Fei Toto tafadhali ufanyie sana Kazi huu Ushauri wangu mzuri na nakuomba Usiupuuze kabisa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,742
109,178
Mdogo wangu Feisal Salum ( Fei Toto ) leo GENTAMYCINE nimeamua kukupa Ushauri wangu kama ambavyo pia nilimpa Mdogo wangu wa Kinondoni Biafra Jonas Mkude hakuufuata na sasa yamemkuta hadi anakwepa hata Kuonana nami.

Fei Toto najua Sakata lako lote na labda leo niseme tu Ukweli kuwa Mpango uliosukwa Kipumbavu na baadhi ya Viongozi wa Simba SC ili uanzie nchini Uturuki kwa muda kisha urejee Kuchezea umefanyika kwa Kukurupuka.

Fei Toto nakujua Wewe ni Mshabiki mkubwa wa Simba SC ( Kiasili na Moyoni ) kama alivyo Kaka yako na Mzanzibari Mwenzako Rafiki yangu wa Ilala Bungoni enzi hizo Nadir Haroub 'Cannavaro' hivyo ulikuwa unataka Kutimiza Ndoto yako Kuchezea Simba SC ila Waliokuongoza na Kukudanganya wamekosea sehemu ndogo sana.

Mdogo wangu Feisal Salum 'Fei Toto' leo Mimi Kaka yako GENTAMYCINE nakuomba nenda Mwenyewe Klabuni Yanga anza Kwanza kwa Kuwaomba Radhi kwa yote yaliyopita, waambie unataka Kucheza Soka nje ya Tanzania ili wakupe Baraka zote na Leseni yako kisha uondoke / uachane nao kwa Amani.

Fei Toto nikuhakikishie Yanga SC ya sasa Wamejifunza pakubwa hasa Kisheria baada ya Kuteswa na Bernard Morisson katika lile Sakata lake na Simba na Yanga hivyo kwa sasa hawawezi Kukosea tena Wanatamba hivi kwakuwa Walikokubania hakika huchomiki hata ende Mahakama ya Mungu Mbinguni.

Rafiki yako Jonas Mkude nimejitahidi mno Kumsihi abadilike hasa kwa Kulewa Kwake na Kusema Kauli kuwa kabla Mama yake hajafa anataka aichezee Yanga SC ili amfurahishe ambaye imesharekodiwa na Watu na kuwafikia Viongozi wa Simba SC ambao na Wao sasa kwa Makusudi wameamua Kumkomoa kwa kumwambia Kocha asikupange au akupange katika Mechi za Kawaida na zisizo na Umuhimu kivile ili Kukuzuga na Kutuzuga Sisi wana Simba SC tujue kuwa hakuna / huna Tatizo.

Fei Toto bila Yanga Kubariki kokote atakapoenda hatofanikiws kwani GENTAMYCINE nazijua tabia za Siri za hivi Vilabu Vikubwa nchini vya Simba na Yanga wanazowafanyia Wachezaji Jeuri na Viburi.

Kwa msiojua Wazee wa Yanga na Simba pale Klabuni Jangwani na Msimbazi huwa wanaweza / wanatunza Jasho za Wachezaji wao Mahiri na Tegemeo katika Chupa Maalum ili Siku akiwazingua tu wanamkalia Kikao cha Kummaliza Kiuchawi / Kiushirikina kupitia Chupa yenye Jasho lake walioiifadhi Klabuni.

Wahanga wa hivi Karibuni wa Mchezo huu wa Wazee wa Simba na Yanga ni Wachezaji Bernard Morisson akitoka Yanga SC kwenda Simba na Frank Domayo kutoka Yanga SC na kwenda Azam FC.

Wengine walikuwa ni Ramadhan Singano akitokea Simba SC kwenda Azam FC na Victor Costa akitokea Simba SC kwenda Yanga SC.

Fei Toto Mdogo wangu cheza na Wote ila siyo Watu ( Wazee wa Simba na Yanga ) na ndiyo maana naendelea Kusisitiza kuwa rudi Yanga SC, jishushe Kwao, Waombe Radhi, Waage kwa Amani ili Wakubariki na uende zako kwa Amani.

Nakutakia kila la Kheri Mdogo wangu.
 
Fei toto endelea kushikilia msimamo wako uende ukacheze soka nje ya nchi. Fata mfano wa kina Emanuel Adebayor alivyoondoka arsenal kwenda man city.

Kipaji ni mali yako sio ya hao waliokuwa wanadai kukulipa milioni 4 ya karatasi yenye 50% ya madalali, hakuna asiyejua ulikuwa ukilipwa mshahara wa milioni moja tu huku mkataba wako ukiandikwa milioni 4.
 
Mdau wa maswala ya soka la Tanzania na Africa kwa ujumla ameshahojiwa na kasema Fei kakosea na kamshauri aende kwake amwombe awe mtu kati kwenye swala lake na Yanga ili walimalize, huyo si mwingine ni Alhaj Ismail Aden Rage....sasa Fei asilimia kubwa ya wataalamu wa sheria za soka wanamshauri yeye amekomaa na kina Fatuma karume na wababaishaji wa mitandaoni,...elimu ni kitu muhimu sana
 
Kilichobaki👇

IMG_20230506_141218.jpg
 
Sula l
Mdau wa maswala ya soka la Tanzania na Africa kwa ujumla ameshahojiwa na kasema Fei kakosea na kamshauri aende kwake amwombe awe mtu kati kwenye swala lake na Yanga ili walimalize, huyo si mwingine ni Alhaj Ismail Aden Rage....sasa Fei asilimia kubwa ya wataalamu wa sheria za soka wanamshauri yeye amekomaa na kina Fatuma karume na wababaishaji wa mitandaoni,...elimu ni kitu muhimu sana
Suala la mikataba ni suala la kisheria sio la wapiga domo tu .

Hili sakata linaenda CAS ..Yanga lazima wateme bungo
 
Back
Top Bottom