Dkt. Biteko azindua kituo cha kisasa cha kujazia gesi asilia kwenye magari (CNG)

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Biteko JamiiForums.png

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko leo amezindua kituo cha kwanza cha kisasa cha kujazia gesi asilia kwenye magari na karakana ya kuweka mfumo wa gesi asilia ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa mipango ya Serikali kuchochea matumizi ya gesi asilia kama nishati safi na salama kwa mazingira.

Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam tarehe 11 Novemba, 2023 na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, Balozi Sherif Ismail wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Balozi Isaac Njenga wa Jamhuri ya Kenya, Balozi Fred Mwesigye wa Jamhuri ya Uganda, Mha. Felchesmi Mramba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya TAQA, Pakin Kafafy.

Dkt. Biteko amesema kuwa, kujengwa kwa kituo hicho na TAQA Arabia na washirika wao JCG Oil & Gas niutekelezaji wa maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa na maono ya kuleta wawekezaji nchini wakiwemo wanaowekeza kwenye Sekta ya Nishati, hivyo ameahidi kuwa Wizara itafanyia maelekezo yake ili kutekeleza maono yake.

Dkt. Biteko amesema kuwa, Serikali inaweka msukumo mkubwa kwenye matumizi ya gesi ya asilia yakiwemo magari, mitambo ya viwandani, hivyo kuzinduliwa kwa kituo hicho ni kuonesha azma ya Serikali ya kuhakikisha kuwa Gesi inayopatikana Tanzania inatumika ndani ya nchi kwanza.

Amesema kituo hicho kitajaza gesi kwenye magari 800 kwa siku na kina pampu sita zitakazojaza gesi kwenye magari sita kwa maramoja ambapo ujazaji wa gari moja utakuwa ni wa dakika tatu hivyo hicho ni kituo kikubwa kitakachosaidia kubadilisha magari na kufanya yatumie gesi badala ya mafuta pekee.

Amesema Kampuni hiyo inatarajia kujenga vituo 12 vya CNG jijini Dar es Salaam ili kuwa na vituo vingi zaidi vya kujazia gesi kwenye magari.

CNG Airport Taqwa master gas Jamiiforums.jpg

Ameongeza kuwa, kampuni hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wapo kwenye majadiliano ili kujenga vituo vidogo vya Gesi ya Kusindika (LNG) ili kuweza kutoa Gesi jijini Dar es Salaam na kupeleka kwenye mikoa mbalimbali ili nayo iweze kujaza gesi hiyo kwenye magari..

Amesema kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono katika uwekezaji wao ili kuchochea ukuaji wa nishati nchini.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo ameishukuru Wizara ya Nishati kwa kutekeleza maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya usambazaji nishati katika maeneo yote ikiwemo gesi asilia.

CNG Airport Taqwa gas Jamiiforums.jpg

Amesema kuwa Wilaya ya Ilala, inaona faraja kufunguliwa kwa kituo wilayani humo kutokana na kuwa kitovu cha Mkoa wa Dar es Salaam kwani Wilaya hiyo ina wananchi wasiopungua milioni 1.6 ukilinganisha na idadi yote ya wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao jumla yao ni milioni 5.3.
 
Dkt. Biteko amesema kuwa, kujengwa kwa kituo hicho na TAQA Arabia na washirika wao JCG Oil & Gas niutekelezaji wa maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa na maono ya kuleta wawekezaji nchini wakiwemo wanaowekeza kwenye Sekta ya Nishati, hivyo ameahidi kuwa Wizara itafanyia maelekezo yake ili kutekeleza maono yake.

Nchi ngumu sana hii...kila kitu ni lazima ujipendekeze
 
Jambo jema, maana tulikua tunajazana hapo Ubungo maziwa hadi kero. Sa100 anazidi kuupiga mwingi.
 
Tatizo vituo viko Dar tu ni shida..Dangote magari yake anaweka mitungi kibao ya CNG sababu njiani hamna vituo vya CNG

Kama kweli tumedhamiria gesi yetu itumike vituo vijengwe nchi nzima tuachane na matumizi ya mafuta au hata serikali basi kuonyesha iko serious magari yote ya Serikali na wabunge na mahakama na taasisi za umma waanze kutumia CNG kwa kuanzia.
 
Dkt. Biteko amesema kuwa, kujengwa kwa kituo hicho na TAQA Arabia na washirika wao JCG Oil & Gas niutekelezaji wa maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa na maono ya kuleta wawekezaji nchini wakiwemo wanaowekeza kwenye Sekta ya Nishati, hivyo ameahidi kuwa Wizara itafanyia maelekezo yake ili kutekeleza maono yake.

Nchi ngumu sana hii...kila kitu ni lazima ujipendekeze
Ujinga mwingi sana Nchi hii. Kila kitu ni maono ya Rais. Hata kupata kwangu mlo mmoja kwa siku huenda ni maono ya Rais pia. Disgusting. Kituo chenyewe ni hiki kilichojengwa hapa Airport Mkabala na Msikiti?.
 
.

.
Kwa tafsiri nyingine ni kwamba wananchi hawana serikali bali kuna serikali ambayo ni mali ya rais.

Magufuli alileta mila mbaya sana kwenye siasa za nchi. Kiongozi kusifiwa sifiwa ni dalili ya kudharauliwa. Ndio maana kipindi cha Kikwete hakukuwa na machawa maana walijua Kikwete ni mwelevu sana asingekubali unafki wao. Kikwete alikuwa anatafuta kusifiwa na wananchi sio mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya wala wana ccm wenzake sababu alijua yeye ni mtumishi wa wananchi.
Bahati mbaya sana katika nchi hii Uongozi bila kuchagizwa na kauli za Kichawa haunogi.
 
Vifunguliwe walau hata majiji yote

Dar viko kama sikosei.vitatu sasa hivi mikoani vipi?
 
Mi nikishaona tu sijui maono ya Rais huwa sitaki kusoma tena, ina maana siyo mahitaji ya wananchi ni maono ya Rais? rubbish
Hivi hii nchi sisi tumerogwa? Wakuu wa nchi wanakuwa miungu watu tatizo nini? Hili swala la Gesi ni la leo kweli? Mtwara watu wameuawa ili kuitoa gesi lini? Si ni takriban miaka kumi iliyopita Mh Kikwete akiwa raisi. Haya si yalitakiwa yafanyike wakati ule? Hiki chama kwa kweli kina mauzauza sana. Ingewezekana kukipiga dawa kikafa kama mdudu alae majani ningefanya hivyo. Kinahitaji kufutwa mara moja
 
CCM ni laana ya nchi
 
Back
Top Bottom