Ezekiel Wenje: Magufuli asingekubali ufisadi huu wa awamu ya sita (Ripoti ya CAG)

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,665
Mbunge wa zamani wa nyamagana (chadema) EZEKIEL WENJE amesema kama Magufuli angekuwa hai asingekubali ufisadi huu ulio tajwa kwenye report ya CAG.

Wenje aliyekuwa waziri kivuli wa mambo ya nje ameosesha kubwa kwa sasa Chadema wanaona kubwa Magufuli alikuwa bora sana kwenye kupambana na rushwa na ufisadi

My take, kwa Magufuli kila goti litapigwa

USSR

Screenshot_20230407-181319.jpg
 
Kwani Kuna anayekataa JPM alikua anapambana na mafisadi? Wapinzani hatukugombana na JPM sababu ya kupambana na ufisadi ila masuala kama utawala Bora, kuharibu uchumi, kuua sekta binafsi, kuua wakosoaji, kulipunguzia bunge nguvu, kuingilia masoko mfano korosho, kutugawa kikabila na kikanda, kuandaa bajeti zisizo tekelezwa hata kwa 50%, kuminya media, kupunguza mamlaka ya bunge hasa kwenye kuisimamia serikali, kumtimu CAG kisa kuhoji kwanini haruhusiwi kukagua miradi ya kimkakati n.k.

So msifiche madudu ya JPM kwenye kitu kimoja alichojaribu kukifanya best (ingawa alifeli pia).
 
Inaitwa few to mention
Alikuwa mwanadamu sio Mungu
Madhaifu alikuwa nayo
 
Nafikiri ugomvi mkubwa wa wapinzani dhidi ya Magufuli ulikuwa issue ya utawala bora. Hata Mbowe alishakiri Tanzania haijawahi kupata Rais wenye udhubutu kama Magufuli lakini aliainisha mambo ambayo alikuwa hakubaliani nae.

Zitto pia majuzi kasema hivyo hivyo kuwa ule woga kwa mali ya umma aliojenga Magufuli ni moja ya makosa yaliyofanywa kwa utawala huu kuachana nayo.
 
Kwani Kuna anayekataa JPM alikua anapambana na mafisadi? Wapinzani hatukugombana na JPM sababu ya kupambana na ufisadi ila masuala kama utawala Bora, kuharibu uchumi, kuua sekta binafsi, kuua wakosoaji, kulipunguzia bunge nguvu, kuingilia masoko mfano korosho, kutugawa kikabila na kikanda, kuandaa bajeti zisizo tekelezwa hata kwa 50%, kuminya media, kupunguza mamlaka ya bunge hasa kwenye kuisimamia serikali, kumtimu CAG kisa kuhoji kwanini haruhusiwi kukagua miradi ya kimkakati n.k.

So msifiche madudu ya JPM kwenye kitu kimoja alichojaribu kukifanya best (ingawa alifeli pia).
Wewe kinachokusumbua ni chuki tu. Na chuki kama ilivyo upendo hupofusha. Huwezi kuona mazuri na hata yakijadiliwa mazuri ni kama roho inakuuma. Mada hapa ilikua namna JPM asingekubali ufisadi huu wa sasa, lakini kwasababu hiyo ni kama sifa nzuri kwa kiongozi aliyekwisha fariki huwezi kukubali kuijadili kwasababu chuki imekujaa, unataka uhamishe magoli. Utabaki hivyohivyo na chuki zako na utakuja kufa bila kelele kama wafuasi wa kibwetere huku JPM akiishi milele kupitia mazuri aliyoyafanya.
 
wewe kinachokusumbua ni chuki tu. Na chuki kama ilivyo upendo hupofusha. Huwezi kuona mazuri na hata yakijadiliwa mazuri ni kama roho inakuuma. Mada hapa ilikua namna JPM asingekubali ufisadi huu wa sasa, lakini kwasababu hiyo ni kama sifa nzuri kwa kiongozi aliyekwisha fariki huwezi kukubali kuijadili kwasababu chuki imekujaa, unataka uhamishe magoli. Utabaki hivyohivyo na chuki zako na utakuja kufa bila kelele kama wafuasi wa kibwetere huku JPM akiishi milele kupitia mazuri aliyoyafanya
Huyu udini utammliza

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ezekiel Wenje acha unafiki!! Kwanza wewe mwenyewe ulikimbia nchi ukawa unaishi Kenya kwa kumuogopa Dikteta Magufuli. Umerudi nchini baada ya maridhiano yaliyofanywa na Mbowe na Samia waliokuwa hapa.

Tuchambue madhaifu ya ripoti kwa nna yalivyo lakini kamwe tusimuingize Magufuli katika huu mjadala.

Magufuli angekuwapo ingekuwa hivi:

(1) Aldha Ripoti ingebadilishwa ili isionyeshe udhaifu wa ufisadi
AU
(2) CAG Kichere angefukuzwa kazi kama ilivyomtokea Profesa Assad mwaka 2018.

Tumpongeze Samia kwa kukubali Ripoti ya CAG ya mwaka 2021/22 isomwe na kujadiliwa kwa uwazi.

Tusubiri hatua za kiutaratibu zitumike kuwachukulia hatua wate waliohusika kwa kuwa siyo kila query ni fraud
 
Magufuli huyu huyu aliyepambana na CAG Assad kwa kushirikiana na Ndugai hadi Prof wa watu akauona uCAG mchungu?

Wenje amekula maharage ya wapi?
 
Ezekiel Wenje acha unafiki!! Kwanza wewe mwenyewe ulikimbia nchi ukawa unaishi Kenya kwa kumuogopa Dikteta Magufuli. Umerudi nchini baada ya maridhiano yaliyofanywa na Mbowe na Samia waliokuwa hapa.

Tuchambue madhaifu ya ripoti kwa nna yalivyo lakini kamwe tusimuingize Magufuli katika huu mjadala.

Magufuli angekuwapo ingekuwa hivi:
(1) Aldha Ripoti ingebadilishwa ili isionyeshe udhaifu wa ufisadi
AU
(2) CAG Kichere angefukuzwa kazi kama ilivyomtokea Profesa Assad mwaka 2018.

Tumpongeze Samia kwa kukubali Ripoti ya CAG ya mwaka 2021/22 isomwe na kujadiliwa kwa uwazi.

Tusubiri hatua za kiutaratibu zitumike kuwachukulia hatua wate waliohusika kwa kuwa siyo kila query ni fraud
Unateseka ukiwa wapi

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom