Father: Son of politician elopes with my daughter

Mar 29, 2015
4
0
Article hii ilichapishwa kwenye gazeti la the Citizen ya tarehe 8/2/2015

Mwandishi akiwa Imani Makongoro. Link Hiyo hapo chino.

http://www.thecitizen.co.tz/News/national/Father--Son-of-politician-elopes-with-my-daughter/-/1840392/2617026/-/bn8w01z/-/index.html

Dar es Salaam. A Tabata resident in Dar es Salaam, Mr John Kayombo, has accused a son of politician Fred Mpendazoe of impregnating and eloping with his daughter, who is a schoolgirl.

Mr Kayombo told this reporter at Tabata Relini recently that Vitalis Mpendazoe, son of the former Kishapu legislator, has been cohabiting with the daughter -- a Form Five student at Songea Girls' Secondary School -- at his parents' Tabata home since last year.

"On September 13 last year, the headmistress of Songea Girls' Secondary School phoned me to pick up my sick daughter. I did so and two days later I sent her to hospital for examination. It was established that she was pregnant. When I asked who had put her in the family she mentioned Mpendazoe's son, Vitalis," Mr Kayombo said.

He added: "I communicated with Mpendazoe, who told me my daughter and his son had fallen in love and I should leave them to live together. I was extremely disappointed at the response."

Mr Kayombo said he reported the matter to the Tabata Police Station. The case was assigned to a detective on December 17. He said, while investigations were still going on, sadly his daughter had a miscarriage because, according to some medics, the embryo was implanted outside the uterus.

"Vitalis went around saying I won't make any headway in my case. I reported the matter to the police," lamented the father.

He said on December 28 he received a call from the Tabata officer commanding station (OCS), Ms Leokadia Kobelo, telling him that the case would not proceed because the daughter was aged above 18.

"Vitalis has been cohabiting with my daughter at his parents' home as a husband and wife!" said the distressed parent.

Songea Girls' Secondary School head Tupoke Ngwala said Mr Kayombo's daughter was discontinued from school after it was established that she was pregnant. "All information has been communicated to the parent."

When contacted, the Tabata OCS denied knowledge of Mr Kayombo's case.

"He was supposed to talk to me instead of rushing to the media," the OCS said.

For his part, Mr Mpendazoe said the case involving Mr Kayombo's daughter was discontinued because she was above 18, of sound mind and an adult capable of making-her the daughter was aged above 18.

"It isn't true that the girl is staying at my house and I haven't seen her for a fairly long time. I remember the last time she came to me, saying she had a dispute with her father and I'm the one, who sent her to the police, who advised her to stay at her grandfather's home. Therefore, I don't know her whereabouts and I'm on my way to Shinyanga," Mr Mpendazoe said.

Vitalis admitted knowing the girl, but claimed she was not a secondary schoolgirl. He insisted that she was doing a certificate course in a city college he did not name.

"Her father threatened to kill her and me. That forced her to leave home. I've been communicating with her although I don't know where she lives now. She isn't a schoolgirl," insisted Vitalis.

Vitalis also claims that the girl was forced to abort, the accusation that Mr Kayombo rejects, saying doctors told him that the pregnancy was ectopic, with the embryo implanted outside the uterine cavity. Mr Kayombo asks the media and well-wishers to help so that his daughter would return home and continue her studies.

Mr Kayombo added, however, that although Mpendazoe and his son claim not to know the whereabouts of the girl, she still lives in their home.

Kutokana na wadau wenye mioyo ya kupenda haki. Wemeweza kunipatia nakala ya makala ilioandikwa na Kareen iliotumwa Leo Mwenda the Citizen kwa mwandishi hiyo.

Nimeona nivyema kuweka the first version.

Nakusalimu wewe msomaji wa gazeti hili. Namshukuru Mungu kwa kunipa afya njema hadi sasa na kunipa nafasi hii yakuendelea kutimiza na kupigania ndoto zangu.

Mimi Kareen nimefikia uamuzi huu mgumu wa kusema haya ninayo yakusudia si kwa mapenzi yangu ila Ni kutokana na mazingira niliojikuta nikiwemo kutokana na baadhi ya vitendo visivyopendeza vinavyofanywa na baba yangu. Kiukweli kabisa ninaipenda familia yangu.

Mnamo tarehe 8 mwezi wa pili nilipata kusoma nakala ilioandikwsa na mwandishi wa gazeti la The Citizen toleo la jumapili. Katika habari hiyo, nilishtushwa na kuumia Sana pale nilipoona kuwa inahusu suala lililonitokea Mimi kama mhusika ikielezewa na Baba yangu akimshutumu kijana mmoja kwa kunitorosha na kuwa Mimi na ishi nae katika nyumba ya mzazi wake.

Kweli Ni mzazi wangu ILA kwa kitendo hicho cha kuweza kupeleka suala Hilo magazetini na kudanganya umma kinanisononesha Sana .

Nataka nieleze wazi kwamba sikai nyumbani kwa Mpendazoe,nimepanga nyumba yangu na ninajisomesha chuo mwenyewe. Siwezi kukata kwamba sikupata ujauzito. Hilo ni jambo la kweli kabisa ila haikua ectopic kama alivyodanganya baba yangu,ilikuwa vizuri lakini baadae ikatoka yenyewe na daktari akasema inatokeaga ukiwa na msongo wa mawazo(stress) au maumbile ya mtu.

Nilikua nasomo Learn IT coarse ya certificate in Business Administration intake ya mwezi wa nne. Nilijiunga na Chuo hicho baada kufikia muafaka na Baba yangu mwenyewe alienipigania kwa hali na Mali ili nisome Chuo baadala ya kuendelea na "A" Level ambapo kaka Zangu, dada yangu na mama yangu walipinga Sana kwa wakati huo. Ikafika mda, mama yangu akakubali uamuzi wangu wa kwenda Chuo badala ya sekondari.

Mama akajitaidi kufanikisha kunilipia Ada. Nikaanza masomo tarehe 28 mwezi wa nne mwaka 2014. Baada ya mda niliamua kufanya kazi part time ya social network support katika kampuni ya marketing moja iliopo sinza. Na PIA vijisenti nilivyopata nikaanzisha biashara ndogo yakunikidhi maitaji madogo madogo ya hapa na pale.

Baba yangu alibadili msimamo wake wa Mimi kuendelea Chuo. Alitaka niache niende sekondari baada ya kushawishiwa na marafiki zake. Kitu ambacho Mimi binafsi sikukitaka na Mara kwa Mara nikieleza mawazo na msimamo wangu huo ilizua ungomvi Kati yangu na Baba yangu.

Ila kwa upendo niliokuwa nao kwa wazazi wangu na kwa mwenzangu, nilikubali. Hapo tayari nilikua mjamzito .tarehe 12 August nlienda shule nikakaa hadi tarehe 13 september nlipoondoka sababu ya kuumwa .Nilirudi Dar nikaenda hospitali (SANI*** MIKOCHENI)tarehe 17 september .

Daktari (DR.FRED LIMB****) ambaye ni rafiki wa familia alinipima na kuniambia nna ujauzito,nilimwambia nipo tayari kuitunza.Baadae akaongea na baba.

Baada ya Baba kuongea na daktari, aliniambia kuwa wamekubaliana niitoe endapo nitakubali ili niweze kurudi shule mapema bila ya wao shuleni kujua na hata mama asijue wala mtu yeyote. Nilishauriana na dada yangu happy na kumuambia kuwa Mimi siwezi toa mimba.

Dada yangu aliniunga mkono na akaniambia kuwa atakua na Mimi kwa hali na Mali. Niliitwa chumbani kwa ndugu yangu ambaye Ni daktari katika hospital hiyo. Nae akaniambia kuwa Baba anataka niitoe na yeye atafanya hivyo endapo nitakubali na pia alinishauri nifanye atakavyo Baba yangu.

Maana alisema kuwa mimba bado sio kubwa Sana ikiwahiwa haitaleta madhara yoyote.Baba na rafiki yake huyo wanaonekana kuwa wazoefu maana baba alisema,"usiogope ,siwezi kukushauri vibaya,tumeshawatoa wasichana wengi ujauzito na sasa wapo salama"Sikuamini kuskia haya.Alisema kuwa yeye,Dr. Fred na daktari mwingine ambaye hakumtaja ni watu wazoefu.

Nlishikilia msimamao wangu wakutokutoa.Mwenzangu alikua tayari kunitunza na kunisaidia kipindi chote hadi nipate mototo.Baba aliendelea kunilazimisha nitoe mimba lasiivyo atanifukuza nyumbani na nisimjue tena.Pia alisema atafurahi nikifa kwani nitampunguzia mzigo.

Baada ya wiki mbili nilimtumia ujumbe wa simu baba wa mwenzangu kumuomba tuonane,alikubali.Nilienda kwake na baada ya muda akaja kutoka kazini,alimpigia mwenzangu pia aje.Nilimueleza jinsi hali yangu ilivyo matatani na nikamuomba nikae kwake kwa muda huku wakiendelea kuwasiliana na baba,alinikubalia na kuniuliza maswali kadhaa pia akamuita mwenzangu nakumueleza yaliyojiri.

Tuliamua kutoa taarifa kituo cha STAKI SHARI tukapewa rb .Baba wa mwenzangu alijaribu kuongea na baba lakini kila akipiga simu alimtukana na kumtishia vitu vya ajabu,pia alikua anatuma ujumbe wa simu mara kwa mara akimtishia baba huyo.Hali ilikua hivyo hadi tulipoitwa kituoni TABATA SHULE,kila mtu alitoa maelezo yake,mwenzangu alitoka kwa dhamana lakini aliambiwa audhurie kila siku hadi kesi itakapoamuliwa na alifanya hivyo.

Mimi nilikaa kwa babu yangu Thomas huku nikiendelea na chuo,chakushangaza hakuwahi kunipa hata nauli ya kwenda shule wala pesa ya hospitali nikiumwa.

Walikubaliana kufanya kikao nyumbani kwa babu kikao cha kwanza kilifanyika jumapili tarehe tano mwezi wa kumi. Nilika huko kwa babu nikisubiri kwa hamu kujua nini kitakachojiri siku huyo. Nikiwa kibarazani na bibi, niliwaona ndugu wa mwenzangu wakiwasili.

Katika kikao hicho, Baba yangu alitaka aombwe msamaha na Baba wa mwenzangu, alitaka kujua gharama za malezi kama chakula hospitali na kadhalika zitagharamikiwa, na PIA gharama za malezi ya mtoto mtarajiwa na gharama za elimu yangu zitagharamikiwa na wao. Ila kikuu zaidi alitaka katika hayo yote alipwe milioni ishirini na laki nane kama malipo ya gharama alizozitumia kunisomesha shule tangu vidudu.

Kwa umbali niliokuwapo nilidhani sikusikia vizuri. Kwenye kikao hicho mama yangu hakuwepo na waliamuru mazungumzo yawe ya wanaume Tu na wakina mama wasiambiwe chochote kwani yeye ndio mwenye maamuzi ya mwisho. Ndugu wa mwenzangu waliondoka.

Kuhakikisha nilichosikia. Nilimpigia mwenzangu anijuze kilichojiri. Alinieleza vile kama nilivyosikia mwanzo.Nili Mimi PIA nilijihisi kama vile nimekuwa bidha ilioko sokoni. Nilimjuza bibi yangu kuhusu kilichojiri aweze kuongea na babu ili washauriane upya ili hiyo gharama ifutwe. Nilikasirika Sana nakumuambia mama kuhusu uamuzi huo na ndugu zangu wengi hawakulipenda.

Wote walimsihi Baba yangu aachane na Dai Hilo na ashughulikie vitu vya msingi. Siku iliofata, nilimuomba mwenzangu aweze kunisaidia niweze kurudi chuoni Learn IT niendele na masomo maana nilikosa miezi miwili amabayo nilikua na uwezo wa kufika walipo wenzangu.

Alikubali na kunisaidia katika Hilo. Nilirudi chuoni nilipokiwa nimeanza mwezi wa nne. Ila kwa mda huo niliamua kuingia masomo ya jioni kutokana na hali yangu. Mwanzangu alijitahidi Sana kunihudumia kwa kipindi hicho.

Aliniwezesha kufikanchuoni na kunifuata usiku saa moja. Aliweza kumalizia Ada ya hapo chuoni. Mbali na hayo gharama za kwenda hospitalini kwa ajili ya matibabu na check up aliniwezesha na kila Mara aliweza acha shughuli zake na kuambatana na Mimi.

Saa zingine dada na mama PIA waliambatana na sisi PIA. Chuo kilinisaodia PIA kupunguza msongo wa mawazo niliokiwa naupata. Baba yangu hakuwa na furaha na Mimi. Mara kwa Mara yeye hakujali suala la hali ya afya yangu. Baba na wenzake mawazo Yao yalikua kwenye kupata unafuu wakifedha.

Mara nyingi niliwasikia wakiwa wanapanga jinsi gani watakavyo gawana na nitumia hizo pesa. Nilikuwa naumia Sana kuona mzazi wangu, Baba yangu kujali pesa kuliko afya yangu kuliko uhai wangu.

Kikoa cha pili kilifika. Katika kikao hiki, mwenzangu alikuwepo. Baba wa mwenzangu alikuwa ametoka kufanyiwa upasuaji ILA alijitaidi kuwepo baada kukosa kikao cha kwanza. Itikadi za kimila zilifuatwa. Salamu zikatolewa. Fedha za beberu nazo zikatolewa. Baba wa mwezangu aliomba radhi kwa yote yaliotokea. Aliomba msamaha kwaniaba ya yeye kama mzazi maana Baba yangu alidai kuwa alimdhihaki kwa kumtumia mama mdogo Richard kama mshenga kinyume na taratibu za mila jambo ambalo halikua na ukweli wowote. Ila Baba huyo akaomba msamaha ili mazungumzo yaweze fanyika.

PIA alifikisha ujumbe wa msamaha kutoka kwa mwenzangu maana kimila haruhisiwi kuongea katika vikao vya haina hii. Walikuja na mshenga anaetokea kijiji kimoja nu huko kwetu kutokana na amri waliopewa Baba yangu kuwa mazungumzo lazima yaendeshwe na mshenga. Yote hayo waliyafanya kwa utiifu. Ni uvumilivu wa hali ya juu. Ingekua Mimi ingeniwia ugumu.

Kutokana na kukubali majukumu kutoka mwanzo naamini kwenye vikao vyao vya ndugu wa mwenzangu mwenzangu alitoa msimamo wake wakubeba majukumu yote yanayohusiana na ujauzito wangu. Baba huyo alisema kuwa malezi yangu na mtoto, elimu, matibabu, yote watayabeba wao. Maana wao waliona kuwa hayo Ni mambo matano makuu yakuyatekeleza ukijumlisha suala la uombaji msamaha. Kwenye kikao hicho PIA walitoa laki Saba nusu kama pesa za kugharamikia usumbufu uliotokea.

Baba na ndugu wengine waligawana na kwenda kunywa pombe kwa furaha baada ya kikao ,babu yangu asinipe hata hela ya nauli wala matibabu ilikua kama haoni nipo kwake bali alinisema mara kwa mara nikiamka .

Yote hayo waliyatekeleza .Chakushangaza baba alikana kuwa hakupokea pesa yoyote alipoulizwa na polisi. Waliomba na kusihi kuwa Hilo la milioni20 liweze kutolewa maana hali ya uchumi wao sio mzuri. Walijibiwa "kuwa shida haigongi hodi wewe si unataka kugombea uraisi, uwezo wakupata hizo pesa unazo. Nenda kakope popote uzilete" alisema Baba yangu.

Walijaribu Sana kujieleza ndipo Baba na babu Zangu walishuka mpaka milioni kumi. Ndugu wa wenzangu wakiomba hudhuru watoka nje Mara moja. Waliongea huko Kisha kurudi baada mda. Kikao kiliendelea na wakasema wanaweza kujitaidi kutoa milioni tano ILA kwa kukopa huko na kule kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki. Baba yangu alikasirika nakuja juu alisema kuwa bado anadharaulika kwa kupewa milioni tano. Babu ndipo alipomshika mkono na kumvuta chini akae. Wakakubaliana baada ya mwezi wakutane tena kujua kama hiyo milioni tano utakuwa imepatikana.

Kipindi hicho hicho mwalimu mkuu songea girls alikuwa amekuja Dar kwenye semina na alikua na shahuku ya kujua maendeleo ya matibabu yangu na nini nilichukwa naumwa. Baada ya kikao hicho ndipo Baba akamueleza kuwa nilikua na ujauzito. Kikao kifuatacho kilipangwa baada ya mwezi mmoja mnamo tarehe 30 mwezi wa kumi na moja.

Baada ya hapo kuyokuelewana kwangu na Baba yangu uliendelea tena hasa kuhusiana na suala langu la kuendelea na Chuo. Kwa mda huo sikuweza kukubali maana kukaa nyumbani ilikuwa shida maana ngomvi kila Mara. Na sikutaka tena kukaa na Baba. Babu nae alikua ananilazimisha nienda kwa na Baba.

Kwa kipindi hicho dada yangu alaikua anatafuta internship kwa ajili ya project zake za Chuo. Sikuweza kukubali kurudi kwa Baba niwe nakaanae peke yangu maana imani ilishatoweka na hofu ilinija hasa kuhusu usalama wangu. Wote nyumbani walikua wanaondoka na kumuacha mwenye. Kaka Zangu, dada yangu hadi mama nae alishaondoka. Nivigumu kuwa mvumilivu siku zote.

Na hivyo nilikata keenda kwake na kutaka kwenda kukaa kwa mama. Cha kushangaza, suala hili nalo lilifikishwa polisi na ndipo aliambiwa kuwa Ni vyema nikakae kwa mama ili niweze kupata kuhudumiwa vizuri. Niliondoka na kwenda kwa mama. Niliendelea na Chuo pale Learn IT.

Ila hali yangu ya kiafya haikuwa nzuri. Kila baada ya siku mbili au tatu ulikua lazima niende hospitalini kwa ajili ya matibabu. Siku moja ndipo tuliambiwa kuwa ujauzito umeshindwa kukua zaidi.

Nikapewa dawa zakuongeza damu na za kuboost ukuaji wa mimba. Mda huo ulikuwa kama wiki kumi na mbili ili ultrasound ilionesha wiki kumi. Mara ya pili tulienda tena na ikaonesha wiki tisa. Baada ya wiki ndipo niliambiwa kuwa inanibidi niitoe mimba kutokana na kutokudevelop kwa mimba. Tukiwa katika hospitali hiyo TMJ mwenzangu alitokwa na machozi.Nilipewa dawa na daktari nikaenda nyumbani. Baada ya siku mbili ndipo reaction ilitokea nakuwaisha hospitalini.

Mwenzangu alinikuta hospitalini maana wakati huo nilikuwa natokea kwa mama . Mama alimtaarifu Baba kuhusu hali yangu. Mwenzangu akatoka kwenda kunitafutia chai na vitu vingine vya muhimu.

Baba alikuka kumuona ILA hakukaa Sana . Alimuambia mama kuwa asimuambie mwenzangu na ndugu zake kuwa mimba imetoka. Hakufahamu kuwa siku zote za matibabu yeye ndio ananileta na kunihudumia. Baada ya mda daktari alikuja na kunipa matibabu. Kisha na mwenzangu akafika. Akafanya malipo ndipo nikaweza toka hospitalini hapo.

Mama alimueleza mwenzangu kuwa alikiwa amekatazwa kumwambia kuhusu hali yangu. Na PIA mama alisema kuwa bora hakuwepo wakati Baba alipokuja maana chochote kingeweza tokea.

Nilirudi nyumbani na mama. Siku kadha zikapita nikaambiwa niache Chuo kwamba napoteza mda. Nijiandae kurudi sekondari. Niliwas na mwenzangu na kumuuliza kama wameshaipata hizo milioni tano. Haikupatikana pesa yoyote. Aliniomba ushauri afanye nini. Nikimuambia kuwa asisumbuke na malipo hayo maana Mimi sio bidha ya kuuzwa. Ukifika siku hiyo. Mshenga alipiga simu na kuwaambia wakina babu na Baba kuwa pesa hazijapatikana.

Kutokana na ukosefu wa pesa hizo, Baba alimuamuru mkuu wa kituo kuprocess shitaka liweze kusonga mbele ili liende mahakamani. Siku zikapita nani nikaitwa kituoni kwenda kujaza pregnancy sheet Yao na mwenzangu aliambiwa aende peleka RB namba ya taarifa tuliotoa wakati ile nilioenda kwao.

Kwai hiyo tukapanga twende pamoja. Tukafika kituoni tukisindikizwa na marafiki endapo chochote kitakachotokea kuwepo watu wakutoa taarifa. Baada ya mda tukaanza kuondoko. Mwenzangu akarudi kujaza jina lake kuwa ameripoti kituoni jamba ambalo alikua anafanya kila Mara kila siku. Tukaondoka.

Kila siku zilivyoenda nilisakamwa kuhusu uamuzi wangu wa kutaka kwenda Chuo. Na PIA nikawa na lazimishwa nionge na Baba kuhusu shule. Kwa uchungu niliokiwa nao wakati huo Hilo jambo sikuweza lifanya. Niliona Ni bora nibaki nyumbani na kutokwenda shule kabisa kuliko nionge na Baba.

Siku zikaenda. Babu yangu mmoja alikua amekuja kutoka singida na kufikia kwa Baba n Aliniomba niende kumtembelea, Nilimuahidi kuwa ntaenda. Tarehe 27 mwezi wa kumi na mbili nilienda kumsalimia Babu. Nilipofika nyumbani sikuwakuta.

Nikaamua kumsubiri.walirudi mida ya saa 12 jioni,nikaanza kuongea na babu. Baba akanipmba nimsonge ugali na kumuungia nyama. Nikafanya hivyo ILA nikawambia kuwa yanibidi niwahi kurudi nyumbani nikaokaa na mama. Hapo ndipo matatizo yakaanza tena maana Baba hakutaka niondoke. Nikamuomba babu aongenae maana sikutaka nikae hapo kwa siku hiyo na wala siku za karibuni.

Nilipigia simu mama nae akasema niwaage nirudi kwake. Nilivyoanza kujianda kuondoka. Baba kampigia simu mama na kumkaripia kuwa kwanini ananiruhusu kuondoka. Mama akanipigia na kuniambia nisiondoke na kama nikiondoka nisirudi kwake. Nilijisikia vibaya Sana kuona kuwa hata mama yangu ananigeuka maana wakati wote wa Sakata hili amekuwa akitengwa katika hatua zote za maamuzi juu ya maisha yangu.

Ila Hilo nalo halikunivunja moyo. Niliondoka na kwenda kulala lodge ya karibu. Nikiwa huko nilimtumia ujumbe mama kuwa nimeondoka lakini majibu yake yalionyesha kutokujali kwani alisema hataki balaa nisiruri kwake. Siku hiyo ya jumapili ndivyo ilivyoisha nnikiwa nimemuumiza moyo mama yangu kipenzi kwa kukataa kukaa kwa Baba yangu. Kesho yake asubuhi mwenzangu alienda kuripoti kituoni kama siku zote zingine.

Alipofika huko ndipo aliambiwa kuwa case hiyo alioifungua Baba yangu dhidi yake ya Dai kuwa amenitorosha kutoka shuleni imefingwa sababu mimi ni mtu mzima, na pili kuwepo na taarifa kituoni tulipoenda Toa taarifa kuhusu ujio wangu kwao na maamuzi yangu Nimeyafanya nikiwa timamu. Mwenzangu alifurahi Sana. Aliniuliza nilipo na Kisha kunifuata.

Tukasali na kumshukuru Mungu kwa kuotuokoa katika hili. Nilijaribu kuwasiliana na mama ILA hakuwa anapokea simu Zangu. Baba yangu ndipo hapo hakutaka tena kusikia jina langu kwa sababu nilikata kufanya maagizo yake ya kuandika kuwa Nina umri mdogo aliniambia mimi si motto wake na niendelee na umalaya. Hapo ndipo nilikuwa na kitendawili cha kukitegua.

Niende ishi wapi maana mama yangu kanikasirikia na Baba yangu ndio hata nisiwaze maana huko kituoni mapolisi na mkuu wa kitua wametukanwa kupita kiasi mpaka nawaonea huruma. Mwenzangu nae alikuwa anasafari ya kikazi kwenda shinyang kahama. Alichonisaidia Ni kuniachia pesa ya kulipia lodge na pesa za matumizi.

Siku aliokuwa anasafiri, tulipigiwa simu wakati tofauti na mwandishi wa gazeti la the citizen na kusema kuwa Baba yangu alienda huko kuomba atoe makala kuhusu Mimi. Na kua Mimi Ni mwanafunzi nilietoroshwa shule nakua naishi na mwenzangu kwa mzazi wake.

Nilimuambia kuwa Mimi Ni mwanachuo na hayo yote yalitokea wakati niko Chuo na ghafla kupelekwa sekondari nilipokaa karibia mwezi mmoja na kurudishwa nyumbani. Na PIA nilimuambia kuwa siishi na mwenzangu wala kwa mzazi wake.
Ila mwandishi huyo huyo ndie ameandika makala ya kuhusu suala hili.

Sina kinyongo nae na ninampongeza kwa kazi nzuri ILA kama mmoja wa wauisika au mhusika mkuu ninahaki ya kuhoji uhalali wa makala yake dhidi mzazi wa mwenzangu bila ya yeye kufanya utafiti yakinifu.

Sawa ameripoti kwa kunuku na lakini mbona taarifa alizo ripoti zimelalia upande mmoja? Kama muandishi anaefanya investigative reporting analazimika kutafuta facts za kusuport habari yake na si kuchukua habari kwa juu juu.

Kuhusu mimba kuharibika Hilo likitokea mwezi wa kumi na moja. Ila nilianza kulazimishwa kutoa mimba mwezi wa tisa, miezi miwili kabla. Najua kuwa kiheshima na kidesturi na kimili si vizuri kumsema mzazi kuwa Ni muongo. Ila ninalazimika kudiriki kuweka hivyo maana sio jambo zuri lililofanyika. Nimenyanyasika na kushtumiwa ili niweze Toa mimba kwa manufaa yake.

Nilielekezwa kuandika umri mdogo iko nimuweke mtu ambaye Hana hatia hatiani, nilitolewa Chuo ili niede sekondari ili mazingira yawe yamekaa kuashiria kua Mimi Ni mwanafunzi iko pesa ziweze patikana. Najisikia vibaya kuwa chambo katika mchezo huu niliojikuta nikiwa kama mtaji wa kupatia pesa.

Kuitwa Malaya na maneno mengi mengine yasio FAA kwa mzazi kwa mtoto kisa ya kukataa kutii kutoa mimba. Saa nyingine huwa nafikiria kama ningekubali kubadili miaka yangu na kumweka mwenzangu hatiani ingekua kwa faida ya nani? Yangu au Yao?

Laki Saba na nusu waliopewa kwa ajili ya matibabu na malezi mengine ILA hata nauli ya Chuo sikupewa. Hata nauli ya kwenda hospitalini sikupewa.

Hata siku yakuumwa kwangu na mimba kutoka sikulipiwa . Kama mtoto inauma Sana kuona hivi vitendo vinafanywa dhidi yangu na mzazi wangu. Baba yangu anatakiwa kua kimbilio langu na siobtishio au kitu changu. Kusemea magezetini si aibu ya familia moja Bali ya familia zote.

Na isingekua Baba huyo wa mwenzangu kunisaidia kuto kutoa ujauzito siku leo ningekuwa wapi. Siku zote sikujua kuwa yeye Ni mwanasiasa mpaka niliposoma makala ya huyo mwandishi. Kama watanzania wote wengekuwa wanamoyo wakuokoa viumbe visivyo na hatia kama huyo Baba tungekuwa nchi ya kitofauti.

Sikubaliani na utoaji mimba hata siku moja na hata ikitokea ikajirudia ningefanya uamuzi huo huo wakutotoa mimba. Wasichana wenzangu tuwe na ujasiri wa kutotoa mimba maana Ni hatari kwa maisha yako na ni dhambi mbele ya mwenyezi Mungu.

Maisha ya binadamu hayana price tag. Thamani yangu anaijua Mungu Tu. Mimi sio wa milioni kumi wala ishirini. Nawaomba wazazi mtuelewe na mtuthamini sisi watoto hasa pale tikiteleza. Busura na hekima zianzie kwenu ili sisi tuige mfano mzuri. Thamani ya elimu Ni kubwa na elimi bora Ni ile ipendwayo na asomae na sio asomeshae. Tusikilizeni sisi watoto. Tunajua yanayotusibu zaidi maana sisi ndio wahusika wakuu.

Napia wapeni wakina mama zetu nafasi za kuongea na kufanya maamuzi katika familia. Udiktwkta haufai na haujengi Bali hubomoa familia na nchi kwa ujumla. Mfumo dume ushapitwa na wakati. Siukubali na nawasii wasichana wenzangu na wakinamama tufanya hima kuondokana na mfumo huu kwa kana kwamba wote tuna hali sawa katika jamii.

Wazazi wangu na familia yangu naipenda Sana. Nakupenda sana Baba yangu na yote nimeamua kuyasahau. Nakupenda Sana na nakutakia maisha marefu na baraka Tele. Naomba mnisamehe kama kitendo hichi kimewakwaza ILA ndani ya nafsi yangu roho imenishinikiza kufanya jambo hili kuweka ukweli bayana. Tena naomba mnisamehe kwa yote. Mungu awe pamoja nasi daima.Nawapenda wo
te

Baada ya uamuzi kutolewa. Alifukuzwa nyumbani kwa kuwa hakukubali kufanya matakwa ya Baba yake pale alipomuambia abadili miaka yake na andike kuwa yuko na umri wa miaka 17. Pia ugomvi mzima no pale tu alipo Fanya uamuzi Wa kutotoa mimba. Nyumba ikawa chungu. Wanajamii Forum, Mimi Hi MTU niaeamini kuwa kila kiumbe kinahaki ya uhai na sikubali na Article hii ilichapishwa kwenye gazeti la the Citizen ya tarehe 8/2/2015

Mwandishi akiwa Imani Makongoro. Link Hiyo hapo chini.

http://www.thecitizen.co.tz/News/na...hter/-/1840392/2617026/-/bn8w01z/-/index.html

Baada ya uamuzi kutolewa, Alifukuzwa nyumbani kwa kuwa hakukubali kufanya matakwa ya Baba yake pale alipomuambia abadili miaka yake na andike kuwa yumo na miaka 17. Pia ugomvi mzima no pale tu alipo Fanya uamuzi Wa kutotoa mimba. Nyumba ikawa chungu. Wanajamii Forum, Mimi Hi MTU niaeamini kuwa kila kiumbe kinahaki ya uhai na sikubali na suala la kutoa mimba na nilimuunga Mkono katika kila hali.

Je, nilivyokuwa Shinyanga na kupewa taarifa ya kufukuzwa kwake. Nilifanya uamuzi Wa kumsaidia kupata hifadhi na kuweza kujitegemea?

Je, nilifanya kosa kukaa kimya mda wrote Wa kuandikwa magazetini kwa kashaf isio na ukweli?

Je, pale Mpendazoe anapochafuliwa bora sababu za msingi na kutofanya chochote ni jambo la kijinga ama no udhaifu?

Je, pale unapomuona mzazi anatumia mwanae Kama chanzo cha kupati mtaji na kulikalia kimya ni udhaifu?

Je, pale unapoitwa police central kwa Mara kwa Mara na kutii wito ni udhaifu?

Je, pale unaopoona bongo unatungwa dhidi yako nakutofanya polite in ujinga?

Kwa dunia na elimu an exposure ya sasa ni ujinga Wa hali ya juu kumchukua MTU na kuishi nae kwa mzazi wako.

Mpaka hapo kuna defamation nyingi zilizofanyika bila kuchukuliwa hatua yoyote. Kusiamia misimamo ya kutotoa mimba ni jambo la muhimu Sana katika nchi hii.

Ninaliomba jeshi la polish pale nitakopofika kesho Central Police kwa wito wao pia wachukue hatua ya kuchunguza allegations za utoaji mimba na makosa mengine. Kisingizio cha kusema kuwa Penal code/ criminal law is not retrospective inabidi iwekwe pembeni maana utoaji Wa ushahidi tayari no being retrospective.

Kesho SAA tatu Niko central polic kuhusu hili suala.

Utoaji wa mimba tulipinga na tunazidi kupinga na namuunga Mkono katika kila hali na Mali katika maendeleo yake.

Je, nilivyokuwa Shinyanga na kupewa taarifa ya kufukuzwa kwake. Nilifanya uamuzi Wa kumsaidia kupata hifadhi na kuweza kujitegemea no udhaifu?

Je, nilifanya kosa kukaa kimya mda wote Wa kuandikwa magazetini kwa kashafa isio na ukweli?
Je, pale Mpendazoe anapochafuliwa bila sababu za kimsingi na kutofanya chochote ni jambo la kijinga ama ni udhaifu?

Je, pale unapomuona mzazi anatumia mwanae Kama chanzo cha kupatia mtaji na kulikalia kimya ni udhaifu?
Je, pale unapoitwa police central Mara kwa Mara na kutii wito ni udhaifu?
Je, pale unaopoona bongo unatungwa dhidi yako nakutofanya chochote in ujinga?

Kwa dunia na elimu an exposure ya sasa ni ujinga Wa hali ya juu kumchukua MTU na kuishi nae kwa mzazi wako huku ukijua a in a ya MTU unaie deal nae.

Mpaka hapo kuna deformation nyingi zilizofanyika bila kuchukuliwa hatua yoyote. Kusimamia misimamo ya kutotoa mimba ni jambo la muhimu Sana katika nchi hii.

Ninaliomba jeshi la polisi pale nitakopofika kesho Central Police kwa wito wao pia wachukua hatua ya kuchunguza allegations za utoaji mimba na makosa mengine. Kisingizio cha kusema kuwa Penal code/ criminal law is not retrospective inabidi iwekwe pembeni maana utoaji Wa ushahidi tayari no being retrospective.

Kesho SAA tatu Niko central police kuhusu hili suala.

Na hata kutangaza nia bado
 
Hii kesi ata ikiendelea haitafika mbali..kwanza binti yuko upande wa mshtakiwa binti abaye ndo shahidi wa kwanza,kwa vyovyote vile lazima ataturn into a hostile witness.lakin kwa kuwa nchi yetu inanuka rushwa chochote kinaweza kutokea.
 
Hii mbona kawaida watoto siku hizi mitaji Hii haina tofauti na wazazi wanaodai mahari kubwa kwa binti zao. Binti mwenyewe unakuta bikra ilitoka akiwa LA Sita B, wewe ni boyfriend wa 36 bado baba anataka mahari milioni 7 mfyewwww
 
Back
Top Bottom