Fahamu mita za LUKU zinazofungwa majumbani

Weka betri mpya ili iwake kisha chomeka kwenye switch uwashe
Kuna ulazima gani wa kuweka betri kwenye remote kisha kuchomeka kwenye switch ili kuiwasha wakati ukishaweka betri unaweza kujaza token numbers? Au ukiweka betri kisha token numbers bila kuchomeka kwenye switch umeme hautawaka?
 
Kundi lapili ni lile la wateja wanao tumia units zaidi ambao huanzia units 0 283.4 hadi hawa ndio wale wanao itwa Tarrif 1 hawa bei ya units ni shs 292 nahapa atatumia mita ya single phase
Naomba kujua kwa nini hawa wa tariff 1 wananuna umeme kwa gharama kubwa ukilinganisha na hao wanaotumia umeme mwingi kama hapo chini
 
ASAHTE
Natumia mita ya remote, lkn kila siku ikifika saa kumi na mbili (12) jioni hadi saa nne(4) au tano(5) usiku umeme huwa unaka kwangu lkn kwa majilani unakuwa upo. Niko dsm, kinondoni kigogo mbuyuni karibu na uwanja wa msako no.0769049343


Wa-Dar mkoje jamani!!

Asahte=Ahsante
Majilani=Majirani
 
Kwahili leo TANESCO mmefanya la maana kutoa elimu kama hii hapa Jamii Forums, Kwanini mmetofautisha tariffs kwa mteja mkubwa na mdogo per unit? Wakati unit moja ni hiyo hiyo mega watts 1000 au KWH 1
Mkuu inaonyesha physics na hesabu zilikua baba mkwe!!
 
Wateja wetu wengi wamekuwa wakijiuliza iwapo wamefungiwa mita sahihi kutokana na matumizi yao ya umeme? Ama mita ambazo wamefungiwa ni za Viwandani na kulalamika wanatumia umeme mwingi zaidi tofauti na matumizi wanayotumia

Mita za LUKU zinazofungwa majumbani ni sahihi kwa matumizi ya nyumbani, ufungaji wa mita za majumbani hutegemea sana upimwaji wa matumizi /mahitaji ya umeme katika nyumba husika.

Mteja anafanyiwa tadhimini kabla ya kuunganishiwa umeme, wakati wa uunganishaji wa umeme inaangaliwa maombi kama Mteja ameomba kufungiwa njia moja (single phase) ama njia tatu (three phase) na haiwezekani Mteja aombe njia moja ya umeme afungiwe njia tatu.

Iwapo matumizi ya umeme ya Mteja yakiongezeka kufika unit 7500 hapo atalazimika kutumia mita za njia tatu (three phase) zenye uwezo wa Volts 400 kutoka mita ya njia moja yenye Volts 220 -250.

Wateja wengi hawafahamu hasa anapo tumia umeme ukafikia units 300 anadhani TANESCO ilikosea kumfungia umeme/mita. Sio kweli, kinachotakiwa ni Mteja kuwa na matumizi mazuri ya umeme ili kupunguza gharama.

Aidha, mita za LUKU za njia tatu kwa baadhi ya Wateja wenye mahitaji makubwa ya umeme wamefungiwa majumbani mwao hasa ambao tangu tathmini inafanyika ilionekana mahitaji ya umeme yatafika units 7500 maeneo mengine ni ya Kibiashara na ambako matumizi ya umeme wa njia moja hautofaa huwa wanafungiwa huo wa njia tatu.

Kwa wastani wa units 10 usiku na 6 mchana maana yake Mteja ana zaidi ya units 300 kwa mwezi yaani 16x30 utapata units mia nne (400) hayo si matumizi madogo, pia yapo mambo mengi ya kuyaangalia linapokuja suala la matumizi ya umeme, cha kwanza hiyo mita iko sahihi? TANESCO huwa inapima mita kulingana na maombi ya Mteja, ikiwa itagundulika kuwa mita ni mbovu Mita hiyo huondolewa eneo la Mteja, na Mteja atasahihishiwa account zake kulingana na kile kipindi mita haikusoma ipasavyo,

Jambo la pili ni Mteja anatakiwa kukagua mfumo wa umeme wa nyumba yake na kuhakikisha hakuna hitilafu (leakage) yoyote inayo pelekea umeme kuvuja na kumuongezea matumizi Mteja (Wiring system) na pia Mteja kuhakikisha earth load iwe shaba halisi.

Tatu ni vifaa anavyo tumia Mteja vina uwezo gani wa kutumia umeme? Nirahisi ku hesabu umeme tunaotumia na kutoa malalamiko kwa TANESCO, na Shirika litafanya ukaguzi ili kubaini matumizi hayo pengine ni sahihi, kila kifaa kina kiasi cha umeme kinachotumia kwa dakika ama masaa kadhaa. Inashauriwa Mteja kutumia vifaa vinavyotumia umeme mdogo (Energy Server), pia inashauriwa kuepuka vifaa vya mitumba sababu vingi vinatumia umeme mwingi.
Energy server = Energy Saver..
@# 2

IMG_20190912_151637.jpg
 
Mimi nilizoea mita ya zamani sasa nimukutana na mita ya bahdela,inanichanganya sijui ni kiasi gani cha unit kimebakia maana inabadilishabadilisha ma namba namba hata siielewi.msaada tafadhali.
 
Yanii huuu ni uongo ulio pindukia ikumbukwe umeme ni taaluma kama taaluma nyingine tena ni taaluma nyeti kuliko nyeti tulizo nazo na wala taaluma hii isichangwanye na imani za kishirikina

Mtu asiye jua umeme hawezi jua kazi ya earth rod. Mfumo wa wiring wa nyumba wa kisasa lazime uwe na kitu kinacho itwa PE yaani protective earth. Kwa kifupi kama hufahamu,

Protective earth ni namna ambayo vifaa vyote vinavyo tumia umeme yaani electic appliances in case vikawa na leakage ya umeme kwenye outer case au kiwambo cha nje basi protective earth itafanya kazi ya kuukusanya ule umeme na kuupeleka kwenye earth au udongo. Mfano. Nadhani ushawahi kuona Fridge au deki hata feni ambayo ukiigusa inakupiga shot au inatetemesha basi jua fika hicho kifaa kina leakege ya umeme au umeme unavuja. Kwasababu umeme unavuja huo umeme ilitakiwa ukusanywe na upelekwe ardhini. Soo kaz ya Protective earth ni kuupeleka umeme unaovuja kwenda ardhini

Na inabidi ujiulize ni kwanini kwenye udongo au ardhini??????

Ni kwasababu hata earth lod ya transformer ipo kwenye udongo ivyo huo umeme unavuja kutoka kwenye vifaa vyako vya umeme huzunguka na kurudi tena kwenye transformer kupitia earth au udongo. Kumbuka ardhi inapitisha umeme

Earth rod

Hiki ni chuma kinachoweka ardhini ili kuunganisha protective earth na earth yenyewe (ardhi). Maranyingi material yake ni copper yaani shaba.

Kwanini ni shaba???

Kwa mtu aliye soma umeme anajufika shaba au copper is a one of mostly good conductor of electricity yaani ni kipitisha kizuri cha umeme kuliko vyote kwasababu kina ukinzani mdogo (Law resistance) Pia kinahimili joto
Pia sifa nyingine ya shaba huwa haishiki kutu (Rusting) hivyo basi ukiwa na earth rod ya shaba ni uhakika tosha kuwa una kifaa madhubuti cha kupeleka umeme ardhini

Chumvi na mkaa
Kama nilivyo sema ardhi au udongo unapitsha umeme. Na ili ardhi ipitishe umeme vizuri inabidi iwe na unyevu. Kama wote tunavyo jua Chumvi ina unyevu hata ukiiweka mkononi lazima upate unyevu pia mkaa una absorb moisture yaani unatunza unyevu na hii ndio sabab chumvi na mkaa huwekwa kwenye earth rod na hii ni technic tuuu lakini nishasoma vitabu vingi sijawahi kuona hii kitu

