Falsafa na Maisha 101: Ni muhimu sana kuwafunza watoto wetu falsafa muhimu za maisha, la sivyo maisha yao duniani yatakuwa magumu sana

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,603
Nimekuwa nikijaribu sana kuwasoma wanafalsafa wa miaka ya nyuma. Na kwasasa nikijiangalia kuna mengi sana yamebadilika kwenye maisha yangu, hususani kwenye maadili na kuwa na self control ya maisha yangu.

Haya ni moja wapo ya mambo ambayo falsafa inazidi kunifundisha

1. Usiwe mtu wa kulalamika na kulaumu kwa mambo usiyeweza kuyabadili. Jamii ya sasa, imezoea kuwa na malalamiko kiasi kwamba malalamiko yamejeuka kuwa ni tabia ya kudumu, kwa maana ya kwamba mtu aliyezoea kulalamika na kulaumu, usitegemee hata siku moja atakuja na proposition ya solution yenye maana, zaidi zaidi walalamishi huishia kulalamikia mambo ambayo wao wenyewe hawajui ni kwanini wanalalamikia. Yaani mtu anafika kipindi akiona jambo ni positive lazima yeye aangalie pakulalamika na pakutolea lawama ni wapi.

Hii kitu ina athari kubwa sana kwenye jamii na maisha ya watu. Na inawezekana kabisa ni kichocheo kikubwa cha watu kuendelea kuwa masikini.

Kipindi cha Magu, wafanyabiashara walikuwa wanaishi kama mashetani ila utashangaa ni nadra sana kusikia wakilalamika, always walikuwa positive wanaangalia fursa za kuponyoka.

Ila angalia masikini pangu pakavu tia mchuzi, always ni watu wa kulalamika pasipo kuwa na hoja. Unakuta wazazi wanalalamika kwamba eti shule haina tundu la choo, wakati huo mda wangeutumia kutatua tatizo.

Mbaya zaidi miaka ya hivi karibuni hata kwenye mitandao ya kijamii hususani JF comments na michango ya wadau imejeuka ni lawama na malalamiko, kiasi kwamba kwa sisi ambao tumeshatoka huo ulimwengu wa malalamiko na lawama inatuwia vigumu sana.

Hilo ni jambo kubwa sana ambalo mimi nataka kumrithisha mwanangu... 'Acha kuwa mtu wa malalamiko na lawama'

2. Usiwe mtu wa kupenda kutafuta raha na starehe za mda mfupi.

Kutokujua hili jambo kumewafanya watu wengi ku base starehe zao kwenye vitu kama tiktok, sex, alcohol etc..

Sisemi kwamba ni mbaya, ila kama kuna mtu kwa siku anatumia masaa 3 mpaka 4 kuangalia tiktok, instagram, wasap... unaweza kunielewa namaanisha nini hapo... yaani kutumia 15% ya masaa 24 just kwa starehe ya haraka, kuangalia vi clip na kujichekesha, we ipime kama ni kitu kitaleta mabadiliko.

Badala yake wana falsafa wanatuambia kwamba, uwekeze muda wako kufanya shughuli ambazo hazikuletei furaha pale pale unapozifanya.

Mfano mimi nilivokuwa mdogo nilikuwa mchoraji 'artist' na ilikuwa kila navotaka kuanza kuchora nilikuwa nateseka sana, maana ilibidi kwanza nianze ku set scale na kuchora visanduku nk na ilikuwa ikinisumbua, ilikuwa inanipa pain sana, kwasababu upande mmoja natamani nichore picha nzuri ila upande mwingine ile painful process ilikuwa inaniumiza sana.

Ila sasa pale ninapomaliza kuchora huwa ilikuwa napata satisfaction ambayo siwezi kuielezea... yaani unamuonesha mtu picha anakuambia 'Huyu ni Nyerere umemchora?'.... Yaani basi nilikuwa nafarijika sana coz, nimetumia muda ku create value halafu nimeongeza ujuzi. Na huo ujuzi to some of us, ndo unakuja kukupa utajiri na maisha (Angalia hiyo perspective vizuri)

Ingelikuwa Mark Zuckerbarg yupo busy na starehe za haraka kama kucheza game pindi alivokuwa mtoto badala la ku solve maths problems na kuandika coding algorithms asingekuwa pale alipokuwepo.... (Ifikirie in that way)

Na hii ndo namna mimi naamini utamlea mwanao aje kuwa independent thinker... otherwise maisha ya kizazi kijacho yatakuwa magumu sana, regardless mzazi umepambana umemuachia mwanao urithi wa mabilioni, kama atafeli kwenye falsafa za maisha kama hizo hapo juu na nyinginezo ambazo zijazisema, maisha yake yatakuwa magumu duniani... Kizazi chako hakitakuwa na sustainability.

Ni somo pana sana hili ... ila madhara ya jamii kuishi kinyume na misingi ya falsafa za maisha yana matokeo mengi mnoo ambayo ni hasi, saa nyingine pia baadhi ya magonjwa, uraibu, crimes, etc etc
 
Wazazi washakasirika kuwapotosha watoto wao, wengi wanaona bora watoto wao wajikite kusoma vitabu vya dini visivyo wahusu (Quran na Biblia) ila si kusoma na kwenda shule. Waafrika tuna matatizo ya kiakili sana.
 
Back
Top Bottom