Farhan: Kila timu ibebe mzigo wake mwenyewe

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
21,838
38,729
"Kitu kimoja kuhusu mpira wa miguu hakuna kinachodondoka kutoka angani, wakati wanaanza project yao wengi hawakuamini watafika popote, ila Wahuni walifahamu wanachokiandaa kifupi The Premier League and Africa wasnt ready for this show.

Zilianza kelele za Bahasha zikapita na kuondoka, zikaja kelele za kununua mechi zikapita na kuondoka, zimekuja kelele za Udhamini (HAIER) nazo zitapita na kuondoka na kinachosalia kwao ni UBORA.

IHEFU ni timu ya nne kwenye Ligi Kuu Msimu huu kuchukua mabao 5, anaungana na KMC, JKT na Simba! Hakuna uchawi unazungumzia ubora tu! Stephen Aziz Ki anaweza kukifanya alichokifanya leo hata kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, ni ubora tu! Pacome anaweza kukifanya alichofanya leo hata mbele ya Belouzdad mabingwa wa Algeria.

Tiba pekee kwa timu za Ligi Kuu zinazoteswa na huu ubora wa Yanga ni kukaa chini na kuona wapi wanapatia, wamebeba ubingwa wa Ligi mara mbili, wamecheza fainali ya CAF wakifungwa mmoja na kushinda mmoja, wapo Robo fainali Afrika hivi sasa, hii yote ni uchawi? Hapana ni FOOTBALL.

Kama kazi iliyomshinda Bingwa wa Algeria ataiweza Ihefu? Shughuli iliyomshinda TP Mazembe ataiweza Namungo? Sasa hivi wapo kwenye ubora wao tena wa ajabu mno! Bahati mbaya sana Washindani wao bado hawajaisaka tiba ila wanahangaika na Panadol kupooza maumivu sio kutibu kabisa ugonjwa.

Sio rahisi popote duniani anaondoka Kocha Mkuu, anaondoka Striker wao tegemeo, anaondoka Kiungo wako wa maana na Mabeki wawili wa Kimataifa halafu ukareplicate ubora ule ule kama hakuna kilichotokea! PUT SOME RESPECT TO Wahuni.

Wahuni Mean Business! Kila timu inapokutana na Yanga ibebe mzigo wake mwenyewe wala asitokee mwingine kuwategea wenzake.
 
Waacheni waendelee kujificha kama mbuni.

Yanga inaendela kutoa burudani tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom