Fao la kujitoa NSSF

Wafanyakazi wote waandamane wapinge hiyo sheria kandamizi! tusitegemee serikali dhaifu wala bunge la wapenda posho kutupigania.

Sawa kabisa kamanda. Tena tusiwaamini hata wandishi wa habari kwani kunataarifa kuwa wakati wa mchakato wa kuandaa ile sheria kandamizi kwa wananchi wakawaida, NSSF iliandaa semina ya uongo na kweli ya wahariri chini ya mwamvuri wa Editors Forum na walilipwa laki nane nane wote. Usishangae kuona mpaka hivi sasa hiyo ishu haipewi kipaumbele tena kwenye vyombo vya habari. Nawataja NSSF kwasababu ile siyo penshion fund bali ni social security fund. Penshion fund ndio unatakiwa pesa zako uzipate uzeeni na ndio maana inaitwa penshion ila social security fund inatakiwa ukupe maisha wakati wowote na hivyo basi, kujitoa uanachama ni sehemu ya maisha hayo. Kuondoa mafao ya kujitoa NSSF ni ushenzi wa maksudi uliofanywa kwa kushirikisha wadau wote ambao wangeweza kupiga kelele za kutetea wananchi wanaoonewa. NSSF wenyewe walijua walichokuwa wanakifanya ila sina uhakika kama hawa wenzetu wanaojiita editors walijua ni kwanini tunawapa zile pesa. Hivi sasa wamenyamaza kwani na wao ni sehemu ya tatizo. Pesa zetu siyo zakutusaidia sisi tena bali ni za kujengea vyuo ili serikali ya CCM izidi kusifiwa huku kijana Mtanzania akilazimika kusubiri mpaka miaka 55 ndio apate nyumba.
 
Hilo lije kuwa swali la Dr. Slaa kwenye kampeni kuwa atahakikisha FAO la kujitoa analirudisha maana tusije tukawachagua chadema nao wakaja na uzi huo huo
 
Back
Top Bottom