenyewe kataka kuondoka....

"Me nitasema nini na wakati umeamua kuondoka yaani kosa dogo tu unataka kunifanyia na kusahau kuwa kiasi gani nakupenda sawa nenda...."

Alilalama femi na muda huo alikuwa anarusisha mpira kwa kipa yaani anaamisha lawama zake kwa msichana wa watu, femi aliinuka kwenye kochi kwa huruma na kutaka kwenda chumbani kwake.

"Nisamehe mpenzi wangu "

Khaaaah kama mapenzi ndo hivi jamani me basi yaanisichana wa watu ndio aliomba msamaha na mwisho wa siku akarudi chumbani au anakijiti cha uganga huyu femi maana sio bure.....

ITAENDELEA
 
FEMI (play boy)

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 04

MAWASILIANO: 0783652467

SONGA NAYO...........

Siku iliyofuata femi aliamka asubuhi sana yaani ilikuwa mapema kuliko kawaida mpaka wafanyakazi na bibi yake walikuwa wakimshangaa yaani huyu imekuaje leo ila sasa shoga yangu brandina ambaye kwa namna moja au nyingine amekuwa mkorofi sana kwa femi akaanza

"Weeeh mwenzetu umeota ndoto mbaya au ??"

"Unasemaje ??"

Yaani wabongo bhana unauliza swali na wewe unaulizwa pasi na kupewa jibu

"Umeota umekufa au maana sio kwa kuamka mapema kiasi iko "

"Brandina we siku yako moja tu nakuambia moja yaani moja subili uone "

Alizungumza femi lakini pia siku hiyo alizungumza kwa kawaida sana mpaka kila mtu ambaye anamjua femi ni mtu wa aina gani alishangaa sana, femi alimsogelea brandina chap akamshika mkono na moja kwa moja akawa anamvuta kuelekea chumbani brandina aliogopa sana na kupiga kelele lakini hakuna ata mmoja alimsaidia

"Umezidi mdomo tu muone femi mkomeshe huyo......"

Alidakia mfanyakazi mwengine uku akicheka sana, femi alifika chumbani akiwa na brandina alisogea na kufunga mlango vizuri....

"Acha ujinga na utoto nataka unisaidie kitu "

"Kitu gani ?? Kwanza angalia ulivyoniumiza "

"We nawe sasa ukishasikia mtu anataka msaada wako unavyoanza kulinga nakutoa chochote mtu wangu yaani ishu ya leo muhimu mno "

"Unavyojiongelesha kumbe ukiwa na shida zako unakuwa mpole sio ??"

"Unanichocha sasa na Madole yako nambie unanisaidia unisaidii ??"

"Unataka nini ??"

"Hayo ndo mambo sasa, sikia yaani leo ndio siku muhimu kuliko zote unazozinua wewe mshikaji wangu, leo nataka nikamfanyie surprise kubwa sana mwanamke nimpendae, achana na awa viruka njia ninaowaletaga yaani huyu ni mke wangu kabisa, ndio maana umjui "

"Kwahiyo me natakiwa kufanya nini ??"

"Cheza kama Pele mshikaji wangu, nichagulie nguo fulani hivi kali ya heshima kwanza ile nikimfata tu mwenyewe asemw kweli huyu ndo mchumba "

"Mmmh kaka una hekaheka wewe, utafika mbinguni umechoka haya kaa hapo nifanye kazi yangu....."

Basi brandina alifanya kila awezalo na alijualo ili kumfanya femi aonekane wa tofauti kuliko wote na kweli aliweza maana femi aliwaka ukimuangalia tu mwenyewe unapagawa ukijulisha na uzuri na zile dimpozi alizorithi kutoka kwa mama yake basi weeeh .

Siku hiyo nyumba nzima walimsifia yaani, hakupoteza muda baada ya yote akachukua gari special kabisa ambayo bibi yake mara nyingi uwa anatoka nalo akiwa na safari maalumu au muhimu sana lakini yeye alichukua kwaajili ya kwenda kutimiza jambo lake ila wakaka mna hekaheka mjue, alifika chuoni kwanza gari tu lilisababisha watu wote wampe attention kubwa sana alishuka kwa mbwebwe zote siku hiyo yaani nyie mimi pia nilikuwepo kati ya wale washangaaji muda huo femi alishajua Mere alipo ni kama aliweka watu wa kumuwinda mere hivi, mkononi alikuwa amebeba ua sio ua la kawaida yaani ni pesa zilizotengenezwa kuwa muundo wa maua zilikuwa takribani milioni moja na kadi fulani hivi, kila mwanamke aliyekuwa pale alitamani yeye apewe, na waliokuwa wakijua mahusiano ya femi na swaumu, walimpigia simu swaumu na kumwambia kuwa anafanyiwa surprise hivyo swaumu akatoka library mbio mpaka kwenye eneo alilokuwepo femi, swaumu wa watu mwaya alisimama mbele ya femi cha ajabu bhana femi alimpita swaumu kama amuoni 🥹 nyieee hivi mnajua maumivu ya hii kitu, swaumu aliganda akiwa ameweka mikono yake mbele maana alipanga kumkumbatia lakini ndo hivyo.

Safari ya femi iliishia kwenye kimbweta ambacho alikuwa amekaa Mere na rafiki zake ambao wote kwa pamoja walikuwa wakijiuliza hii ni kwaajili ya nani , femi pasi na kufanya ajizi alipiga magoti mbele ya Mere, kwanza Mere alishtuka sana na kusema


"What is this ? Am I dreaming??"

Yaani Mere hakuwa akiamini kwamba kile kitu kilikuwa ni kwaajili yake, muda wote femi alikuwa na tabasamu pana sana usoni mwake, tabasamu ilo lilipambwa na dimpozi nzuri mno, wanafunzi wote walikuwa wakishangilia na kupiga kelele kwa lile tukio

"Mere will you be my life partner??"

Fami hakutaka kupoteza muda chap akauliza uku akinyoosha ua lile la pesa nyingi kwa mbele akisubili Mere apokee lakini aka.........

ITAENDELEA
 
FEMI (play boy)

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 06

MAWASILIANO: 0783642467

SONGA NAYO.....

Waliendelea kucheka pale na kupiga story za hapa na pale chakula kikaandaliwa na wakala kwa pamoja

"Nawaza brandina umetokea familia gani mbona mdomo juu juu kama chuchunge kila kitu unajua wewe ??"

Aliuliza mmoja kati ya marafiki wa brandina

"Unafikili alikuwa anaongea basi mbwa huyu ? Alikuwa kimya sana pumbavu zake ila sasa hivi anaongea kama Kameza flash tena anaongea bila kukata maneno ni ana nyoosha kama fundi ujenzi "

Alidakia femi

"Sema brandina we chombo unanikela hayo magagulo yako unayoyavaa"

"Hapa mmeniita tupige story au mmekuja kunichambua ebu niambieni maana brandina hivi brandina vile nyie mbwa nyie mkichoka kila mtu kwao "

"Eeeh huyu nyie uoni aibu kutufukuza"

Kwa pamoja wakaanza kumzomea lakini frank tu ndio alionekana kuwa bize sana na simu take aiseeh alikuwa bize kuliko kawaida lakini wenzie hawakuwa wamejua kwani walikuwa bize na brandina ambaye alikuwa na maneno mengi na alikuwa akiwapa story za uongo na kweli mpaka wanasahau maumivu ya viboko walivyochapwa na swaumu...

Majila ya saa mbili usiku bibi yake femi alirudi kama kawaida akitoka na kurudi lazima arudi akiwa amebeba zawadi kwaajili ya femi ata kama itakuwa inajirudia lakini lazima alete

"Aaah jamani leo naona wote mliochapwa viboko mko hapa "

Femi alistuka na kujiuliza bibi kajuaje kama tumechaowa viboko

"Bibi umejuaje ??"

Femi alishindwa kuvumilia na kujikuta akiuliza

"Nimejuaje na mnatrendy uko online kila mtu anawaangalia dunia kiganjani taarifa zimenifikia mapema, kwanza imekuwaje yule binti ana tatizo la akili au ?

Aliuliza bibi huyo femi akawageukia rafiki zake mwisho akajibu

"Hapana alikuwa na hasira na mimi nilimkosea "

"Ndio akutandike kiasi hiki ?"

Muda huo bibi femi alimsogelea mjukuu wake na kuangalia alama alizokuwa nazo mwilini na ukizingatia femi alikuwaweupe sana basi weeeeh alama zilionekana vizuri sana "

"Kumkosea tu ndio akuumize hivi ? Kesho nakuja chuoni kwenu "

"Bibi...."

Femi alitaka kuongea kitu kwa bibi yake lakini bibi hakutaka kusikiliza zaidi alipanda ngazi na kwenda chumbani kwake

"Kwani si mnipe hizo simu zenu za kupangusa ili na mimi nione mlivyokuwa mnafundishwa adabu "

"Brandina toka hapa "

Alifoka femi muda huo aliweka matani pembeni maana aliwaza bibi yake akienda chuoni itakuwaje ? Ingawaje anajua bibi yake muda wote anakuwa upande wake lakini uendaji unaweza ukaleta mambo makubwa zaidi....

Baada ya muda kwenda marafiki zake waliaga na kuondoka femi alibaki akiwa na mawazo sana siku hiyo mawazo yalikuwa kwaajili ya bibi yake, lakini pia alimuwazia swaumu kilichomchanganya zaidi ni mere kutokupokea simu zake wala kujibu jumbe zake...

Siku iliyofuata Femi aliwai kwenda chuoni yote kwaajili ya kuonana na mere msichana pekee ambaye amavuruga na kuharibu akili ya kijana femi.

"Mere, mere......"

Aliita femi baada ya kumuona mere ambaye moja kwa moja alionekana kumchunia femi hakutaka ata kuongea nae, yaani ilikuwa kati kati ya wanafunzi wengi femi alitilia huruma sana

"Nisikilize basi mama utaniua mwenzio nisaidie kipenzi zungumza na mimi niambie nimekukwaza na nini ??"

Alilalamika femi lakini mere hakusikia zaidi alienda library ambapo femi hakuweza kuingia kwani hakuwa na kitambulisho cha chuo alikisahau nyumbani

"Mshikaji sasa hivi unatutia aibu ujue...."

Alizungumza mmoja kati ya marafiki wa femi huyu alijulikana kama Kevo

"Kweli kabisa angalia yaani we wa kupiga goti na kumlilia mwanamke michozi kama hivyo eti .? Unazingua bhana hatujakuzoea hivyo "

Alidakia rafiki yake mwingine lakini femi hakuacha kulia alilia tena kwa sauti ya juu kabisa, alipiga simu ya mere lakini ilionesha wazi kuwa mere alikuwa amemblock femi femi aliteseka sana

Ila nyie mere kama ananifurahisha hivi anatunyooshea play boy

"Nyie amjui tu me sijuagi kama mapenzi yanauma hivi lakini mjue tu kuwa mere ananitesa...."

Alilalamika femi frank akamsogelea rafiki yake na kuanza kumtulia, wanasemaga anayekupa bega la kulilia ujue huyo ni rafiki ambaye anaupendo wa dhati na wewe basi tuseme frank ndiye rafiki wa kweli wa femi na anajua mengi kuhusu femi

"Tulia basi japo mere sijamzoea nitazungumza nae ili nijue shida nini "

"Unafikili kutakuwa na nini ?? Mere anaonekana ni mwanamke ambaye anajitambua sana nafikili atakuwa amepata story zangu za kutoka na kila mwanamke ingawaje sio wote wanajua ila kina Imani kuna watu wamenichafua kwa mere "

Aliendelea kulalamika femi

"Tulia basi braza....."

Hatimaye siku iliisha juu juu femi akiwa ni kama mtu ambaye ajitambui kabisa alirudi nyumbani na kujifungia chumbani kwake hakuulizia chakula wala chochote kile....

"Kaka femi "

Ilisikika sauti ya brandina kiwa mlangoni kwa femi akimuitilia femi ambaye hakuitika wala kufungua

"Mbona hivyo jamaninumepatwa na Nini ??
Aliuliza brandina lakini hakupata majibu

"Sawa usiitike lakini kuna msichana yuko getini anaitwa Mere kasema "

Weeeh hapo femi baada ya kusikia jina la mere hakufikilia kufuta machozi wala kufanya chochote kile akakurupuka na kutoka nje chap alivyotoka tu brandina akaingia chumbani....

Femi alikimbia mpaka getini lakini akakuta patupu akarudi akiwa na hasira sana

"Brandina unafikili me bibi yako au babu yako si ndio ?? Unafikili mi ni mtu wa kijijini kwenu si ndio ?? "

"Tulia basi mzee baba kwahiyo ukaenda hadi getini, mtu ulikuwa utaki kufungua mlango me nifanyeje jamani eeh ?? Umejifungia mda wote huo uje kujiua uku "

"Kwanza umenikumbusha bora nijiue tu "

ila femi jamani kwahiyo alikuwa ajui kama kuna kujiua ?? Akachukua shuka lake na kulifunga kwenye feni iliyoko chumbani kwake, muda huo brandina aliganda akimuangalia tu, femi akavuta kiti chake vizuri akasimama juu yake

"Nikusaidie kusukuma kiti au ??"

Aliuliza brandina swali ambalo lilimshtua sana femi haraka akashuka kwenye kile kiti kumbe ugali anaupenda akawaza hapa brandina akiwai akasukuma basi nimekwenda na maji

"Brandina una uhakika we ni mwanamke kweli ?? Maana huna ata huruma "

"Wacha weeh me sina huruma na mere je ?? Anayekufanya unalia siku nzima ?? Dume Zima....."

Hapo femi aliishiwa na nguvu akakaa chini na kushusha pumzi ndefu sana ya uchovu.....

ITAENDELEA
 
FEMI (play boy)

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 07

MAWASILIANO: 0783642467

SONGA NAYO......

Baada ya femi kukaa chini brandina akasogea na kukaa karibu yake na kumshika bega

"Femi sizani kama kukaa ndani na kulia kujiumiza inaweza kuwa njia ya wewe kutatua matatizo yako wewe na mere, ndio kwanza leo una siku ya tatu tangu muanze mahusiano lakini anakuendesha kiasi iko niseme tu kuwa sijakuzoea hivyo, simaanishi kwamba uendelee na maisha yako ya uhuni hapana ila naitaji usimame kama mwanaume simama kama femi mfuate mere ukiwa hauna hasira ukiwa autelemshi machozi na kuongea nae kiundani, najua unajiuliza nimejuaje kuhusu mere lakini nilimuuliza Kevo leo kwanini upo hivyo ndo akaniambia"

Brandina baada ya kumaliza kuzungumza akainuka na kutaka kuondoka lakini femi alishika mkono na kumrudisha nyuma

"Brandina kwani we sio binadamu ??"

" maswali gani hayo nawe kama me sio binadamu ningekuwa nani ?? "

"Nawaza yaani sijui nikutafasili vipi lakini we ni mtu powa sana Mungu akutunze kipenzi kwaajili yangu, nyumba nzima wewe ndio unanielewa hata bibi yangu anielewi kama ambavyo wewe unanielewa "

"Kawaida nimefundishwa upendo na na kujali kwenye familia yangu nisubili nikuletee chakula "

Kwa namna moja au nyingine femi alijisikia afueni akapata na nguvu akaingia bafuni na kuoga baada ya muda akatoka na kumkuta brandina akiwa amesimama pembeni

"Aaah ungeweka hapo kisha ukaenda unajichosha muda mwingine "

"We nawe, sijaja kuleta tu nimekuja kukulisha pia "

"Una wazimu wewe "

"Nina wazimu gani njo nikulishe mtoto mzuri...."

"We kichaa nini mtoto mzuri nani ??"

"Jamani mtoto mzuri kaacha kulia na kaenda kuoga sasa ni muda wa kula dada yake niko hapa kumlisha "

"Hahah maliza kuota halafu weka chakula changu chini na utoke nje....."

Alizungumza femi wote wakacheka na brandina alionekana kuzamilia kumlisha femi ebu kwanza tumjadili brandina naye ana nini ?? eeeh maana sio kwa kumuhudumia femi namna hii sio powa kabisa na leo amekuja na style ya kutaka kumlisha ebu tuone...

Femi alikaa kitandani na brandina akamfata na kuanza kulisha femi akakubali na kuachama mdomo ili kupokea kijiko cha chakula

"Jinga wewe yaani una asama kabisa me nikulishe Thubutu nina kazi zangu kibao "

Alizungumza brandina na kurudisha kijiko kile kwenye sahani kisha akamkabizi femi chakula

"Hakikisha kinaisha "

Kisha brandina akaondoka femi alibaki akimshangaa tu na kujicheka mwenyewe

"Kwahiyo na mimi nilikuwa nataka kulishwa au ??"



Majila ya usiku kabisa femi alipokea simu kutoka kwa frank

"Unaendeleaje mshikaji wangu ??"

"Safi tu "

"Mere alikucheki au ??"

"Hajanicheki na ameniblock sema nini broh nahisi Mere nilikurupuka sio sehemu yangu ya maisha siku tatu tu amenifanya nadhalilika na kusahau mimi ni nani ?? Nitaendelea kupiga mpaka nitakapopata niliyepangiwa na Mungu kuhusu mere basi tena "

"Aaah broh mbona umekata tamaa mapema me naona kabisa unampenda mere tena sana "

"Nampenda sawa lakini nitafosi moyo kukaa sawa Mere mtoto wajini yule nilikurupuka tu "

Alizungumza femi na hakutaka maneno mengi sana akakata simu na mwisho alizima kabisa baada ya kuona kama frank anamsumbua hivi

Eti nyie kwahiyo somo la brandina limemuingia femi ?? hivi kweli hatolia au ndo anajikosha tu mbwa huyu

Siku iliyofuata kama kawaida femi alitumia mavazi yake kisha akaenda chuoni alipofika alikuwa bize sana picha linaanza alimpita mere kama amjui yaani kwanza rafiki zake wote wakashangaa hawakuamini kile kitu wanachokiona waliona kama ni ndoto hivi

"Weeeh kwa mere ujamuona ??"

"Nimemuona kafanyaje ??"

"Aaah kafanyaje tena leo anaonekana yuko kwenye mood nzuri kaongeee nae "

"Ebu twendeni bhana "

Alijibu femi kwanza hata me mwandishi wenu nilibaki mdomo wazi amewezaje kumove on gafla hivi au hakuwa akimpenda tuangalie ule kweli alikuwa akimpenda kweli....

Upande wa mere alibaki akijiuliza tu imekuwaje leo femi amempita kama amjui, haraka akamtoa kwenye block na kumpigia, femi alipoona namba ya mere alifurahi sana ingawa akucheka kwa sauti lakini alitabasamu tabasamu pana sana lililofanya dimpoz zake zichukue nafasi kubwa....

"Hallo..."

Alizungumza femi baada tu ya kupokea simu

"Eeeh baby tunaweza kuonana mara moja ??"

Aliuliza mere

"Baby ?? Sorry naongea na nani ??"

Femi aliamua kuigiza kuwa namba ya mere ameifuta kwenye simu yake wakati kabla hawajapatana Namba ya mere tayali ilikuaa kichwani yaani anakutajia ata akiwa usingizini

"Femi najua jana nimekukwaza lakini hii aimaanishi kuwa sikupendi nakupenda sana mpenzi wangu ujui tu nimekuwa mpweke kiasi gani kwaajili yako "

Mere aliongea kwa sautinya mahaba sana yaana sauti fulani hivi ambayo ilimfanya femi apata kigugumizi na kushindwa kuzungumza meneno na kueleweka na ukizingatia alikuwa na rafiki zake ndo kabisa....

"Oya washikaji nakuja kuna kitu nimesahau kwenye gari..."

Femi aliwaga rafiki zake kijanja na kuondoka

"Tuonane kwenye gari....."

Femi na mchumba wake yaani Mere walionana ndani ya gari lakini hawakuishia hapo wakawasha gari na kutoka mbali kabisa na eneo la chuo na kila mtu akaamua kuzima simu ili kuepusha usumbufu.....

ITAENDELEA
 
FEMI (play boy)

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 08

MAWASILIANO: 0783642467

SONGA NAYO......

Mere na femi siku hiyo walitumia muda wao pamoja vizuri sana ambapo kwa muonekano tu ilionesha wazi ni kiasi gani hao watu wanapendana sana femi akiwa bize na mere wake pembeni mwa fukwe za bahari simu yake ya mkononi iliita na ilikuwa ni namba ngeni aliiangalia kwa muda kisha akapokea

"Femi, hivi ndo kweli umemchagua mere kuwa kila kitu kwako ?? Hivi unamjua vizuri huyo msichana yaani ndio kwanza ni mgeni chuoni ndio kwanza ni mwaka wake wa kwanza hapa chuoni lakini umempokea kwa moyo wote mambo unayomfanyia mere ukuwai kunifanyia mimi au mwanamke wako yoyote yule unayemjua achana na wanawake wengine kwanza ata swaumu mwanamke ambaye uliwai kusema ni wandoto zako mwanamke ambaye aliacha nazi akaangua koroma unajua swaumu anapitia wakati gani baada ya kuachwa gafla na wewe ?? 🥹 achana na swaumu vipi kuhusu mimi, femi nimekuvumilia kila kitu najua wanawake wako wote lakini nimenyamaza tu nilikubali uwe na mahusiano na rafiki yangu swaumu nikiamini unampenda femi umeshafikilia kua swaumu akijua mimi na wewe ni wapenzi atanionaje ?? Unafikili ataelewa kuwa mimi ndio kwanza chuk kizima natamani uzungumze kitu lakini najua unaogopa kwakuwa uko na mere basi fanya hivi ukiwa peke yako nipigie nimekumisi mno "

Alimaliza msichana wa watu na kukata simu akiwa na kilio cha kwikwi...

"Ouk saaa usijali hizo document nitatuma nikifika nyumbani maana nimesave kwenye laptop kwenye simu sina "

Yaani simu imekatwa lakini femi anajifanya kuwa bado a aendelea kuongea na simu

"Baby, siku yangu ya leo imekuwa nzuri sana kuliko kawaida "

Alizungumz mere

"Mimi niseme kuwa tangu nimekuwa na wewe ndio najiona kama binadamu vile "

"Ahaha yaani wewe, si ulininunia lakini ??"

"Achana na hizo mads basi kipenzi si tumemaliza kila kitu ??"

"Yaah ni kweli..."

Waliongea mengi na baada ya muda kwenda na giza kuanz kuchukua nafasi yake Mere aliondoka ingawaje femi alisisitiza kumpeleka nyumbani lakini mere aligoma na badala yake akaita bolt kwenye pochi yake akiwa amejaa baada ya kupewa pesa na femi ila femi pesa za familia anajua kuzitumia jamani....

Femi alifika nyumbani akiwa na furaha sana alifika sebuleni na kaanza kupiga kelele kwa kuitilia jina la brandina ambaye kwa muda huo alikuwa jikoni haraka akatoka

"Nini tena jamani "

Femi akamuwai brandina akamshika mkono yake yote miwili na kuanza kumzungusha akifutahi sana muda huo bibi femi alikuwa amesimama juu akiwaangalia tu jinsi ambavyo walikuwa wakizunguka pale sebuleni

"Femi utaniangusha bhana kizunguzungu niachie...."

Alifoka brandina lakini haikusaidia kitu ndio kwanza femi aliongeza speed yaani furaha ilipita maelezo

"Uwezi amini mtoto ananipenda yule kumbe jana alikuwa na hasira na mimi tu ila ananipenda hatari "

Alizungumza femi kwa furaha sana

"Mmmmh love love love "
Ilisikika sauti ya bibi femi iliyomshtua sana brandina

"Oooh bibi kumbe umesharudi ??"

Hapana ndo naenda kijana wangu unataka unipeleke au ??

Bibi kiazi mjukuu kiazi wamekutana

"Mbona uko na furaha sana mjukuu wangu kuna nini ?? "

"Bibi we subili kwanza naweka mambo vizuri zaidi halafu nakuambia kila kitu tulia bibi tulia "

"Mmmmh unanipa amsha amsha ya kujua nini kinaendelea ujue..."

Muda huo huo simu ya femi iliita alipoangalia kuwa ni namba ya mere alikimbilia chumbani bibi yake alibaki akimshangaa tu

"Mere unalia nini nambie basi shida iko wapi ??"

"Femi we acha tu napitia makubwa mimi, mtu wa pekee ambaye naweza nikaongea nae na anaweza akanipa moyo basi ni wewe pekee umebakia "

"Mere niko kwaajili yako nambie shida nini mpenzi nambie jamani unaniweka roho juu "

Mere aliongeza sauti ya kilio mwisho akakata simu hiyo ilimchanganya zaidi femi ambaye haraka akapiga simu na ikapokelewa na muda huo zilisikika sauti mbali mbali za watoto wakilia, mere akilia lakini na sauti ya kiume ikifoka.....

"Natamani ningepajua nyumbani kwao ningeenda sasa hivi "

Alizungumza femi komoyomoyo huku akiwa anatetemeka kwani alikuwa na wasiwasi sana juu ya mere....

"Baba tuhurumie usiku huu nitaenda wapi na familia yangu nitaenda wapi na watoto hawa mimi nakutafutia pesa yako nakupa nakuomba "

Alisikika mere akiomba uku akilia sana hapo femi aliweza kuelewa kuwa ni baba mwenye nyumba alikuwa akimfukuza mere na ndugu zake akiitaji nyumba yake baada ya kushindwa kulipa kodi

"Mere nisikilize, nisikilize kipenzi unadaiwa kodi ya miezi mingapi ?? Na unalipaga kwa mwezi bei gani ??"

Aliuliza femi kwa sauti ya juu sana ingawa alikuwa hana uhakika kuwa anasikika au laaah lakini alisikika mere akijibu

"Usijali mpenzi wangu ili jitasimamia mwenyewe "

"Acha ujinga mere nisipokusaidia wewe nimsaidie nani ??" .

Subili kidogo mpenzi nakupigia "

Alizungumza mere kisha akakaa simu..

ITAENDELEA
 
FEMI (play boy)

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 09

Mawasiliano: 0784642467

SONGA NAYO......

Femi alikaa kwa wasiwasi muda wote anaangalia simu yake kama inaita au kuna ujumbe wowote umeingia kutoka kwa mere lakini hakukuwa na mafanikio yoyote moyo wake ulikuwa juu juu kuna muda akawa anajicheka mwenyewe

"Eeeh ata maharage ayaangaliwi kwa umakini huu sio bure mere kaniloga "

Alizungumza na kujicheka juu, uvumilivu ulimshinda akachukua simu yake na kutaka kumpigia mere lakini muda huo huo ujumbe ukaingia kwenye simu yake kutoka kwa mere

"Naona hadi aibu mpenzi wangu, mama yangu anaumwa sana baba alishatukimbia nazani nilishawai kukuambia familia iko mikononi mwangu nimepanga nyumba nzima ambapo nalipa kodi 150k sasa imeisha tangu miezi miwili iliyopita baba mwenye nyumba amekuja kutufukuza femi uwezi amini vitu vyangu viko nje sijui ata mama yangu na wadogo zangu nawapeleka wapi mimi "

Weeh ujumbe huo ulimchanganya zaidi femi wa watu lakini kwakuwa pesa kwake ni kitu kidogo alichofanya ni kumuuliza pesa anapokea kwa namba gani Mere hakupoteza muda akataja namba chap na femi akafanya mambo alimtumia pesa ya kodi takribani miezi 8 hivi ebu piga mahesabu msomaji wangu ni sawa na bei gani ?? Baada ya kutuma pesa femi akapiga simu tena

"Kama kunatokea shida naomba uniambie kipenzi nijuze kila kitu sawa mummy ??"

"Asante penzi yaani daaah wewe ni kila kitu kwangu kwanini Mungu hakukuleta kwangu mapema jamani nimeangaika na wanaume nimeteseka kumbe Mungu aliniandalia wewe nitakupenda mpaka kifo mume wangu mtatajiwa "

Basi femi baada ya kukata simu ya Mere alipokea simu nyingine kutoka kwa rafiki yake frank

"Nambie mwanangu vipi ??"

"Safi broh nakupigia muda wote simu yako inatumika tu mzee baba umekuwa customer care au ??"

"Ahahahaha acha Zako nilikuwa naongea na mere "

"Weeeh mmeshapatana au ??"

"Mapema si unajua kwa mtoto nimenasa halafu kwangu kanasa "

"Powa bhana, nilikuwa na shida mshikaji wangu ndani sina ata mia nasubili boom langu alijatoka, njaa baba njaa nimevumilia nimeshindwa we ndo uliyebakia "

"Subili kidogo "

Alizungumza femi kisha akakata simu na muda huo huo akamtumia elfu 50 yaani ukiachana na femi kuwachanganya wanawake lakini ako na huruma sana ka anacho anakupa na bila kukudai muda mwingi amekuwa akiwajali rafiki zake na katika kundi Zima yeye ndiye mwenye uwezo....

Ikiwa ni siku ya jumamosi ni siku ya mapumziko ya bibi yake femi lakini pia ni simu ya mapumziko ya femi kwani hakuwa akienda chuoni bibi yake alimuomba amsindikize akamgembelee shoga yake, kwakuwa femi alikuwa akipenda kuwa karibu na bibi yake hakugoma zaidia alijiandaa na safari ikaanza....

Walifika eneo husika ilikuwa nyumba fulani hivi ya kawaida Sana iliyozungushiwa fens ya michongoma

"Aaah leo shoga yangu atoamini kuniona unajua hatujaonana ndani ya miaka miwili kila mtu yuko bize na mambo yake "

"Bibi naee umeanza sasa uanze kulia umo ndani nakuacha naondoka "

"Kwahiyo unaniona mimi ni mtu wa kulia tu si ndio ??"

Mtoto shika adabu yako sawa ?? Niheshimu unifikii hata kwa sekunde weupe tu kama utovu wa papai "

Bibi anaongea huyu kaambiwa kidogo tayali kapaniki

"Eeeh basi shuka twende "

Walishusha zawadi walizokuwa wamebeba kwaajili ya rafiki huyo...

"Karibuni sana "

Ilisikika sauti ya binti fulani hivi ilikuwa sauti nyororo na nzuri sana kwanza kwa shauku femi akaacha kushusha zawadi na kugeuka ili kumtazama msichana huyo alishtuka na kusema

"Nasma..... "

Ajabu femi anamfahamu msichanaz ata msichana huyo alipomuona femi alifurahi na alimkimbilia na kumkumbatia alitaka na kumkisi kabisa lakini femi alimkatalia kwani bibi wa msichana huyo alisimama mlangoni na kuwaangalia kwa makini sana alionekana ni bibi ambaye apendi mambo ya kijinga

"Karibuni sana sana jamani daaah kweli binadamu wanakutana unajua nilipoona page yako insta sikuamini kama ni wewe hauzeeki mzee mwenzangu "

" bi nasma bhana "

"Subili kwanza huyu ndo femi ?? "

"Ndio"

"Mamaaaah we femi mbona unakuwa haraka kama mtoto wa kike ?? Mara ya mwisho kumuona alikuwaga na mama yake na kipindi iko walikuwa wanamuita bwabwabwabwa ade ade "

Alizungumza bi nasma

"Mzee mwenzangu una kumbukumbu mwenyewe enzi hizo alikuwa anawaza ubwabwa na maharage tu sasa hivi anawaza wana......"

Bhana bibi si ndo akataka kulopoka kuwa anapenda wanawake lakini aliishia kati

"Naombeni maji ya kunywa kwanza....."

Bibi aliamua kuzuga kwa kuomba maji ya kunywa

Basi wazee wale wakiwa bize na maongezi wajukuu wakatoka nje

"Hatimaye Mungu kakuleta kwetu kabisa, hivi femi nini uoni kuwa mimi na wewe ni Mungu amepanga kuwa pamoja ?? Eeh kwanza tulikutana Beach bado Mungu akatukutanisha chuo kimoja darasa moja course moja, haya leo hii tunagundua kuwa bibi zetu ni marafiki wa muda mrefu "

"Nasma ebu acha mambo yako uko sawa, kwanza imetoka gafla tu wamejua kuwa tunajuana wala sikutaka wajue, na nahisi bibi hajakukumbuka kwaajili ya uzee kipindi kile si alikuona nyumbani ??
"

"Acha ujinga ujue "

"Ujinga wa nini me nampenda Mere kuliko chochote yaani kama hajaniloga naomba akaniloge nibaki kuwa wake tu "

"Eeeh makubwa femi sio wewe uliwai abia kuwa kwenye moyo wako yupo swaumu tu ?? Au sio wewe leo hii shoga yangu swaumu anaangaika uko anateseka analia vipi akija kujua kuwa Nina mahusiano na wewe lakini pia haunipendi femi kama umeniloga mwambie mganga wako aniague bimechoka kutesema 🥹"

Kaaah femi jamani kazidi sasa daah halafu wanawake wote wanampenda hii bahati angepata kaka angu mmoja hivi nyumbani tungekoma .

Nasma wa watu akaanza kulia na femi alikuwa akijua udhaifu wa Nasma alichofanya ni kumkumbatia na kumkisi (deep ) Nasma wa watu akatulia kabisa kaona kafika kwa femi, aliishiwa na nguvu kabisa lakini muda huo huo walisikia jina la nasma likiitwa haraka wakaachiana....

"Abee bibi "

"Unafanya nini uko nje nawe bibi umempa maji tu chakula je ??"

"Aaah nisamehe bibi huyu femi anapenda sana sungura hivyo nilikuwa namuonesha "

hapo bibi femi alicheka na kumuangalia msichana yule na kujisemeq kimoyomoyo

"Huyo femi anayeogopa hadi mende leo hii akacheze na sungura ?? Huyo kuku mwenyewe amkute keshapikwa akiwa mzima kukamata tu mtihani ujana kazi "

Ila huyu bibi jamani, waliandaliwa chakula pale na walikaa mpaka jioni kisha Wakarudi nyumbani

"Ujui nina furaha kiasi gani kumbato lako tu limenichanganya kesho nakuja kulala hapo chuo tutaenda wote "

Nyie 🥹 sa mbona wanawake tunajirahisisha hivi huyu jamani femi aliangalia ujumbe ule kutoka kwa Nasma hakujibu kitu zaidi aliangalia na kusikitika aliingia ndani akaoga na kukaa chumbani akichati na mere wake....

"Mmmmh mkaka weeh unachatika na kucheka mwenyewe utakuwa chizi "

Kama kawaida brandina achezagi mbali nyie yaani huyu msichana daaah

"Umeanza kwanza unakuja kama kamzimu vile "

Bhana brandina ana akili fulani hivi za kitoto alimtukia femi pale kitandani na kuanza kumpiga

"Nani kimzimu nani "

Brandina aliendeleza utoto wake mwisho walitulia na kuangaliana tu kila mtu mapigo ya mbio yalikuwa yanaenda moyo brandina na utoto wake leo ataeleza, kila mtu akafumba macho na kuanza kumsogelea mwenzie usoni zaidi waka......

NITARUDI....
 
FEMI (play boy)

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 10

Mawasiliano: 0783642467

SONGA NAYO........

Basi mwaya brandina na femi waliendelea kusogeleana na walianza kukisi lakini kabla hawajafika mbali ilisikika sauti ikiita

"Brandina, brandina....."

Haraka brandina akajito mikononi mwa femi na kutoka nje kwa aibu sana

"Yaani wewe usiku huu kwa femi ?? Subili siku akunyooshe uko ndani ndo utakumbuka umu ndani umeletwa kufanya nini ? Wenzio wote tumekaa muda mrefu na umetukuta lakini hatuna hata hayo mazoea na huyo femi wewe sasa dada kihede mswede nakuambia siku yako moja tu femi mwenyewe unamjua "

Brandina aliona kama mfanyakazi mwenzie anamchanganya tu akiangalia na hali aliyotoka nayo chumbani kwa femi ndio kabisa akampita na kutaka kuondoka

"Shika simu Tako ilikuwa inaita mama yako amepiga muda mrefu mno "

Brandina alichuku simu yake na kuondoka

Upande wa femi aliinuka pale kitandani na kwenda kwenye kioo

"Aaah femi jamani ndo nini kwani si tumekubaliana wewe ni wa Mere tu ?? Kwanini unapata hisia na brandina ?? Eeeh "

Femi alibaki akijiongelesha mwenyewe kama kichaa Pale kwenye kioo.....

Siku iliyofuata ilikuwa junapili na wote walishinda nyumbani ata femi hakutoka alitaka kwenda kwa kina mere lakini mere alimpa sababu ambayo femi aliielewa na alitulia tu nyumbani akicheza game, siku hiyo ilikuwa ngumu sana kwa femi lakini pia kwa brandina kwani kila mtu alikua akimuonea mwenzie aibu kutoka na kitendo cha usiku, cha wao kukisiana ukizingatia femi na brandina wamejenga ukaribu mzuri sana wa kirafiki ingawaje kuwa wafanyakazi wengine lakini femi alikuwa akimkubali sana brandina ambaye ana miezi 8 tu tangu aanze kufanya kazi kwa kina femi

"Kaka femi chakula....."

"Asante weka hapo "

Alijibu femi uku akiwa bize na game lake

"Kitapoa ufanye ule %

Alirudia msichana huyo ambapo femi aliinua uso wake na kumtazama kwa makini

"Kwanza brandina yuko wapi ?? Mbona chakula umeleta wewe ??"

"Yupo jikoni, kwani kuna ubaya mimi kuleta chakula ?:

"Mwambie brandina aje mara moja "

Alizungumza femi lakini msichana huyo aliganda akimuangalia femi ambaye alikuwa bize tena na game kwa muda huo baada ya dakika Kazaa femi aligeuka na kuangalia alishangaa kumuona msichana huyo akiwa amesimama

"Jamani ujaenda tu ?? "

"Subili nikuulize kitu femi ukiachana na wanawake wote unaowaleta hapa Kati ya mere na brandina nani unampenda zaidi ??"

"Usimfananishe mere na brandina sawa ?? Mere ni mke wangu mtarajiwa halafu brandina ni mfanya kazi wangu mtiifu anajua nini nataka nini sitaki iki napenda iki sipendi, kwanza nikuulize una miaka mingapi tangu uje hapa ??"

"Miwili na nusu lakini haijalishi "

"Haijalishi nini sasa, elewa.ni sijawai kukuelewa halafu mbona kama uko na wivu na brandina sasa kama ni wivu wacha nikuongezee kitu brandina ni msichana unique sana halafu anajua kumsoma mtu kwa muda na ana huruma, kwanza kwanini nakueleza yote haya ebu baba chakula chako kwanza kishapoa halafu jiitie brandina "

"Brandina akijisikii vizuri...."

"Anaumwa au ??"

"Sijui "

Alijubu msichana huyo na kuondoka femi alijikaza mwisho wa siku alitoka chumbani kwake mbio mbio akimuwai brandina bahati nzuri alimkuta akikatiza sebuleni kuelekea chumbani kwake

"Brandina "

Aliita femi lakini femi kwa kuwa utoto ni mwingi alipomuona femi na kukumbuka tukio la usiku akiwa na wenge lake akataka kukimbia ile anageuka mbele tu bibi femi huyu na kwakuwa alikuwa amegeuka na kasi kubwa alimsukuma bi femi akaenda chini na sio tu bi femi na brandina pia akaanguka kwa kumuangukia bi femi kwa juu .

Haraka brandina wa watu akainuka na kutaka kumuinua bi femi

"Niache mie una haraka ya wapi binti ?? Eeeh unawaiwapi haya unataka unitoe meno ya barazani nitakuwa na muonekano gani mimi "

"Nisamehe bi femi "

Bi femi alichukia sana alichukua simu na kumpigia simu mama femi

"Huyu mfanyakazi wako nimemchoka nataka h
aondoke "

"Mama jamani ata salamu kweli "

"Salamu kitu gani huyu mfanyakazi wako mshamba alitaka kunitoa meno yote saa hizi "

"Mama nawe mbona unafoka tu amefanya nini...??"

Kabla bi femi ajajibu femi akampokonya simu bibi yake

"Mama achana na huyu mbibi asikusumbue, ujui tu mama brandina ndio mfanyakazi bora hila bibi ni ampendi tu"

Alizungumza femi kisha akakata simu, femi akamshika mkono brandina mpaka kwenye kochi

"Umeumia ??"

Aliuliza femi uku akimkagua brandina yaani mpaka bibi alishangaa yeye ndio alianguka chini hajaulizwa chochote lakini brandina ameulizwa Na anakaguliwa

"Femi niko sawa ni nini jamani "

Alifoka brandina kisha akamfata bibi

"Nisamehe sana bibi ni bahati mbaya kwani umeumia ??"

"Ata nikiumia utanisaidia nini ?? Nitokee hapa mie"

Brandina aliondoka na kwenda chumbani kwake, femi pia alikuwa amerudi chumbani kwake, majila ya saa mbili usiku femi alipokea ugeni hakuwa mwingine Bali ni Nasma ila wanawake bhana

"Mbona ukunipigia kama unakuja....??"

Aliuliza femi, kwa kuogopa sana

"Nani kwanza amekufungulia mlango mkubwa? "

"Huyu msichana wenu mpya anaonekana mkalimu sana, alitaka kukuita kwanza lakini nikamwambia kuwa Mimi ni mwenyeji najua kila kona so akaniacha "

"Unamzungumzia brandina au ?"

"Sijui kama ilo ndo jina lake lakini sikuwai kumkuta hapa kabla....."

Femi alitoka chumbani kwake mbio mpaka sebuleni ambako alimkuta brandina akiwa bize anaangalia zake movie ambayo ilikuwa ya comedy hivyo alikuwa akicheka sana

"Brandina??"

"Eeeh we nawe mtu asikae kwa amani kaa kimya kwanza movie yangu itanipita "

Yaani brandina hapana kabisa huyu msichana ananifurahisha mno

"Unakichaa nini ?? Sikia brandina huyu sio mwanamke wangu ni rafiki yangu kwanza sijui amefata nini usinichukulie vibaya sawa ??"

Alizungimza femi kwa wasiwasi sana mpaka brandina akastopisha movie yake na kumgeukia

"Femi uko sawa kweli ?? Sa mbona kama uko na wasiwasi ?? Eeeh halafu haya maelezo anatakiwa kupata mere siku akikufuma sawa sio kwaajili yangu me nishazoea na sina cha kukufanya mshikaji wangu "

"Oooh ila kweli, sasa kwanini nilikuwa nakuelezea wewe ?? Anyway play tuangalie pamoja "

Basi femi akasahau kabisa kama ameacha mgeni kule chumbani akakaa na kuanza kuangalia movie ambayo ilikuwa na comedy nyingi mno hivyo walikuwa wanakicheka tu.

"Baby......"

Vile movie imekolea watu wako bize nasma akatoka ndani kwa hasira sana mpaka sebuleni ambapo alimkuta femi akiwa bize na movie.....

"Yaani mimi nimekaa nakusubili sijala ujanikaribisha ata kinywaji, umekaa hapa na huyu chokolaa si ndio ??

Nasma alionekana kuwa binti mwenye dharau sana ndio maana alimuita brandina chokolaa

"Unasemaje wewe kwani nilikuita hapa au kwanza una njaa umeambiwa hapa ni restaurant ??"

Alifoka femi


"Oooh nimeshachoshwa na hizi drama zako, baada ya kutembea na wafanyakazi wenu wote leo umeamia kwa huyu si ndio ?? (Akamgeukia brandina) we msichana kama ujui hapa unachezewa tu hakuna kitu utapata "

Brandina akainuka na kuwaacha bila kusema neno femi alibaki akiitilia jina la brandina tu, kwa kuwa kelele zilikuwa nyingi sana bi femi alitoka chumbani kwake na kuja sebuleni

"Shikamoo bibi ??"

"Marahaba, oooh nasma karibu "

"Asante umekuja saa ngapi ??"

"Muda sio mrefu "

"Bibi yako anajua kama uko uku ??"

Femi na nasma wakaishia kuangaliana tu

"Haya karibu, femi utamuonesha chumba cha wageni kule, ata hivyo kesho bibi yako ataketa nguo zako kwani utakaa hapa kwa week moja bibi yako anasafiri "

"Sawa....."

Femi akamuita mdada mwingine

"Kamuoneshe chumba cha wageni mpatie taulo, shuka ambazo ziko safi na chakula pia ana njaa sana "

Alizungumza femi kwa hasira sana kisha akaondoka na kwenda kujifungia chumbani kwake....

Siku iliyofuta femi alikuwa bado amechukia sana na wakiwa njiani kuelekea chuoni kila mtu alikuwa kimya lakini nasma akaanziaha maongezi

"Sasa mbona jana nimekugongea mlango ujafungua jamani ??"

Aliuliza lakini pia hakupatiwa jibu

"Kwahiyo bado ata Mere haumpendi ?? Yaani uku una mere uku una brandina sio femi hii tabia ungeacha...."


Femi aliendesha gari mpaka kwenye kituo cha daladala

"Shuka......"

Alifoka femi kisha aka.....

ITAENDELEA
 
FEMI (play boy)

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 11

WHATSAPP: 0676604840

KAWAIDA: 0783642467

SONGA NAYO........

Shuka.......

Alifoka femi akimtana Nasma ashuke kwenye gari yake, kisha femi akatoa wallet yake na kutia not ya shilingi elfu 5 na kumpatia Nasma

"Nafikili hii itakutosha kabisa kukufikisha chuoni "

"Usinifanyie hivyo femi "

"Nisifanye nini ? Nasma unaniona mimi kama Babu yako si ndio ? Usinizoee kiivyo nimesema shuka "

Hapo nasma na michozi ilianza kumtililika maana anamjua femi akiamua jambo lake ameamua uwa arudi nyuma kabisa.....

"Sikia femi niamini mimi siongei tena nasma mimi nafunga mdomo wangu niamini mpenzi wangu "

"Mpenzi tena nasma shuka "

"Basi nawe femi utaniwi "

Femi aliwasha gari akiwa na hasira, sana nasma alibaki akimuangalia tu walifika chuoni wakashuka na kila mtu alipita njia yake yaani kama awajuani vile

"Some one is boring today"

Alizungumza mere baada ya kumkuta femi akiwa ametulia tu na kuonekana kuwa ana mawazo sana

"Femi uko sawa mpenzi??"

Aliuliza tena maana alipofika Femi wala akugeukw kumtama

"Yaah niko sawa "

"Sijakuzoea hivyo mpenzi wangu shida nini niambie "

"Mere naomba nipe muda wa kukutafuta kila nikikutafuta kuanzia usiku wa saa 3 haujibu sms zangu lakini online nakuona nambie ratiba zako nambie natakiwa kukutafuta kuanzia saa ngap ??"

"Ooooh nilipanga kuja kuzungumza ilo na wewe, lakini kama ni ilo ndo lina kusumbua mume wangu mtalajiwa nisamehe sana, ni hivi sio kama napenda ni ratiba yangu kuwa kila ikifika saa 3 usiku ni muda wa kunyoosha mama viungo anafanya ndani ya masaa mawili mimi kuwepo online ni sawa, nakuwa naangalia mazoezi ya mama kwa dokta wake muda huo nakuwa live ndio maana nikimaliza nakuwa nimechoka sana ni kumuogesha mama na mimi kuoga na kulala nisamehe mimi mpenzi wangu najua unakosa muda mzuri wa kuwa na mimi 🥹"

Mere akaanza kulia

"Come here baby "

Mwaya femi mwenyewe akawa mpole akamshika baby wake na kumtuliza

"Sikuwa najua nisamehe mpenzi una majukumu makubwa sana kwenye umri mdogo "

"Femi mama yangu ndo kila kitu familia yangu ndo kila kitu kwangu ujui tu mama yangu jana Amelia sana kwa kukushukuru ana Sali kukuombea ujui tu femi namshukuru Mungu kiasi gani kukupata wewe, kunausa nasema Mungu amekutumia wewe kuja faraja kwenye familia yangu nakupenda mno hakikisha kuwa hauniachi "

Basi mwaya femi alifurahi sana baada ya kusikia maneno mazuri na matamu kutoka kwa mtu ampendaye

"Wacha niende darasani nina presentation "

Aliaga Mere na kuondoka femi alibaki akiwa amekodoa macho tu akiangalia goma lake linavyoondoka

"Femi....."

