Fanya yafuatayo ukigundua kuna majambazi nje ya Nyumba yako

Unless wanajua una mzigo na wana uhakika hujaupeleka benki; Jambazi haibi TV; Laptop na Smartphone; hao ni vibaka tu na huwa na mapanga, mashoka, visu na nondo.
 
Ukifunga mlango hasa wa kitasa usiache ufunguo mlangoni. Huwa unatikiswa na kuanguka chni kisha unavutwa kwa nje na waya ikiwa mlango wako unaacha kamwanya kwa chini. Hapo utafunguliwa na wataingia kama kwao. Hoi ni kwa vibaka. Hutokea hasa kwenye nyumba ambazo hazina geti kabla ya mlango wa mbao.
 
Tafadhali chukua dakika chache kupitia maoni haya


1. Majambazi kwa kawaida huanzisha mashambulizi yao kupitia mlango wa nyuma (kawaida milango ya jikoni) kwa sababu kwa kawaida hawaonekani. Weka milango mizuri jikoni kwako. Tumia "chuma cha kukatisha" ama "Kizuiawezi" nyuma ya milango ndani ya nyumba. Kama una funguo "Kizuiawezi," kamwe usiache ndani ya kufuli. Kama inawezekana, tumia kufuli kwa kuongeza. lengo ni kuleta ugumu kadiri inavyowezekana kwa wezi kuingia ndani ya nyumba na kukuongezea wewe muda wa kuwaita watu kwa msaada.

2. Unaposikia mtu anavunja mlango wako, kama huna unahakika kabisa vitendo vyako vitazuia kuingia ndani ya nyumba, usijaribu kuwa shujaa kwa kusukuma nyuma ya mlango (Wanaweza kukupiga risasi kupitia mlangoni), au kuweka vitu vizito kama jokofu au makochi (Wanapatwa na hasira zaidi na kama watafanikiwa kuingia ndani wanaweza kufanya ukatili vibaya mno).

3. Kama unalala bila nguo au na nguo kidogo, Vaa haraka mara tu uwasikiapo. Kwa wanawake hasa, usijaribu kubaki na nguo za kulalia. Vaa suruali na blauzi isiyovutia.

4. Iwapo umepiga simu kwa mtu kwa msaada, weka simu mbali nawe kama vile huitaki ili usijulikane kuwa umepiga simu.

5. Angalia sehemu ya kukatia umeme kwenye nyumba yako kisha zima umeme iwe giza nyumba yote (hii itawachanganya na kusababisha wakimbie.

6. Kama una bunduki, imesajiliwa au la, itumie lakini tu kama una unauhakika kuwa unaweza kuwasababishia madhara. Huu siyo muda wa kupiga risasi juu kuwatisha! Mauaji ya mvamizi katika eneo la nyumba yako wakati wa kujilinda mwenyewe na mali zako ni halali kisheria upande wa utetezi. Pia hata ukitumia silaha nyingine yoyoyte kama vile kisu.

7. Wakati Majambazi wamefanikiwa kuingia wape chochote wakitakacho. Usifiche chochote. Usijaribu kuwa Jasiri wala kujadiliana nao.

8. Usiwatazame moja kwa moja (au usiwafanye wajue kuwa unafanya hivyo). Kama unamfahamu yeyote kati yao usioneshe dalili zozote za kumtambua na wala usitaje jina lake. Hata hivyo kariri maumbile yoyote unaweza kusaidia na kutambulisha katika uchunguzi.

9.Wakati hatimaye wanaondoka katika nyumba yako usiwafukuzie ..

10. Kuwa mlinzi wa jirani yako kama utasikia uvunjaji katika nyumba zao, piga simu polisi kwa msaada.

11. Wakati Majambazi yanaingia kwenye eneo la nyumba yako, usiwashe taa yoyote katika chumba chako. Washa taa za nje lakini zima taa za ndani zote ili majambzi/wezi wasiweze kukuona.

Mbwa Walinzi wanakubalika sana majumbani kwa ajili ya kutoa taarifa mara kitu kigeni cha hatari kinapokuwa kwenye eneo.

Mwenye mawazo ya ziada anaweza kuongezea
Kwa kuongezea tu ukilala na kahaba inabidi ukeshe kama bundi!maana utajikuta unapata tabu saaana!
 
Back
Top Bottom