FAO la Kujitoa na Uchaguzi 2020

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,931
3,227
Serikali kupitia SSRA wanataka kulazimisha na kudhulumu haki za wafanyakazi. SSRA na Serikali ya CHAMA CHA MAPINDUZI chini ya JPM (aka mtetezi wa wanyonge) wanataka kusitisha FAO la Kujitoa.

Kumbuka 90% ya wafanyakazi ni masikini na hawana nyumba za kuishi....SSRA wameshindwa kusaidia wafanyakazi ambao ni wanachama wa PPF Na NSSF kupata mikopo ili wanunue nyumba nafuu NHC au WHC au wanunue viwanja wajenge....


NSSF wanasema wanatoa mikopo, ila hii ni hila tu maana Masharti ya mkopo ni magumu sana na NSSF wanataka masharti magumu kama dhamana za benki.

Kama mtu ana akima kama millioni 20, kwa nini akima yake isiwe dhamana na apate mkopo kama millioni kumi, ili mtu anunue kiwanja na mtu akajenga?

Masharti eti mtu umeachishwa kazi au mkataba umeisha ukiwa na miaka 35..utakaaje ungoje mpaka miaka 55 ustaafu...Kodi ya nyumba nani atalipa?

Afya duni?

Hata hao wachache watakaostaafu na miaka 60, je ataishi hapo miaka 5? akifa mke na watoto watapewa hiyo Pension? NOOOOO

Rais wetu ni msema kweli (mpenzi wa Mungu) na mtetezi wa wanyonge..Je uchaguzi wa 2020, atawaambia nini watanzania kwenye hii dhuluma?

Kila siku tunasikia ufisadi NSSF, mara trillions serikali inadaiwa, mara posho za wafanyakazi nssf billion 10.... a lot....

Ila mwanachama wa PPF au NSSF kupata mkopo walau nusu ya amana, ni dhambi?


Hali halisi mtaani ni kilio tu maana, wafanyakazi wana hasira..

TUCTA, Twico, wote ni hewa, wako kimya
 
Serikali haina hela..inatafuta vyanzo vya mapato...hela zenu za nssf/ppf ni chanzo kimojawapo cha mapato ya serikali hii.
Sidhani kama Juma Ponda Mali anajali maisha yenu nyie akina yakhe.
 
Tutaelewana tu 2020 nadhan atapata kura za policcm
Ndio makosa mnayoyafanya kila uchaguzi hayo,mnashindwa kujua wananchi wanataka kusikia nini
Wenye ajira nchi hii hawazidi asilimia 15,ukiwaleza wapiga kura huko mbwinde kuhusu fao la kujitoa hawatakuelewa
 
Huu ni wakati wa kuamka na kutolazimishwa kujiunga na mifuko hii pamoja na vyama vya wafanyakazi!!!!
 
PPF kulipwa mpaka miaka miaka 55 hata ukitoka leo utazikodolea macho tu ndio nchi yetu tufanyeje!
 
Kitu pekee atakachokwambia mwanasiasa cha ukweli ni JINA lake tu, ili usisahau kwenye karatasi ya kura.;)
 
Wafanyakazi wengi wataumia kwa kubaniwa fao la kijitoa na serikali itafaidika sana na pesa ya bure toka mifukoni kwa mfanyakazi watakaokufa kabla ya kufikisha umri wa kustaafu, ndani ya kipindi cha miaka minne ijayo wafanyakazi wanatakiwa kupiga propaganda ya hali ya juu kwa familia na ndugu zao kuwa hawataweza kuwasaidia hapo baadae kwani jamaa wamezulumu haki za mfanyakazi
 
Mgaya anawania tena Uongozi TUCTA

Hafai huyoo

Kibaraka

FAO LA KUJITOA...

Viongozi wa Matawi, fukuzeni huyo Mgaya....akampumzike agombee ubunge kwa ticketi ya CCM
 
Mdau kwa hili la fao la kujitoa nakuunga mkono mia kwa mia. Ikumbukwe fao hili ni malimbikizo ya makato yako kwa kazi uliyofanya (kama nakosea nisahihishwe). Hakuna sababu ya kumnyima mtu fao lake kes kuwa ni jasho lake.
 
Mkutano Mkuu wa Wafanyakazi, TUCTA leo

Waziri Mkuu kahutubia

Mgaya kasoma risala ila kasahau ishue muhimu FAO la Kujitoa..

Huyu Jamaa amezeeka, hafai pale TUCTA
 
Mdau kwa hili la fao la kujitoa nakuunga mkono mia kwa mia. Ikumbukwe fao hili ni malimbikizo ya makato yako kwa kazi uliyofanya (kama nakosea nisahihishwe). Hakuna sababu ya kumnyima mtu fao lake kes kuwa ni jasho lake.
Hilo jina "FAO la Kujitoa" ndio nuksi. Labda iwe mwanachama kurwheshewa muchango yake akiachishwa kazi kabla ya muda wa kustaafu. Wenyewe wanasema hakuna kitu kiitwacho FAO la kujitoa kwa kuwa inakuwa inakinzana na dhana halisi ya hifadhi ya jamii.
Kipindi kama hicho hizo fedha zingewasaidia wanachama kujiajili na kuanza maisha mapya. Ingekuwa ni kazi ya mifuko ya hifadhi kuwashauri namna ya kuniwekea akiba ya uzeeni wao binafsi
Kaazi kweli kweli
 
Hilo jina "FAO la Kujitoa" ndio nuksi. Labda iwe mwanachama kurwheshewa muchango yake akiachishwa kazi kabla ya muda wa kustaafu. Wenyewe wanasema hakuna kitu kiitwacho FAO la kujitoa kwa kuwa inakuwa inakinzana na dhana halisi ya hifadhi ya jamii.
Kipindi kama hicho hizo fedha zingewasaidia wanachama kujiajili na kuanza maisha mapya. Ingekuwa ni kazi ya mifuko ya hifadhi kuwashauri namna ya kuniwekea akiba ya uzeeni wao binafsi
Kaazi kweli kweli

Hii mifuko ilianzishwa kama Mifuko ya akiba (PPF na NSSF)...wao wakabadilisha wakafanya mifuko ya hifdhi....Hili jambo walifanya kimya kimya bila kushirikisha wafanyakazi. Hivyo, kwa sababu walibadilisha, inawezekana kurudisha iwe mifuko ya akiba pia...So sheria inatungwa ili iwe msaada kwa jamii, sio kutunga sheria za kukandamiza ustawi wa jamii.

Kwa mazingira ya sasa, FAO La KUJITOA lazima liendelee kuwepo.... Hii Serikali imekuja na hoja nyepesi sana

Hoja za wafanyakazi ni nzito na LAZIMA FAO LA KUJITOA liendelee maana wafanyakazi wana haki na pesa zao na wanahaki ya kupanga hatima yao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom