Fanta na SNAKS ya clouds TV imenikumbusha MWL.CROSPEL 1990

conductor

JF-Expert Member
May 29, 2013
718
570
Kipindi cha CLOUD TV (Fanta na snacks) kimenikumbusha Mwl.Crospel 1990.

Umri umesogea sasa, 41 si Haba, mwaka 1990 nilitimiza kile kigezo kikubwa sana cha kunyoosha mkono ushike sikio ndo uanze darasa la kwanza, ulipokuwa ukipitia KIUNZI hicho, hatua ya pili mnaanza kuandika kwa vijichi vyenye ncha kiasi ili muanze kuandika AEIOU/12345.

Kabla ya kuanza shule,nilikuwa mchungaji wa NG'OMBE maarufu kwani natokea koo ya wafugaji na wawindaji, hapa nilipata training nzuri ya kuishi na wanyama, kama NG'OMBE,Mbwa,kondoo (Kama movie ya TAIZAN) na nilifundishwa na wanyama wenyewe,kwani masaa mengi nilikuwa polini mvua,jua, ugonvi wa wafugaji na wakulima nilipambana navyo katika umri mdogo sana wa miaka 4 (WANYAMA WANA UPENDO SANA KULIKO BINADAMU),nilipofikisha miaka 7 ndo nikabadirishwa kitengo ,Nikaanza Kipaimara, na huko unapimwa kwa Sara na nidham yakutosha karibia mwaka mzima, (hapa father KAGURUMA/KAPILIPIL kutoka RUTABO na makatekista kadhaa wanakupa baraka zao na cheti.(mtihani wao ni kukariri Sara na wakati mwingine unatumikia misa kama unaonyesha uwezo mzuri (nako huko nikapita).

JANUARY 1990 msela nikapelekwa kuanza ngwe ya s/MSINGI (RUZINGA S/M) maisha mapya kabisa afu magumu sana kwani baridi,usafi wa nguo, kukutana na sura mpya nayo ilikuwa kipengele kingine cha maisha.

Maisha ya KIDUMU,MFAGIO,na Vijiti vya kuesabu na kuandika kwenye udongo ni kazi yangu sasa. Ubongo ulianza kuwa umegoma kuyapokea Maisha hayo licha ya miaka 8 kwani huko porini matunda na kuchimba viazi vya watu kula ilikuwa kawaida ,au kwenda mkachoma mahindi porin kuni zipo,kiberit unaiba njiti moja au Ile kanuni ya kupikicha Kijiti kupata moto niliijua mapema,Ila nilikuja kusoma somo hilo nikiwa form one (evolution of Man).

WAKATI tumeanza na kufuzu kuandika chini, mwezi wa sita wa darasa la Kwanza unaingia darasa rasmi kuanza kukalia dawati, na kuandika kwenye Daftar (madaftar hayo yalikuwa ya aina mbili, moja lina draft kwa ajili ya HESABU,na jingine la mwandiko lina mistar mikubwa na midogo) .Miezi SITA ya kwanza nilisoma ila si Kwa mapenzi ,nilisaidia tu pengine na zile tabia za kifugaji (ushap),kipindi cha kuanza kutumia daftar na pencil serikal ilikuwa inatoa madaftar bure na kalamu, siku ya kufungua shule,.

Maisha rasmi yakaanza,mchakamchaka wewe asubuhi mnakimbia karibu vijiji 5, ukiwa peku, nayo nikajifunza, kuchota maji nayo nikajifunza, kuibiwa madaftar na mihogo/mahindi nayo nikajifunza.

Siku ya KWANZA TU tumingia darasani ilikuwa juma nne nivaa nguo nzur ina malinda kama brauzi hivi nayenyewe nilipewa na dada yangu kwani ilikuwa nyeupe msela nikavaa bila kujari ubora ilimradi nyeupe na kaptura kubwa imepitishwa nguo kama mkanda (rastika) ili isivuke basi tumeingia darasani tunasubiri Mwalimu aingie ,alipofika darasani tukamslimia "SHIKAMOO MWAAAAALIMU) aliitwa Mwalimu CROSPEL jina la pili silikumbuki, wakati anaingia alikuja na bakuri limejaa mahindi yaliyokaangwa (iliitwa bisi) ,akakaa mbele HUKU anatafuna mahindi, pemben ana fimbo,chaki, madaftar mengi na kitabu kikubwa cha rangi mbili.

Nilipoingia darasana kwa mara ya kwanza nilichagua dawati la mbele ila sijuh kwanin ilitokea hivyo (sikuwa mshamba kwani wanafunzi wengi tulikuwa tunachunga pamoja NG'OMBE,na kuchota maji maeneo mengi pamoja,)na tumeishazpeana huko kaz za nje, mwalim CROSPEL akaweka maneno ubaoni ili tuyaandike kwenye madaftar , badae anaendelea kula bisi yake alafu akisahihisha madaftar ya darasa la pili.

Ndo ukafika muda wa kupita kukagua tunacho andika Mimi nilikuwa wa kwanza kabisa mstari wa Kati kati Ila mbela kabisa, msela kuandika kwenye Daftar ilikuwa NGUMU balaa hivyo nilifuta na kukosea maneno.alipopita ana karamu nyekundu akaona nilivyoandika UPUPU alimipiga kofi la shavuni, nilisikia masikio yameziba na macho hayaoni kabisa watoto wenzangu wakastuka wakajua basi hiyo ndo darasa la Kwanza rasmi lazma upitie upepo huo, yale madarasa madirisha yalikuwa wazi , dogo mmoja aliitwa RASHIDI nadhan alijistukia mapema huko back bencher alipitia dirishan akatokomea msituni na daftari akaliacha hapo ndo hakuonekana tena shuleni na akaacha shule. Wengine waliendelea Kula makofi wengine neno "VEMA " sijuhi kama bado neno hili linatumika kama appreciation ya kufanya vizuri.

Nilipotoka hapo akiri ilikaa sawa na bora zaidi mpaka nikawa monitor mpaka nilipo ama kwenda CANADA alipokuwa baba mdogo kuanza maisha mapya nikiwa darasa la tatu. Sikuwaiga kurudi shuleni hapo ila nitakwenda kusalimia siku moja shule yangu ya 1990. niulizie marafiki zangu wakina Lea ,Mwijage, Kamugisha na Adelina alikuwa mfupi sana ila ana katako flani hivi, pia kujua mwl Huyo CROSPEL yuko wapi nimshukuru kunifungulia dunia leo eti msela naendesha ndiga kali na mke mkali ,watoto kumbe nilkuwa mfugaji na boya/ndina. Vijana wa Leo msikate tamaa kila dhama na tabia zake..hata hivyo Kofi lile lilinifundisha kujiamin nimeongoza MIGOMO kadhaa vyuoni nilipoona mambo sio kwa walim wasio serious. ENFIDE ET CARITATE.

FB_IMG_1676801299970.jpg
FB_IMG_1676712634217.jpg
 
Back
Top Bottom