MATUMIZI YA UMEME YANAYO SABABBISHWA NA LEAKEGE

Kuna matumizi ya umeme yasio ya lazima ambayo husababishwa na uvujaji wa umeme kwenye wiring ya nyumba. Hii hutakana na sababu nyingi sana. Moja ikiwa ni designe ya kifaa chenywe kilivyo undwa na pia ni greater kati ya wire wa live na neutral au earth.
Ukinzani uliopo ndio husababisha kuonyesha kuwa kiasi hicho cha umeme kimetumika.
Na kiuhalisia ni kweli kimetumika ila bila manufaa yoyote

Nini cha kufanya

Ni muhimu kukagua wiring yako kama ina shida au vipi na pia ni muhimu kupima na kujua leakage ya vifaa vyako ambavyo ni frequent used. Mfano. Fridge linaweza tumika hata masaa 72 bila kuzima so kama lina leakage jua litamaliza umeme wa kuosha


Protective Earh Briefly
PE inafaida kubwa sana kwenye wiring ya nyumba yoyote au kiwanda linapokuja suala la radi. Kwani husaidia kukusanya umeme unaotokana na radi na kuupeleka ardhini

Japo PE ndio inyokula umeme unaovuja kwenye vifaa. Ivyo inashauriwa kuwa na PE kwenye nyumba yako maana faida ni kubwa kuliko hasara ambayo unaweza pata

Swali lako la msingi

Earth lod inapokuwa shaba halisi ndio husababisha kupotea kwa umeme sanaa kuliko unapokuwa na Lod fake.

Nakupa Fact.

Earth lod ya shaba ndio hupitisha umeme vizuri tena kwa uhakia kwenda ardhi ila fake hipitisha kwa mashaka kwasababu ya factors kama kutu au chuma chenyewe kilicho tumika

Mafundi uchwara hawajuii hiki kitu ndio huwaingiza chaka wateja na kuwaweka rehani kwa matatizo mengi

Solution.

Kupotea kwa umeme hakutibiwi kwa kubadirishla lod. Ila ni kujua ubovu yaani fault na hasa leakage inayosababisha umeme uvuje na kuitibu. Na sio kupoteza pesa kwa kuanza kunua lod na kuchimba chimba pembeni ya nyumba yako.

Nadhani ushawahi kukutana mtu au wew mwenyew kuona Circuit breaker ya nyumba yako inazima zima kila mara. Na unaona mtu analaumu sana


Hapa hutakiwi kulaumu ila ndo mida wa kujisifu kuwa wiring yangu na PE yangu ni nzima na inafanya kazi kwa usahihi swala ni kutafuta taizo


Kwa yeyote mwenye shida just call
0712425141
0763554400
Occybeats@live.com
Kuna makosa machache hapa japo umejitahidi kueleza vizuri kwanza Copper sio best conductor ipo kitu inaitwa Silver hio ndio best conductor, Lakini pia detection ya leakage kwenye kifaa haipaswi kuwepo mana itahatarisha usalama wa mteja au mnyama atakae gusa icho kifaa ivo metal case haipaswi kuwa na Potential difference ndo mana inakuwa earthed just incase Potential difference ikitokea ipelekwe ardhini na kumlinda consumer ijapokuwa inamlinda consumer ila tayari hio ni leakage na bill itaongezeka mana umeme utaenda ardhini ambapo ardhi hu act kama dampo la kuchukua izo taka taka au masalai usipokuwa na strong earth umeme hautaenda ardhini na badala yake utampiga mtu shock akigusa metal case ya hio equipment whether ni Fridge au Cooker nini kifanyike ili kusiwe na Leakage kuna kifaa kinaitwa ELCB Earth leakage Circuit Breaker hiki kita detect kuwa metal case imepata Voltage na kufungua circuit ili kuepusha upotevu zaidi.
 
Back
Top Bottom