Alisikika sauti upande wa pili femi akageuka na kuangalia

"Leo ukinigusa nakuumiza swaumu usione siku ile nimekukimbia ukajia leo tena nitakuacha kwanza toka mbele yangu unaniharibia mood "

"Femi nisikize "

"Unataka nini ??"

"Bado nakupenda mno sikuwa kukutana na mwanaume kama wewe please nakuitaji "

"Una kichaa wewe "

"Sawa sawa, ata ukisema me ni chizi naokota sijui makopo ni sawa 🥹 lakini yote kwaajili yako, femi sikuwai kupenda mwanaume Kama ninavyokupenda wewe "

"Khaaaaah kuwa uyaone ndo haya sasa, swaumu yaani unanipenda mimi kuliko familia yako au ebu nitokee hapa si umemuona mke wangu akikukuta nimeisha "

"Femi ata mimi tulianza kama mere kiko wapi ukaniacha subili nikuambie kitu nakuombea maumivu makali ikiwezekana yakuuwe nakupenda sana natamani dunia ijue, lakini sina budi kusema kua wewe ni mnyanyasaji wa kijinsia "

Yaani femi sijui kawafanya nini hawa watu awataki kabisa kuacha yaani hawakubali kabisa wako radhi kushare lakini sio kumuacha femi

"Unataka nini swaumu nimechoka kusikia hizi nyimbo zako "

"Tutoke twende sehemu tukae peke yetu niwe nakuangalia tu hiyo ndo furaha yangu "

"We kweli sio mzima haya usiku mwema binti "

Yaani ndio kwanza ilikuaa ni saa 6 kasoro mchana lakini femi alisema usiku mwema na kuondoka akimuacha swaumu anajililia, femi alizunguka uku na uku akiwatafuta rafiki zake alishangaa Sana baada ya kuwakuta marafiki zake wakiwa wamekaa na mere na mashoga zake tena story zimenoga sana wanacheka na mambo kama hayo

"Itakuwa nachanganyikiwa mere si kaniambia ana presentation anaenda darasani au ?? Ata kama ndo nampenda ndo niwe namuona kila kona au ??"

Femi alimsogelea mmoja kati ya marafiki zake na kumnong'oneza

"Weeeh huyu aliyekaa karibu na frank ni mere au ??"

"Ahahhaha broh umeanza kuumwa lini macho
"

Alicheka rafiki yake huyo na kuwashirikisha wenzie

"Nyie kumbe femi anaumwa macho na amsemi"

Wote wakacheka na kuendelea na story zao jambo ambalo lilimuumiza sana femi yaani amefika ni kana kwamba awamuoni au hawana muda nae hakuwa na sababu ya kuendelea kukaa aliondoka kwa haraka sana lakini pia hakuna mtu ambaye alikuwa na muda nae, kwa muda huo femi alikuwa na maumivu sana

"Bora wote lakini sio frank, yaani frank wa kunifanyia mimi hivi kwa kipi aswaah nimemfanya nini wapi nakosea ??"

Alijiuliza femi kwa muda bila majibu alione kabisa hayuko sawa

"Urafiki aulazimishwi kama ni rafiki yako kama unakosea ana kuambia hakika rafiki wa kweli ni ndugu yako "

Alikumbuka maneno ya brandina akatabasamu akainuka na kuelekea library lakini alisimamishwa na Kevo ambaye alikuwa kule walipo wakina Frank

"Unaenda wapi ??"

"Ebu inua uso wako vizuri halafu soma kibao hapo juu utajua ninakoenda "

"Femi nikuulize kitu "

"Umeanza kuna kitanu naitaji kwenda kusoma uku utaniuliza ata kwenye simu "
Alizungumza femi na kugeukia mbele kutaka kuondoka maana alishachukia sana

"Ni kuhusu mere na frank "

Weeeh mzee baba alivyosikia kuhusu mere akarudi nyuma kwanza maana daaah anampenda huyo binti halagu alivyosikia mere na frank ni kama akili ilitaka kuruka akarudi nyuma chap akamshika mkono kevo na kutoka nae eneo ilo

"Nini kuhusu wao "

"Tuliza mood hiyo baba, frank ni rafiki yako lakini nahisi anakuzunguka sote ni marafiki zako sawa lakini frank ndie mtu wako wa karibu sana sina uhakika lakini nahisi kama anamfukuzia mere kama sio kumfukuzia basi tayali wanamahusiano "

"Mmmmh "

Femi aliishia kuguna tu maana hakuwa anaelewa nini cha kusema

"Usije ukawafata nakuomba fanya uchunguzi wako maana nahisi kuna kitu kwanza uoni sasa hivi frank anakukwepa sana "

Twende mbele na kurudi nyumba huyu Kevo mbona kama mgombanishi tu au mnaonaje maana ananivuluga tu.....

"Sikia kevo naomba niache niende nyumbani kwanza "

"Naweza kukupeleka broh sizani kama uko sawa "

"Usijali "

"Naomba nikupeleke"

Kevo alilazimisha mwisho femi alikubali na kweli alimfikisha nyumbani

"Mmmmh umeenda na mwenzio unarudi mwenyewe "

Brandina akaanza maneno yake pasi na kujua kuwa femi hayuko sawa

"Broh Asante sawa wacha me nikalale unaweza enda na gari I ikusaidie "

Yaani Femi kuhusu kutoa yuko vizuri hana uchoyo kabisa, femi aliingia chumbani kwake akiwa na mawazo sana

"Kuna nini kwani??"

Aliuliza femi akitaka majibu kutoka kwa kevo

"Aaah we acha tu "

Kevo akamsimulia kila kitu brandina

"Yaani kwanini frank anamfanyia mwenzie hivyo hayo ya mwanamke sina muda nayo kwakuwa hakuna ukweli swali langu kwanini frank anamkaushia mwenzie kwa lipi ??"

"Ata me sijui, yaani sasa hivi ameongeza hadi marafiki tena kuna kitu nataka kufanya kwaheri "

Aliaga kevo na kuondoka kaa mwendo wa haraka....

MWAYA MBONA KAMA MWENZENU NAMUONE HURUMA FEMI KAAMUA KUTULIA HALAFU MAPENZI YANAMKATAA.....

ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom