faida ya chama pinzani kuwa na mawaziri kimvuli

zamlock

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
3,840
657
wajameni na wachambuzi wa siasa tuelezeni faida ya chama kuwa na mawaziri kimvuli kwa sababu ni wengi tunahitaji kujua ni faidi kwa wale ambao hata awajui.
 
Wanapata nafasi ya kutoa budget mbadala na kuonesha tofauti ya mitizamo ya chama tawala na wapinzani katika kila wizara/sekta. Hii ni opportunity kwa kambi rasmi ya upinzani katika kuonesha wao kama chama pinzani wangefanyaje katika jambo fulani.

Pia huwa ni mzungumzaji mkuu wa wa wizara husika kwa kambi ya upinzani. Kwa hiyo wapinzani watakaa pamoja na kuunda budget mbadala/kuwa na kauli mbadala katika jambo fulani ambalo waziri husika wa serikali atalisemea vivyo hivyo na kambi ya upinzani hupewa nafasi kusemea jambo hilo kupitia msemaji rasmi wa kambi hiyo. Msemaji rasmi wa kambi ya upinzani ni rasmi na kutambuliwa na kanuni za bunge.

Kumbuka kuwa hii ni tofauti na kipindi cha maswali na majibu ambayo speaker au naibu speaker au mwenyekiti wa kikao husika cha bunge huongeza kikao hicho ambapo kila mbule mwenye kutaka kuchangia anapata nafasi kulingana na maamuzi ya speaker. katika hili speaker au naibu au mwenyekiti anaweza kulimiti idadi ya maswali.
 
Nsololi,
ufafanuzi wako umetulia..wanaJF wengi (singependa kuorodhesha) tungejifunza namna ya kurespond hoja kama alivyofanya mkuu hapo juu.
JF ingedhihirika kuwa jukwaa la great thinkers wa kweli
 
Back
Top Bottom