Faida na hasara za kuoa mwanamke msomi na mwenye kazi na kipato kizuri

Mi siamini katika kuwa msomi au asiye msomi wote ni wanawake,unaweza pata msomi akawa hana akili ya maisha,au akakusumbua kwa kujiona naye anaweza kutafuta pesa,na pia ukampata asiye msomi akawa hajatulia hata ukimuweka mama wa nyumbani ,chamsingi ni kuangalia mtizamo wa mwanamke na akili ya maisha,upendo heshima ni vitu vya msingi na c kuangalia usomi.
 
Cha msingi kuliko vyote ni je, mtaendana? Ni lazima pia mumwombe Mungu wakati mnatafuta wenzi wa maisha jamani. Umwombe Mungu akupe mke/mume mtakayeendana. Elimu ya darasani ni jambo dogo sana. Kwanza lazima tuelewe kwamba wanawake wengi (hapa nchini) wakeshakuwa na elimu kubwa wanaanza kuwa na nyodo. Wengine hata kama hajasoma, akifanya biashara akifanikiwa nae hivyo hivyo - nyodo tupu. Wanaume nao wako hivyo hivyo. Akishapata pesa anasahau alivyoteseka na mkewe walipoanza maisha. Anakuwa na vimada kila kona na kumdharau mkewe.

Kwa hiyo la msingi sio kisomo cha mke au mume. Mke anaweza kuwa hana kisomo cha darasa lakini akajiendeleza akawazidi wasomi wakubwa. Au anaweza akawa amesoma sana lakini maarifa ya maisha ni sifuri. Kwa hiyo, jambo pekee ambalo linapaswa kuwa ndio kipimo cha ndoa nzuri ni je, huyo mume na mke wanaelewana, wanapatana na kuheshimiana? Hivyo vitu vitatu vikishakuwepo ndoa inakuwa tamu. Kimoja tu kikikosekana ndoa inakuwa ndoano, tena inatia maisha doa.
 
  • Thanks
Reactions: 1gb
Kwa uzoefu wangu,nawashauri muoe wanawake wanaojishughurisha,ukioa gori kipa,ni shida tupu,
Wengine sasa hawataki labda akufungulie mwenyewe kitu cha kufanya yaani maisha haya kila mtu
anajichagulia aonacho kinampa amani na furaha
 
By nature all women are selfish! Don't expect any contribution from a woman after marriage out of her thing that is found between her two legs
Una mawazo mabaya sijapenda. Wewe umekitana na wanawake wangapi mpaka ukafikia hiyo conclusion??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom