Facts juu ya uongozi wa CHADEMA vyuo vikuu; kusema uongo ni kazi wanayoiweza...

Status
Not open for further replies.
Seconded!!

Tumeangukia kwenye udini kiasi kwamba sasa majina ya kibantu yanaonekana ni ya kikristo.... Hatari sana hii!!

Kuna kijana nilisoma naye alikuwa anaitwa Jackson John. Siku zote nlikuwa najua ni mkristo mpaka nilipokutana naye kipindi cha mfungo wa ramadhani ndipo nikagundua kumbe ni mwislamu tena wa swala tano!!

Na wakiambiwa waislamu nchi hii ni 32% wanang'aka!
 
Hakuna hata muislamu mmoja? Ahaa Chademaa watakuja na maneno hayo sasa

Wewe Ngwini kama hao ulowataja hawakugombea au waligombea na kura hazikutosha CDM wawapatie "VITI MAALUM?" Je Secretariat iliyopitishwa juzi na CCM Asilimia ya WAKRISTO ni Wangapi? Je tukibatize CCM kuwa ni chama cha KIISLAMU? TAFAKARI
 
Haya ndio majibu ya Pro-Chadema JF dhidi ya Waislam...tunashukuru tutakutana mwaka 2015 kwenye box la kura na chama chenu.

kwani wewe ndiyo mwakilishi wa waislamu Tanzania .... kama ni hivyo basi waislamu wanakazi ..... vinginevyo naona unawawakilisha kile kikundi cha vurugu cha ponda issa ponda
 
Jana niliandika hivi, nilipoona jina la mleta mada hata sikusumbuka kuisoma tena.... sometimes ni vyema kuwapuuzia watu wa namna hii
 
Unaona umeandiiiika kweli kuisafisha CDM kwenye kadhia hii. Lakini umesahau hapo kwenye udini. By the way mbona wote ni wadini moja?

Unashindwa kufikiri toka lini majina yakabeba dini ya mtu, toka lini jina likamaanisha dini, katika kama dini ni majina basi imani yako imekufa au hujui maana ya dini
 
Chuo Kikuu MZUMBE

  • Mwenyekiti ni Roda Edward
  • Katibu ni Bariki Mwakibete

Chuo Kikuu cha UDOM

  • Mwenyekiti ni Nchimbi Method
  • Katibu ni Malale Sende

Chuo Kikuu cha Mwenge
  • Mwenyekiti ni Abel Dendwa

Chuo Kikuu cha SAUT

  • Mwenyekiti ni Patrobas Paschal
  • Katibu ni Makoko Obadia

Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT)

  • Mwenyekiti ni Paul Ndeje
  • Katibu ni Masuala Masaga

Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph - Thobias Leizer

Chuo Kikuu cha Jurdan - Newton Chamkongo

Chuo cha Mtakatifu John

  • Salvatory Sege
  • Leiza Maige

Chuo Kikuu Kishiriki DUCE - Atupele

Watakaotaka facts zaidi kwa ajili ya constructive criticism and critiques waseme tuwaongezee. Watakaotaka kuendelea kujadili ukabila, udini, rangi au eneo analotoka mtu kama vitu vya msingi sana kwao katika kujadili viongozi bora waendelee.

Ndugu mwandishi wa habari naomba unijibu swali moja dogo maana hapo kwenye bold inaonyesha unajua mengi sana. Je hayo majina ya dini moja imetokea bahati mbaya? au ni mikakati? Je katika hivyo vyuo hakuna wa dini nyingine? mfano duce inayochukua waalimu inasemekana wengi 50/50 pengine ni wa ile dini nyingine maana wao si ndio wanafeli sana na siku hizi ualimu ni fani ya wanaofeli? Lakini mwenyekiti wa pale duce anatokea dini nyingine?

Kuna mambo yanaweza kuonekana ni hoja dhaifu lakini mambo kama haya hayamuingii mtu akili hata ukitetea kwa namna gani sana sana sisi tusiofungamana na vyama tutaona mambo mawili.

1. Wewe ni mfia chama
2. Unawezeshwa kubwabwaja

Siku njema ila naomba ufikirie kuwa katika uongozi woote huo uliotuletea wa vyuo mbalimbali uteuzi wa kuwapigia kura hao ulikuwa wa kimkakati au imetokea bahati mbaya?
 
kwani wewe ndiyo mwakilishi wa waislamu Tanzania .... kama ni hivyo basi waislamu wanakazi ..... vinginevyo naona unawawakilisha kile kikundi cha vurugu cha ponda issa ponda

Wewe ni kati ya Pro-Chadema JF unaowakimbiza Waislam ndani ya Chadema kwa kejeli na dharau zako dhidi ya Uislam.
 
Tumaini Makene

Nashukuru kuwa na watu wenye uelewa kama wewe, Watanzania wamekuwa kama samaki wnakokotwa kwenye juya la CCM wakitafuta kila mbinu ya kujinasua kuangamia baada ya kukosa majibu ya matatizo ya watu; maisha bora kwa kila Mtanzania sasa wanapandikiza chuki badala ya kutafuta majibu ya matatizo!!! Sasa ukisema Mchaga au Mwislamu au Mkristo huyo sio Mtanzania, hilo ni jibula matatizo ya Watanzania?

Je, kukitokea fujo na labsha ndio utatuzi wa shida zetu?? Wizi wa EPA, MEREREMETA, DOWANS, mABILION YALIYOFICHWA Uswiss na South Africa yataletwa na udini na ukabila??? Wizi kwenye Halmashauri zetu na rushwa utakomeshwa na udini na ukabila???

Watanzania hasa watu wenye uelewa tuache ushabiki usio na tija tujipange kuokoa taifa letu lililo angamizwa na CCM na hila zake!!!!
 
Last edited by a moderator:
Ndugu mwandishi wa habari naomba unijibu swali moja dogo maana hapo kwenye bold inaonyesha unajua mengi sana. Je hayo majina ya dini moja imetokea bahati mbaya? au ni mikakati? Je katika hivyo vyuo hakuna wa dini nyingine? mfano duce inayochukua waalimu inasemekana wengi 50/50 pengine ni wa ile dini nyingine maana wao si ndio wanafeli sana na siku hizi ualimu ni fani ya wanaofeli? Lakini mwenyekiti wa pale duce anatokea dini nyingine?

Kuna mambo yanaweza kuonekana ni hoja dhaifu lakini mambo kama haya hayamuingii mtu akili hata ukitetea kwa namna gani sana sana sisi tusiofungamana na vyama tutaona mambo mawili.

1. Wewe ni mfia chama
2. Unawezeshwa kubwabwaja

Siku njema ila naomba ufikirie kuwa katika uongozi woote huo uliotuletea wa vyuo mbalimbali uteuzi wa kuwapigia kura hao ulikuwa wa kimkakati au imetokea bahati mbaya?

Unanikumbusha kauli ya Mzee Mtei wakati akilalamika kwa nini Waislam wengi kwenye wajumbe wa tume ya katiba halafu wao Wakiristo wachache.
 
Tumaini Makene

umeongea vizuri ila una mihemko mikali sana na jazba, hebu tulia kidogo, pata juice ya muwa bariid pale kariakoo round about then utulize moyo wako tuje tujadiliane...

Nimeifatilia ile thread ya propaganda na udini kama unavosema kwa umakini sana,pia hata naww nimekufatilia kwa umakini sana
niweke wazi,i am non aligned movement between ccm & cdm..

Ingawa ccm inatumia propganda chafu ya udini na ukabila dhidi ya cdm na wote kwa pamoja tunalipinga jambo hilo,,sasa tujiulize bila kuchagua upande wowote,je lisemwalo lipo??au lilishawahi kuwepo likarekebishwa?ktk ccm kuna wachaga wengi tuh,wachaga waislam na wachaga wakristo,cha kushangaza wakati mwingne wachaga hao hao waislam na wakristo waliopo ndani ya ccm ndio husema ya kwamba chadema ni chama cha kidini na kikabila unauona huo mkanganyiko?

Inawezekana ikawa kweli ni mtaji wa kisiasa wa ccm kwa cdm kama vile ufisadi wa ccm ulivo mtaji wa kisiasa kwa chadema,tujiulize lisemwalo lipo halipo??

Katika list hii uliyoiweka sasa wa hao viongozi wa cdm vyuo vikuu,nikiangalia kwa utafit wa haraka haraka kwa kutumia majina simpati muislam hata mmoja,je ni kweli ya kwamba hakuna vijana wa kiislam vyuo vikuu ambao wana mapenz na cdm?je ni kweli ya kwamba hawakujitokeza kugombea kama unavosema?

Siasa ni mchezo mchafu unafahamika.,ila yapo baadhi ya mambo yasemwayo yanapicha yenye uhalisia kiasi chake

tuyachunguze na kuyafanyia kazi..
 
Last edited by a moderator:
Ndugu mwandishi wa habari naomba unijibu swali moja dogo maana hapo kwenye bold inaonyesha unajua mengi sana. Je hayo majina ya dini moja imetokea bahati mbaya? au ni mikakati? Je katika hivyo vyuo hakuna wa dini nyingine? mfano duce inayochukua waalimu inasemekana wengi 50/50 pengine ni wa ile dini nyingine maana wao si ndio wanafeli sana na siku hizi ualimu ni fani ya wanaofeli? Lakini mwenyekiti wa pale duce anatokea dini nyingine?

Kuna mambo yanaweza kuonekana ni hoja dhaifu lakini mambo kama haya hayamuingii mtu akili hata ukitetea kwa namna gani sana sana sisi tusiofungamana na vyama tutaona mambo mawili.

1. Wewe ni mfia chama
2. Unawezeshwa kubwabwaja

Siku njema ila naomba ufikirie kuwa katika uongozi woote huo uliotuletea wa vyuo mbalimbali uteuzi wa kuwapigia kura hao ulikuwa wa kimkakati au imetokea bahati mbaya?

Hao waislam wao hawakwepo kwenye kuchagua hao wakristo, mbona nyie mna visa sana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom