Fahamu: Wafanya maamuzi serikalini husomea makabrasha vikaoni

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,238
103,907
Hello mwanaJF kila ninapopata nafasi nitakujuza mambo ya hovyo ambayo hufanyika serikalini na wengi wetu hatufahamu. Wengi tunafahamu zaidi kuhusu matokeo na sio chanzo.

Wengi wetu hudhani kwamba watumishi wa serikali ni watu makini sana na hufanya majukumu yao kwa ustadi na weledi. Acha kujidanganya. Huko serikali watu hao hawapo.

Je, unafahamu kwamba wengi wa wafanya maamuzi serikali huwa hawana muda wa kusoma nyaraka na makablasha, kuchambua na kuamua? Subiri nikueleze.

Hii inahusisha ngazi karibia zote, kuanzia vikao vya serikali za vijiji mpaka wizarani na idara zingine za serikali ikiwemo bunge la jamhuri.

Wafanya maamuzi hawa huwa wanakuta nyaraka na makabrasha hayo kwenye ukumbi wa kikao siku ya kufanya maamuzi. Tarehe ya kikao inaweza kutangazwa wiki moja kabla ya kikao lakini sio kwamba waheshimiwa watapatiwa nyaraka hizo ili wapate wasaa wa kuzichambua ili awe kwenye nafasi nzuri ya kuhoji na kushauri HAPANA. Bali ataenda kupitia na kuchambua humohumo ukumbini.

Hili hufanyika pia bungeni kuanzia kwenye vikao vya kamati mpaka vile mubashara. Wanasomea mule mule ukumbini na hivyo kujikuta wanahitaji zaidi msaada wa waandaaji ili kuzielewa hizo nyaraka.

Wafanya maamuzi hawa hujikuta wana uelewa mdogo sana juu ya jambo wanalohitaji kulipitisha. Na hivyo kujikuta wanapitisha kama ilivyokuja.

Hii ndio sababu hasa ya sheria za hovyo kupitishwa kwa sababu watunga sheria hawana muda wa kuchambua miswada.

Nazungumzia kinachofanyika. Lakini kinachotakiwa kufanyika kwa mujibu wa taratibu ni tofauti. Taratibu zinaelekeza nyaraka kusambazwa kwa wakati ili mtoa maamuzi apate muda wa kutosha kuchambua.

Ndio maana wabunge wachache wanaopata muda wa kusoma na kuchambua huonekana vipanga. Ni kwa sababu 90% ni vilaza huku baadhi wakijua tu kusoma na kuandika.

Huku serikali za Halmashauri hali ni mbaya zaidi. Waheshimiwa madiwani hata ajenda tu za kikao huwa wanazikuta ukumbini. Kila kilichomo wanapitisha kama kilivyokuja. Mpaka itokee shida ikajulikana baada ya kuleta athari ndio wanakuwa wakali na kuhoji.

Hitimisho
Kusubiri nchi ya maziwa na asali kwa serikali hii na watu wake ni kupoteza muda. Usitegemee mipango na mikakati mizito kuhusu kilimo, ufugaji, madini na rasilimali zingine kwa wafanya maamuzi wa namna hii.
 
Sijasoma andiko lote hadi mwisho lakini hapo padogo niliposoma panatosha kusema ulichoandika ni ukweli mtupu. Hili hata makazini ni sana tu yaani mpo sehemu wanakupeni vitini eti mpitie mjadiliane mtoe mapendekezo na kufanya maboresho hapohapo mlivyokaa ndani ya dakika chache tu (unakuta dakika 20 mfano)

Huwa nabaki kucheka tu moyoni na kinachofuata ni KANYAGA TWENDE!
 
""Wanasomea mule mule ukumbini na hivyo kujikuta wanahitaji zaidi msaada wa waandaaji ili kuzielewa hizo nyaraka.""

Mtanzania yeyote ni mvivu wa kusoma.

Ukitaka kuficha jambo basi liweke kwenye maandishi, Mtanzania hatoliona.

Hizo nyaraka hata zingesambazwa mwezi kabla, kama mtu ni mvivu kusoma hazitomsaidia kitu.

Sioni tatizo kwa mtu kusomea nyaraka kikaoni na pia si vibaya kumuhoji mwandaaji wa nyaraka kwa sababu yeye ndiye mwenye jukumu la kuufanya ujumbe wake ueleweke na siyo kazi ya msomaji kujielewesha penye utata.

Binafsi nina vitabu viwili nimevinunua na kimojawapo ni cha Ujasusi wa Kidola na Uchumi cha Mzee wa Mizimu Yericko Nyerere lakini sijamaliza hata sura moja kusoma wakati kina miezi zaidi ya minne ndani.
 
Ina maana hawapati muda wa Ku review?
Na Ku compare maamuzi hayo na sehemu mbali mbali ulimwenguni? Especially nchi tunazofanana nazo??
Labda waandaaji huwa wanakuwa wamemaliza details zote...so hakuna haja ya kutafuta data zaidi...!!
Nawaza tuu
 
Je, unafahamu kwamba wengi wa wafanya maamuzi serikali huwa hawana muda wa kusoma nyaraka na makablasha, kuchambua na kuamua? Subiri nikueleze.
Akina Zito, Dr Slaa, Tundu Lissu na akina Halima Mdee walikuwa wana Outsmart lile genge kwa sababu wa ajituma kusoma na kutafuta taarifa.

Mwingine kalala na mchepuko na pombe fofo anaamkia kwenye kikao cha maamuz
 
Back
Top Bottom