Fabregas awaomba radhi mashabiki wa Arsenal!

Achraf Hakimi

JF-Expert Member
Mar 3, 2010
875
1,779


Masaa machache tangu ajiunge rasmi na Barcelona, Cesc Fabregas amewaomba radhi mashabiki wa klabu ya Arsenal kwa kutowaambia lolote juu ya uhamisho wake kwenda Barcelona huku akiahaidi kuwapa sababu zilizomfanya ahame kwenye klabu ndani ya siku chache zijazo.

Fabregas ambaye alikuwa nahodha wa Arsenal amerudi Barca baada ya kuwepo Emirate kwa takribani miaka 8 na hatimaye Jumatatu alimaliza utata wa uhamisho wake kwenda Catalunya.


Kiungo huyo wa Spain anasema uongozi wa Arsenal waliweka sheria kali juu ya kuongelea uhamisho wake na ndio maana alishindwa kuzungumza chochote.


Fabregas anakiri ulikuwa ni uamuzi mgumu kuondoka Emirates Stadium na anasema atawaambia mashabiki wa Gunners ukweli wote kuhusu uhamisho wake wa kujiunga na Barca.

“Nina muda wa kuzungumza juu ya suala hili na nitafanya interview maalum kwa ajili ya kuwaambia story yote mashabiki wa Arsenal kuhusu uhamisho wangu.


“Samahani sikuweza kusema chochote katika kipindi chote cha miezi miwili na nusu, Arsenal walinikataza kuzungumza lolote kuhusu uhamisho wangu hata kama nilikuwa nataka kufanya hivyo lakini nilishindwa.

“Sijisikii vizuri na nilikosa amani juu ya hili kwa sababu nilikuwa na mahusiano mazuri sana na mashabiki kwa miaka mingi. Ilinichukua muda mrefu kupata sapoti na inaniuma kwamba naweza kuwapoteza wao na sapoti zao kwangu.


“Maneno pekee niliyonayo na shukrani kwao, sitosahau vyote walivyonifanyia, nilifanya na kujitoa kwa kila kitu kwa ajili ya klabu ile na najua kwamba wanafahamu lakini najua kwamba ni uamuzi sahihi kurudi hapa(Barcelona).


“Ninaomba radhi kwa fans kwamba sikuwaabia chochote. Nina masikitiko makubwa kuondoka. Nimetumia robo tatu ya maisha yangu pale, miaka 8, nina huzuni kubwa lakini maisha yanaendelea.” -Fabregas
 
arsenal ni ushuzi na ni bora kasepa...
Timu kila siku inasukwa na haikamiliki, kama si usakala ni nini?
Fabregas kaja ana miaka 16 kaambiwa timu inasukwa mpaka uso umemjaa madevu na keshakomaa bado anaambiwa timu inasukwa...

tumeona timu kama REal Madrid ikisukwa na tofauti unaona, timu kama Inter Mourinho aliisuka kwa misimu miwili tu na ikabeba makombe yoote.

Sasa hiyo Assnail inayosukwa kila msimu halafu inaruhusu watu kama Flamini, Hleb, Henry, Clichy, Cesc, Gilberto na wengine weeengi kuondoka ile hali wao ndio wangekuwa mashujaa wa kupigana na kupata vikombe.

Wenger ni Gagulo na anatakiwa afukuzwe na kulambwa viboko 12 ili akamuonyeshe Mkewe anayempaga mawazo mgando kama hayo.


nimefurahi Cesc kuondoka, sasa bado Van Persie na Nasri.

Wapuuzi wakubwa hawa yaani timu iko Dunia ya kwanza halafu wanaleta uongo na porojo kama za CCM wanaojishauaga kuwa uchumi wa taifa utapanda hivi soon na bei ya mafuta, umeme vitashuka. Tutajenga barabara za juu.....puuumbav
 
Timu bovu na haina ambitions. Timu hiyo haina hata kikombe kimoja cha UEFA Champions League!
 
Mimi si shabaki wa arsenal ila kiukweli nasaport uhamisho wake kwa asilimia mia.dogo anakipaji sana na alijitolea na kupigania mafanikio ya timu kwa nguvu zake zote ila alichopata ni masikitiko tu badala ya medali mbalimbali huu ni wakati wake wa kutafuta medali zilizoshindwa kupatika arsenal kutokana na sera mbovu za mchumi wenger na barca ndio mahala pake na mwaka huu arsenal isiposhuka daraja!sijui!
 
mwacheni dogo akasugue benchi mpaka xavi na iniesta watakapostaafu!
Nashangaa sijui kwa nini mashabiki wa Arsenal mmemchukia Fabregas kiasi hicho utadhani yeye ndio alisababisha mkose makombe
Fabregas amerudi nyumbani kwao ambako baada ya kukaa Arsenal kuona hapati mafanikio wakati nyumbani kwao makombe kila siku.Katika kipindi chote cha sekeseke lake amekaa kimya na hakutaka kuwauzi mashabiki.Kina Ashley Cole,Flamini waliondoka kwa sababu ya kutaka pesa
Fabregas ameichezea Arsenal mechi 300+ amefunga magoli 57 na ame-assist magoli 100 ,anaingia kwenye kundi la wachezaji wenye stastistics nzuri kwa wachezaji wa Arsenal ingawa hakupata vikombe
 
Back
Top Bottom