Faida ya mboga za majani kwa afya

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,554
Hakuna aina moja ya mboga za majani inayotosha kukupatia virutubisho vyote muhimu ili uweze kuimarisha afya yako.

Ni muhimu kutokutumia aina moja ya mboga kila siku kwa kuwa haiwezi kukupatia virutubisho vyote unavyohitaji, bali jitahidi kuchanganya au kubadili mara kwa mara ili uweze kunufaika vizuri.

Mboga za majani huwa na faida zifuatazo kwa afya-
  • Huwa na nyuzinyuzi zinazosaidia kuboresha mfumo wa chakula, kurahisisha choo na kutoa kinga dhidi ya saratani ya utumbo mkubwa
  • Aina nyingi za mboga za majani huwa na madini ya potassium ambayo husaidia kudhibiti shinikizo kubwa la damu na magonjwa ya moyo
  • Huwa na kipimo kidogo cha sukari (Low Glycemic Index) hivyo hufaa sana kwa watu wenye tatizo la ugonjwa wa kisukari
  • Kama ilivyo kwa makundi mengine ya chakula, mboga za majani hubeba virutubisho muhimu kwa afya yako kama vile vitamini A, vitamini C, asidi ya foliki, madini mbalimbali na viondoa sumu. Vyote hivi huhitajika mwilini ili kujenga afya.
Chanzo: WebMD
 
Mboga za majani zote ni nzuri kwa afya zetu, Ila ukienda hospitali wanasifia Sana spinach.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom