Fahamu Ugonjwa wa Homa ya Mgunda

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
HOMA YA MGUNDA NI NINI?

Ni Ugonjwa ambao huambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu. Homa ya Mgunda 'Leptospirosis' husababishwa na Bakteria aina ya 'Leptospira interrogans'

Dalili za HomaYaMgunda ni pamoja na Homa, Maumivu ya Kichwa na Misuli, Uchovu, Mwili kuwa na rangi ya njano, macho kuvilia damu, kutokwa damu puani na kukohoa damu

Maambukizi ya binadamu kwa binadamu ni nadra kutokea

BINADAMU ANAPATAJE MAAMBUKIZI?

Maambukizi kutoka kwa Wanyama hadi Binadamu yanaweza hutokea kwa;

Kugusa mkojo/maji maji mengine ya mwili kutoka kwa wanyama walioambukizwa

Kugusa Maji, Udongo au Chakula kilichochafuliwa na mkojo wa Wanyama

Kunywa Maji yaliyochafuliwa na Bakteria wa #HomaYaMgunda

Pia, Bakteria wanaweza kuingia mwilini kupitia ngozi yenye mikwaruzo, macho, pua au mdomo
 
Nadhani ingefaa ukataja ni wanyama gani wanaobeba hao bacteria wanaopelekea kumuathiri binadamu baada ya kugusana na na hao wanyama.
 
Nadhani ingefaa ukataja ni wanyama gani wanaobeba hao bacteria wanaopelekea kumuathiri binadamu baada ya kugusana na na hao wanyama.
Mkuu hata mbwa pia anapata huo ugonjwa na anaweza kuku ambukiza kama hutajikinga.

Hivyo tuendelee kujikinga
 
Back
Top Bottom