Chromium
JF-Expert Member
- Apr 17, 2008
- 589
- 185
Naombeni msaada wa namna ya kutatua kadhia hii ya benki yetu ya NBC. Jana asubuhi nimechukua fedha wakati naenda kazini. Nikaomba na mini statement. Nikaweka kadi (Master Card) kwenye wallet. Nimerudi jioni benki kuchukua kiasi kingine, kutahayaruki fedha haifiki ile niliyoitegemea! Nikaomba statement nyingine. Ikaonekana fedha imekuwa withdrawn asubuhi (wakati nikiwa kazini na ATM yangu)!
Leo nimewaendelea benki. Nimewaeleza hawanipi ushirikiano wa kutosha. Baada ya kuonana na Meneja, anadai kumbukumbu zinaonyesha hela imetolewa na kadi yangu lakini na "Non local NBC ATM". Kwa mujibu wa maelezo yake maana yake ni kwamba fedha imetolewa kwingine na sio NBC ila kwa kadi yangu! Ananituhumu kuacha kadi mahali na mtu mwingine ameitumia kufanya uhalifu. Lakini ninachojua, kadi ilikuwa na mimi kazini na sikulewa aseme kuna mtu alinipekua! Baada ya kuomba ushahidi unaothibitisha kwamba hela hiyo nimetoa mimi kama anavyodai yeye, akaishia kunishauri nijaze fomu ya madai halafu atafuatilia! Sio siri nimeondoka na stress.
Tafadhali naombeni ushauri wa ninachoweza kufanya nipate hela yangu. Naomba msaada wa taratibu zinazopasa kufuata kudai haki yangu!