Fahamu matumizi ya gesi asilia kwenye gari lako

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
HABARI MPYA YA MJINI!!!

GARI LAKO SASA LINAWEZA KUTUMIA GESI ASILIA

Utangulizi:

Taasisi Tecknologia Dar es Salaam (DIT) kwa kushirikiana na wadau wengine wa gesi asilia tunaongeza mfumo wa gesi asilia kwenye magari yanayotumia petrol. Mfumo huu unamwezesha mwenye gari kuwa na uwezo wa kutumia gesi asilia au petrol kulinga na upatikanaji wake. Kwa sasa tunafunga magari yote ya petrol kuanzia madogo IST hadi makubwa V8. Pia tumeanza kufunga gesi asilia kwenye daladala.

Gharama za kuweka huu mfumo:

Gharama inategemea na ukubwa wa injini yaani idadi ya cylinder za injini yako. Mfano kwa gari zenye;
1. cylinder 4 gharama ni 1.8m,
2. Cylinder 6 gharama ni 2.2m
3. Cylinder 8 gharama inaenda mpaka 2.5m.
Hata hivyo kuna baadhi ya gari gharama hizi inaweza zidi kutokana na mfumo wa injini (kama brevis, crown na voxy ambayo injini zake ni GDI)

Faida za huu mfumo:

1. Unafuu wa gharama za uendeshaji;
Kutumia gesi unapunguza gharama kwa zaidi ya asilimia 40 mpaka 50. Bei ya gesi asilia iko chini sana, ukilinganisha na petrol. Mfano 1kg ya gesi ni sh 1500/= ukilinganisha na sh 2200/= kwa lita ya petrol.
1kg ya gesi unaweza kwenda zaidi ya km 20, na kwa mtungi wa 15kg ambao ni sh 22,500/= unaweza kwenda zaidi ya km 200.
2. Kupunguza uchafuzi wa mazingira;
Gesi ni safi ukilingalinisha na petrol au diesel.
3. Kuongeza kipindi cha kufanya matengenezo ya injini yako;
Kwa kuwa gesi asilia ni safi, basi hata injini yako inakuwa salama zaidi. Mfano kama ulikuwa unafanya matengenezo kila baada ya km 3000, kwa kutumia gesi asilia unaweza kufanya hata baada ya km 9000.
4. Gesi asilia ni salama zaidi;
Gesi asilia ni salama zaidi ukilinganisha na petrol kwani inahitaji joto kubwa sana ili iweze kuwaka ukilinganisha na petrol.

Mahali pa kubadilishia mfumo:

Kwa sasa Tanzania nzima ni sehemu moja tuu inafanya kazi ya kubadili, nayo ni Taasisi ya tecknologia Dar es Salaam (DIT).

Mahali pa kujazia Gesi:

Kwa sasa mahali pa kujazia gesi ni ubungo maziwa. Hata hivyo serikali iko mbioni kuongeza vituo zaidi ya 5 sehemu mbalimbali hapa Dar es salaam.

Hitimisho:
Taasisi ya Tecknolojia Dar es salaam DIT inakukaribisha sana uje uweke mfumo wa gesi asilia kwenye gari lako, kwani ni nafuu na salama zaidi.

Asante
Dr. Esebi Nyari
Mratibu wa gesi asilia- DIT
0755821240
0717962127
eusnyari@gmail.com
----------------------------------
Please share
 
Je, naweza kufungua vituo vyangu vya kufanya engine conversion na kujaza gesi mikoani?
 
Je

Je, naweza kufungua vituo vyangu vya kufanya engine conversion na kujaza gesi mikoani?
Mfumo Unafanya kazi kwa kutumia engine moja tu. Wakati mtungi wa Gas ukiwa unatumika na wakati huo huo gari yako inaweza kuwa imejaa Petrol or diesel kutokana na aina ya fuel inayotumika.

Kufanya mikoani ni gharama kubwa sana maana mpaka sasa kuna sheli moja tu Nchi nzima inayotumika kujaza Gas kama imeisha kwenye mtungi.

Na mostly kwa hapa Tanzania hili zoezi linafanyikia Katika Chuo cha DIT tu.
 
HABARI MPYA YA MJINI!!!

Hii habari nafikiri nimeanza kuisoma mwaka 2011 au 2012 hivi so sidhani kama ni mpya. Ila nilichogundua hao jamaa hawako siriaz maana tangu waanze kutangaza mpaka leo bado kituo cha kuwekea hiyo huduma ni kimoja nchi nzima (Dar) utadhani maabara ya kupima covid na hakuna mwamko wala maendeleo yoyote ya kuongeza vituo wala kupanua huduma iwafikie watu wengi. Hata hapo Dar penyewe nadhani wanaojua hii huduma wanahesabika. Nafikiri kuna tatizo mahali ktk utekelezaji wa hili swala.
 
Nibadili mfumo kwa bei kuuuubwa, halafu gesi ikiisha niko shangamwalugesha ndani huko nipaki gaei, ninyofoe mtungi, nilipe nauli 150000 niende mpaka dar ili nijaze gesi ya 22000, kweli? Wakati hiyo laki na nusu ya nauli naweza kujaza mafuta kwenye kiprobox nikatembea mwanza mpaka shy town? Hii huduma inawafaa zaidi wanaoishi na kufanya kazi hapohapo ubungo maziwa (wafanyakazi wa hicho kituo).
 
Hawako serious na kazi yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heheheh umenifurahisha eti wafanyakazi wa ubungo maziwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii habari nafikiri nimeanza kuisoma mwaka 2011 au 2012 hivi so sidhani kama ni mpya. Ila nilichogundua hao jamaa hawako siriaz maana tangu waanze kutangaza mpaka leo bado kituo cha kuwekea hiyo huduma ni kimoja nchi nzima (Dar) utadhani maabara ya kupima covid na hakuna mwamko wala maendeleo yoyote ya kuongeza vituo wala kupanua huduma iwafikie watu wengi. Hata hapo Dar penyewe nadhani wanaojua hii huduma wanahesabika. Nafikiri kuna tatizo mahali ktk utekelezaji wa hili swala.
Mkuu umeongea ukweli ni miaka mingi wana hii technology mm niliona mwaka 2012 kama sio 2013 jamaa gari yake outlander ilikua inabwia mafuta hatari akaweka gas lakin sidhan kama mfumo huo aliutumia sana ziaidi ya dharura na gari aliuza so ntamuuliza changamoto zake n.k
Ila hawa jamaa hawako serious kabsa wanashindwa hata kutangaza na kuongeza filling stations walau hata kila wilaya 5 hapo inakatisha wadau tamaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom