Familia yamng'ang'ania mfanyabiashara aliyeua ndugu yao kikatili

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Familia ya marehemu ,Steven Jimmy(45)aliyeuawa kikatili kwa madai ya kuiba Pambu ya maji, imetishia kumwona rais wa nchi,Samia Suluhu hasan iwapo mfanyabiashara, Pendael Mollel anayedaiwa kutekeleza mauaji ya ndugu yao ataachiwa kutokana na taarifa za kuwepo mchezo mchafu wa kujinasua.

Mollel ambaye amezua gunzo kila kona katika jiji la Arusha na viunga vyake,juu ya tukio hilo,anadaiwa kutekeleza mauaji hayo yeye na mdogo wake,mlinzi wake na watu wengine ambao walijifanya ni askari polisi wakati walipokuwa wakimteka marehemu wakiwa na gari ndogo inayodaiwa ni mali ya mfanyabiashara huyo.

Akiongea na gazeti hili nyumbani kwa marehemu,kaka wa marehemu Joseph Jimmy,alisema kuwa tukio hilo limemsikitisha sana kwa sababu ndugu yao hakuwa na tabia ya udokozi na amewaachia mzigo mkubwa wa kulea familia yake ya watoto watano na mke mwenye ujauzito wa miezi tisa.

"Tumesikia kuna mpango anaoendelea ili aachiwe sisi kama familia hatutakubali tumejipanga kumwona rais Samia Suluhu ,hata kama sisi ni masikini hatutakubali uonevu wa aina hii"alisema Jimmy

Naye mke wa marehemu ,Joyce Ndanasila ambaye ameachwa akiwa na ujauzito wa miezi tisa na watoto watano akiwemo mwenye ulemavu,akiongea kwa uchungu alisema marehemu alikuwa nguzo kuu ya familia hiyo na haelewi hao watoto atawalea vipi.

Ameiomba serikali kuingilia kati kwa wahusika waliojichukulia sheria mkononi ili sheria ichukue mkondo wake kwani anaamini marehemu mumewe hakuwa na tabia ya wizi hata kidogo

Naye ndugu mwingine Ernest Julias au William, alisema uchunguzi wa awali wa kitabibu uliofanywa na Madaktari wa Hospital ya Muriet Jijini Arusha umeonyesha kuwa mwili wa marehemu Stephen Jimmy{43} aliyeuawa na Mfanyabiashara Maarufu wa Madini ya Tanzanite na wenzake alifariki baada ya kipigo kikali na kuchomwa kitu chenye ncha kali kisogoni.

Mfanyabiashara wa Tanzanite Jijini Arusha,Pendael Mollel na wenzake watatu walikamatwa April 19 na Jeshi la Polisi mara tu baada ya tukio hilo kutokea Aprill 18 mwaka huu huku taarifa za kamanda wa polisi mkoani haoa Justine Mesejo akieleza kuwa atalitolea ufafanuzi mara baada ya uchunguzi kukamikika.

Julias alisema ameshuhudia mwili wa marehemu ukiwa na majeraha makubwa maeneo mbalimbali huku jereha kubwa ni kisogoni linaloonekana kupigwa na kitu chenye ncha kali kwakuwa jeraha hilo bado linachuruzika damu mbichi hadi sasa.

Aidha alidai kuwa mwili wa marehemu unatarajiwa kuzikwa Aprill 26 mwaka huu siku ya jumanne katika kitongoji cha ilkiushin Kata olturumet wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.

Julias ameliomba jeshi la Polisi Mkoani hapa kuhakikisha wale wote waliohusika katika kumteka na kumpiga marehemu wanachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria kwani hakuna mtu aliyeko juu ya sheria hata kama ana uwezo mkubwa wa kifedha.

Kwa upande wake mwajiri wa marehemu ,Mohamed Ahamed,alitahadhalisha jeshi la polisi kutopindisha haki katika tukio hilo kwani anaamini marehemu ambaye alikuwa akifanyakazi ya ulinzi nyumbani kwake kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu hakuwahi kumwibia hata kijiko.

"Siku ya tukio baada ya kumuua marehemu,Pendael na wenzake walimpeleka kituo cha polisi Muriet na kuandikisha kwamba ni mwizi na ameuawa na wananchi wenye hasira kali jambo ambali sio kweli na mimi ndio nimefanya jitihada kubwa za kuwasiliana na viongozi mbalimbali juu ya tukio hilo la kinyama na kupelekea kukamatwa kwa wahusika"alisema Ahmed

Kukamatwa kwa Mfanyabiashara huyo na wenzake watatu kulithibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Justin Masejo na kueleza kuwa mtuhumiwa alikamatwa mjini Moshi alikokimbilia kujificha bàada ya kufanya mauaji hayo.

Masejo alisema kuwa watuhumiwa wote wako rumande katika kituo kikuu cha Polisi Arusha kwa ajili ya mahojiano na kuna baadhi ya watuhumiwa wengine wanasakwa na polisi ili kuunganishwa katika tukio hilo.

Alisema kwa sasa hawezi kusema chochote zaidi ya kujua kuwa watuhumiwa wako rumande ila baada ya siku moja ama mbili wahusika wakikamilisha kutoa maelezo na wengine kukamatwa ataweza kutoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya tukio hilo zima.

‘’Ninachoweza kusema kwa sasa ni kukiri kuwa mfanyabiashara wa Madini ya Tanzanite Pendael Mollel tumemkamata Moshi kwa tuhuma za mauaji na wenzake watatu wamekamatwa Arusha na wako kwa ofisi ya Kamanda wa Upelelezi wa Mkoa wa Arusha{RCO}’’ alisema Kamanda Masejo

Tukio hilo la Mauaji lilitokea eneo la Burka ndani ya Jiji la Arusha karibu na uwanja wa ndege wa Arusha aprill 19 mwaka huu majira ya saa 1.45 usiku ambapo Mollel akiwa na wapambe wake na mdogop wake walikwenda kumchukua marehemu katika nyumba ya jirani aliyokuwa akilinda inayomilikiwa na Mahamudu Mohamed.

Vyanzo vya habari vilidai kuwa kabla ya kutekwa kwa marehemu na Mollel na wapambe wake jioni ya siku hiyo tajiri huyo wa Madini ya Tanzanite aliwasiliana na Mohamed mwajiri wa mlinzi huyo na kudai kuwa mlinzi wake ameiba Pampu ya kusukuma maji yenye thamani ya shilingi 180,000 siku ya Aprill 18 Mwaka huu hatua ambayo ilipingwa na Mohamed na kumweleza kuwa afanye vizuri uchunguzi wake.

Habari zilidai kuwa mwajiri wa marehemu aliwasiliana na mafundi walioko eneo la nyumba yake na kueleza malalamiko ya jirani lakini mafundi walimhakikishia kuwa mlinzi siku hiyo ya tukio hakuweza kutoka nje bàada ya kuingia kazini na walikuwa wote lakini alipoelezwa Mollel hakukubaliana na kauli hiyo na kudai kuwa polisi wacha wafanya kazi yao kwani mlinzi wake ni mwizi.

Vyanzo vilidai kuwa Mollel akiwa na wapambe na watu wengine walimchukua marehemu na kumwingiza katika nyumba ya tajiri huyo na kuanza kumpa kichapo kilichokwenda sambamba na kupigwa na marungu na baada ya muda mfupi marehemu alipoteza maisha.

Habari zilidai kuwa baada ya kichapo hicho cha Mollel kwa kushirikiana na wapambe wake tajiri wa Madini ya Tanzanite aliamuru marehemu kupelekwa polisi kwa Mrombo na kuwaeleza polisi kuwa wananchi wenye hasira wamemuua hatua ambayo polisi waligoma kupokea maiti na kuwaelekeza kupeleka chumba cha maiti katika hospital ya Muriet ambapo maiti iko hadi sasa ikisubiri kufanyiwa uchunguzi.

Picha ya kwanza ni marehemu na picha ya pili ni mfanyabiashara anayetuhumiwa kuua
20220423_215123.jpg
IMG-20220423-WA0168.jpg
 
unaua Arusha alafu unakimbilia Moshi ambapo polisi wanakufuata hata na bajaji!!!
 
watu wa porini kuua kwao huona ni kawaida tuuu..
kama walimkata punda miguu yote na kumbaka ili wapate utajiri watashindwa kuua kweli??!!!
ukiishi kule porini utajua maisha ya kule sio lelemama..kaa kiboya unazikiwa humohumo mgodini watu wakiamini kafara ya damu korongo litatoboka
 
Tumerudi kule kule tulipotoka, kwenye serikali ya nakupiga halafu nakulipa.Poleni familia.
 
Hii taarifa mwanzo wa andiko imesema marehemu ana miaka 45 ila kati kati ikasema ana miaka 43.

40+ ana mke ana mimba ya miezi tisa, watoto 5.

Kazi ni ulinzi.

Bwana anafanya njia?
 
Hii taarifa mwanzo wa andiko imesema marehemu ana miaka 45 ila kati kati ikasema ana miaka 43.

40+ ana mke ana mimba ya miezi tisa, watoto 5.

Kazi ni ulinzi.

Bwana anafanya njia?
Sasa miaka 45 asizae?
 
hesabu ni ngumu sana unauwa mtu kwajili ya 180k alafu utatoa 5m kupindisha kesi kweli masai ni masai tu ....ova
 
Back
Top Bottom