Facebook ni nini?

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Wana JF, kuuliza si ujinga ndugu zangu. Naomba mnisaidie, nini maana ya FACEBOOK na inatumikaje? Nimekuwa nikisikia terminology hii kila kukicha na kila niulizpo watu, wengi nona kwao inakuwa mashikolo. Nisaidieni tafadhali. Na kama kuna uwezekano, nielekezeni namna ya kujiunga.
 
unatoka kijiji gani??? usivamie miji kwa pupa!!! ni hatari
 
... Mimi ni mwanasheria msomi., nasaidia watu wasiojua siku zote. Hata pweza paolo anajua. Ni kwamba FACEBOOK/ usokitabu ni forum tu kama JF, tafauti ni kwamba inatumiwa na teenagers zaidi, na pia ilianzishwa na wanachuo wa Havard mwaka 2004 kama jukwaa la kukutana marafiki waliopotezana muda.

Facebook ni forum nzuri sana ya kupotezea muda, kwa hiyo kama huna shughuli jiunge sasa hivi. Namna ya kujiunga ni rahisi tu hata kuliko JF., tembelea Welcome to Facebook na ufuate maelekezo.

Wasalaam.:eyeroll2:
 
unatoka kijiji gani??? usivamie miji kwa pupa!!! ni hatari
Kuwa mjini sio ndio kujua habari za FACEBOOK mbona wapo watu kibao mjini na hawaijui facebook, na wengine tupo bush tunaijua mwanzo mwisho, acha hizo!
 
Kuwa mjini sio ndio kujua habari za FACEBOOK mbona wapo watu kibao mjini na hawaijui facebook, na wengine tupo bush tunaijua mwanzo mwisho, acha hizo!
You make my day for your comments, ni kweli njia inaweza ikawepo kijijini kwenu na bado unaweza usiifahamu. Hii inatokana na ukweli kwamba kupita njia fulani ni utashi unaoambatana na mahitaji tarajiwa!
 
Kukaa mjini co kujua kila kitu, m2 haishi kujifunza kila siku wala usimcheke akuulizae wewe ulitaka aulize wap? kama c hapa jamvini?
 
... Mimi ni mwanasheria msomi., nasaidia watu wasiojua siku zote. Hata pweza paolo anajua. Ni kwamba FACEBOOK/ usokitabu ni forum tu kama JF, tafauti ni kwamba inatumiwa na teenagers zaidi, na pia ilianzishwa na wanachuo wa Havard mwaka 2004 kama jukwaa la kukutana marafiki waliopotezana muda.

Facebook ni forum nzuri sana ya kupotezea muda, kwa hiyo kama huna shughuli jiunge sasa hivi. Namna ya kujiunga ni rahisi tu hata kuliko JF., tembelea Welcome to Facebook na ufuate maelekezo.

Wasalaam.:eyeroll2:

saf mwana JF
 
Inakuwa nzuri sana kama ukijituma kidogo kufanya karisechi kagugo, ukikosa la maana ndy unauliza wananchi! ukigoogle "what is facebook" wallah kesho unaweza hata kutoa seminar kwa wengine kuhusu facebook!
 
Muuliza swali ni kama kada wa chama vileeeeeeeeee.
Maana hajadhubutu ata kugoogle au kuweekpedia ili angalau aje na lolote apa.
Kwa maswali kama hayo kuiondoa CCM madarakani ipo kazi
 
Muuliza swali ni kama kada wa chama vileeeeeeeeee.
Maana hajadhubutu ata kugoogle au kuweekpedia ili angalau aje na lolote apa.
Kwa maswali kama hayo kuiondoa CCM madarakani ipo kazi

Aulizaye anataka kujua, "NO ONE IS PERFECT". Inawezekana hata mie kuna vitu sivijuwi
 
Kwa kifupi Facebook ni website kwenye internet kwa ajili ya ku-socialise mtu na marafiki zake. Ukiingia unakuwa na ukurasa wako inaitwa 'wall paper' ambapo unachoandika au unachoandikiwa humo huwa inasomwa na marafiki zako wote. Mfano, ukitaka kueleza habari kama kupata mtoto unaiandika kwenye wall paper yako halafu marafiki zako wote huisoma bila kuhitaji wewe kuwatumia e-mail au message mmoja mmoja. Marafiki unaowapata ni kwa kuwaalika ama wewe kualikwa. Kuwa na rafiki sio automatic bali ni mpaka wote wawili mkubali kuwa marafiki. Kwenye wall paper yako pia unaweza kubandika picha na video. Vilevile una fursa ya kuwasiliana moja kwa moja na rafiki yako bila kutumia 'wall paper' bali kuna sehemu ya kutumia meseji. Kuna 'features' zingine nyingi tu ndani yake. Ila kwa kifupi ni sehemu ambayo masuala yako ukiyaanika husomwa na watu wengi.
 
Back
Top Bottom