Fahamu ujenzi wa SGR unavyoendelea

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,338
TANZANIA :- FAHAMU UJENZI WA SGR UNAVYOENDELEA

Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway) ambapo ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam - Morogoro (km 300) umefikia asilimia 90.34 na kipande cha Morogoro - Makutupora (km 422) asilimia 57.57.

Aidha, tayari Serikali imesaini mkataba wa ujenzi wa kipande cha Mwanza - Isaka (km 341) wenye thamani ya shilingi trilioni 3.07; na kuendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa vipande vya Makutupora - Tabora (km 294) na Tabora - Isaka (km 133) na hapo baadaye kujenga njia ya Tabora - Kaliua - Kigoma (km 411) na Kaliua - Mpanda (km 207).

Katika kipindi cha Julai 2020 hadi Machi 2021 jumla ya shilingi bilioni 596.8 zimetumika katika utekelezaji wa mradi huu alisema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
 
Umeelezea kifupi ila vizuri sana maeneo utakapopita huo mradi, serikali isikae kulia lia itafute pesa wakamilishe huo mradi, waanze kwa kupunguza posho za wabunge kwa siku, wabunge wakipiga kelele wapunguziwe na mishahara yao, kama bado haitatosha wauze angalau ndege tano za ATCL.
 
🙏🙏🙏
 
Serikali ya Kenya ilimtuma waziri wake wa mambo ya nje juzi kuja kuomba mkopo wa shilingi trillion tatu. Waziri wetu wa fedha alisema watawapa huo mkopo kwa masharti nafuu sana.

Wakati huo huo serikali ya Tanzania imetoa msaada wa shilingi bilioni Saba kwa saccos za wajasiriamali nchini Israel. Waziri mkuu wa Israel ameishukuru serikali ya Tanzania na kutuhakikishia atadumisha utafiki uliopo Kati ya serikali hizi mbili.
 
Serikali ya Kenya ilimtuma waziri wake wa mambo ya nje juzi kuja kuomba mkopo wa shilingi trillion tatu.
Waziri wetu wa fedha alisema watawapa huo mkopo kwa madharti nafuu sana.

Duh hii ni kweli kabisa
 
Kweli kanda ya Kaskazini mwendazake alikuwa hatupendi. Yani miji ya kimkakati (strategic regions) kama Arusha, Tanga na Kilimanjaro aligoma kabisa kuweka hata robo kilometer ya SGR?

Hatari sana yule mzee kwa ukanda na ukabila.

Nateseka kutokea kanda maalum.
 
Serikali ya Kenya ilimtuma waziri wake wa mambo ya nje juzi kuja kuomba mkopo wa shilingi trillion tatu.
Waziri wetu wa fedha alisema watawapa huo mkopo kwa madharti nafuu sana.

Wakati huo huo serikali ya Tanzania imetoa msaada wa shilingi bilioni Saba kwa saccos za wajasiriamali nchini Israel. Waziri mkuu wa Israel ameishukuru serikali ya Tanzania na kutuhakikishia atadumisha utafiki uliopo Kati ya serikali hizi mbili.
Hizi bange bora tu zihalalishwe ili tusivutie toilet 😂😂😂
 
Kweli kanda ya Kaskazini mwendazake alikuwa hatupendi. Yani miji ya kimkakati (strategic regions) kama Arusha, Tanga na Kilimanjaro aligoma kabisa kuweka kata robo kilometer ya SGR?

Hatari sana yule mzee kwa ukanda na ukabila.

Nateseka kutokea kanda maalum.
Lakini mkuu si unakumbuka tren iliyo kua haitembei miaka mingi yeye kafanya itembee
 
Sawa ila hiyo treni haina tija kwa maendeleo katika karne hii ya 21.

Haiwezekani treni itumie masaa zaidi ya 12 kwa umbali wa kilometer 600 wakati kuna treni zinazoweza kutumia masaa matatu tu umbali huo huo.

Hayo matreni ya zamani yangewekwa tu kwenye museums kama kivutio cha utalii.
 
Ngoja tusubiri upepo wa mama
 
Swala la kusubiri
Ndio ujue kuna watu ni wendawazimu nchi hii, hata Magufuli alishasema mbona, ni walevi na mataahira. Ujenge Bagamoyo halafu SGR inafanya kazi gani, itabeba nini toka Dar port? Au ndio tusema pesa zote za SGR ndio zimepotea bure?

Mwingine anaeshindwa kutumia akili zake vizuri anataka tuachane na Rufiji, ina maana pesa zote tulizotumia zimepotea bure?
 
Back
Top Bottom