๐—™๐—ฒ๐—ฎ๐˜๐˜‚๐—ฟ๐—ฒ ๐—บ๐—ฝ๐˜†๐—ฎ ๐—ธ๐˜„๐—ฒ๐—ป๐˜†๐—ฒ ๐˜€๐—ถ๐—บ๐˜‚ ๐˜‡๐—ฎ ๐—”๐—ป๐—ฑ๐—ฟ๐—ผ๐—ถ๐—ฑ ๐˜‡๐—ถ๐—ป๐—ฎ๐—ธ๐˜‚๐—ท๐—ฎ ๐—ป๐—ถ ๐—ฏ๐—ฎ๐—น๐—ฎ๐—ฎ

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Android kila mara wanazidi kuwa imara sana tutegeme feature mpya Kali amazing zitakuja kwenye simu zetu za Android kuanzia version 14

1) Notification flashes
Kwenye Android 14 utakua na uwezo wa kutumia flash ya kamera Ikiwaka kuonyesha ishara ya kupokea notification toka sehemu mbalimbali. najua mwanzoni hii feature ilikuwepo kwenye baadhi ya simu za Android kama vile Infinix, Samsung pamoja iphone uwezo wa kuweka flash notification kwenye simu.

Lakini hii inakuja na operating system ya version 14 Ikiwa uwezo kuweka Rangi mbili yellow flash au white wakati wa notification inapotokea au kupigiwa simu hii imekuja kusaidia wakati umepoteza simu au umeweka kwenye mazingira magumu ni rahisi kuonekana pia unaweza kuweka vibrate au kuondoa.

2) Satellite Connectivity
apple walikua watu wa mwanzo kutambulisha huu mfumo wa Satellite emergency Sos kupitia Satellite inakupa uwezo wa kukusaidia kupata huduma ya dharura kwenye maeneo ambayo akuna mtandao kabisa. Android nao wameamua kuleta huu mfumo kwenye simu za Android version 14.

Utaweza kutoa taarifa polisi au kwa ndugu Ikiwa kwenye eneo ambalo akuna mtandao alafu umepatwa na majanga.

3) App cloning
Kutumia akaunti mbili za app Zako kwenye simu moja ni jambo la kipee sana kuweza kupunguza Matumizi ya kupakua app mara mbili mbili najua mwanzoni ilikuwepo hii feature ila kwa app baadhi tu kama vile Facebook, Instagram, Whatsapp nk.

sasa kwa app zote utaweza kuzitengeneza app moja ziwe mbili Kisha kuweza kutumiwa na mtu Zaidi ya mmoja kwa urahisi tu.

4) Drag and drop
Aisee kwenye Android 14 utakua na uwezo wa kuhamisha kitu chako toka sehemu moja kwenye nyingine bila kubonyeza sehemu ya copy we unaishikilia tu picha Kisha unaipeleka sehemu unayotaka kama kwenye status Whatsapp au message nk bila kubonyeza copy yani drag na ku drop kama unatumia mouse vile .

5) Data sharing
Hii ni feature itaweza kukusaidia kujua kama Kuna app inatumia data Zako kushare baadhi ya taarifa na app nyingine bila wewe kujua mfano location, sms, call logs nk utakua unapewq taarifa labda Whatsapp inatumia taarifa ya location Zako kwenye app Fulani au sehemu Fulani.

Hii itasaidia sana kupata zile app ambazo sio Salama kwako kuweza kufuatilia bila wewe muhusika kujua.

android14.jpg
 

Attachments

  • Samsung-One-UI-6-adottera-la-funzione-Drag-and-Drop-di-Android-14-large.jpg
    Samsung-One-UI-6-adottera-la-funzione-Drag-and-Drop-di-Android-14-large.jpg
    28.8 KB · Views: 10
Kila siku ni maboresho mapya!
Ni vizuri lakini ina Garama zake za kubadilisha simu ili iweze kuendana na maboresho mapya.
 
Sema kwenye hiyo feature ya emergency services kwa mazingira ya bongo hapa inaweza kuwa ya mashaka sana.

Emergency tu ambayo ipo saizi mara kibao nimejaribu kupiga lakini simu inakata kuonesha kama ni huduma ambayo bado haijawezeshwa.
 
Sema kwenye hiyo feature ya emergency services kwa mazingira ya bongo hapa inaweza kuwa ya mashaka sana.

Emergency tu ambayo ipo saizi mara kibao nimejaribu kupiga lakini simu inakata kuonesha kama ni huduma ambayo bado haijawezeshwa.
Ni changamoto ila hii itakua inatumia mfumo wa Satellite kuweza kufanya mawasiliano ivyo ikitokea umepatwa na changamoto kampuni uilnunulia simu Wana uwezo wa kuona wap umekwqma na kupata msaada


Either kuwapa taarifa watoa huduma kwa wateja pamoja na polisi juu ya wapi ulipokwama ila ngoja tuone tutaweza kwa polisi Wetu wa kitanzania
 
maboresho ya maana sana, nashindwa kusubiri!
Vumilia yanakuja boss ila unaweza kutembelea page Yetu ya telegram


Kujifunza Zaidi
 
Enhee...
Zije tuone tu!!
Usijal we vumilia zinakuja boss pia unaweza tembelea page Yetu utajifunzaa Zaidi ya telegram

 
Maboresho ya maana sana, nashindwa kusubiri!
Kufa sasa kama unashindwa kusubiri. Kiingereza na kiswahili ni vitu viwili tofauti bro, usifanye direct translation.

I can't wait haimaanishi "siwezi kusubiri" bali "natamani iwe hivyo" au " au natamani iwe kweli"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom