Ezekiel Wenje awasha moto Bungeni

Kwa mtizamo wangu hakuna rushwa kubwa na ndogo. Kipimo hicho anakijua yule anayedaiwa na anayedai rushwa i.e. shs 2,000 inaweza kuwa ndogo sana kwa mtu fulani lakini kubwa kwa mwingine. Kukomesha rushwa across the board kunahitaji mtoaji kukataa kutoa rushwa na kuwepo na adhabu kali kwa muombaji rushwa. Hii adhabu isiwe kwa watu wachache but everyone regardless ya cheo au nafasi yake kwa jamii. Kukomesha rushwa pia kutahitaji mamlaka husika kuangalia ni kwanini watu wanakuwa tempted kuomba rushwa. Nionavyo mimi rushwa haiwezi kuisha kabisa lakini TZ tunaweza kupunguza rushwa kwa kiwango kikubwa if we are all serious about it.

Kuhusu rushwa kubwa na ndogo, hili ndilo asilolielewa Wenje.

Rushwa ni dhambi kama cannibalism, huwezi kusema eti mie naua na kula watu, lakini sili wakubwa, nakula vitoto vidogo tu.

Ukishakula rushwa umekula rushwa, ukishaua mtu umeua, hakuna tofauti kati ya kuuamtoto na mtu mzima.

Halafu rushwa inafanana na cannibalism katika aspect nyingine pia.

Ukishaweza kuanza kuua na kula nyama ya watu mara ya kwanza, mara ya pili huogopi, tena unapata uchu wa kula zaidi.

Ukishaanza kula rushwa ndogo, utakuwa huridhiki na rushwa ndogo, kila siku unapigia mahesabu rushwa kubwa.

Kwa hiyo tofauti ya hawa askari polisi na mawaziri inakuwa ni opportunity tu, siku yoyote wakipata nafasi na wao wanaitumia kuchukua rushwa.

Ndiyo maana ni muhimu kukemea rushwa yote, kwa sababu ukisema hii ya polisi ni ndogo, hao wanaokula rushwa ndogo leo kesho hawataridhika nayo, watataka kula kubwa, na wakipata ubunge/ uwaziri kitu cha kwanza ni kula rushwa kubwa.

Thank you, nimelisema hili pia.

Hatari ni kwamba sasa tunakaribia kutochambua mada, watu wanangalia, nani kasema? CHADEMA? Oyeeeee, hata kama upuuzi.

CHADEMA ni Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, kutetea rushwa ndiyo Demokrasia na Maendeleo?

Manifesto ya CHADEMA inasemaje kuhusu rushwa? Katiba ya CHADEMA inasema nini kuhusu rushwa?

Ndivyo miongozo ya CHADEMA inavyosema kuhusu rushwa hivi au huyu bwana katetereka yeye kama mtu binafsi tu?

Tuambizane tujue kabisa kwamba CHADEMA wakichukua nchi rushwa "ndogo" itaruhusiwa mpaka rushwa "kubwa" imalizwe kwanza.

jamaa ni mwana taarabu nini ?

Watoto wa shule za msingi wanasoma huku wamekaa chini wakati kumbe inawezekana kabisa kuchangisha idara mbalimbali kuilaini shsbillioni moja. Kwa nini basi tusitumie mbinu hiyohiyo kila idara ya serikali ipewe shule za msingi kama mia hivi iwe ni mlezi wake?

wanafanya makusudi hata wajumbe wa nyumba kumi DAR waliwaita kwenye kikao wakawakalisha chini

Tatizo linakuja.

Kukemea hypocrisy ya wabunge wanaojitia kukemea rushwa wakati wao wanachukua rushwa ni kitu kimoja. Hili sina tatizo nalo, hypocrisy inanuka popote pale inapojitokeza.

Lakini, ukikemea hipocrisy, sio lazima utete rushwa ndogondogo. Unaweza kukemea hypocrisy ya wabunge/mawaziri na kukemea rushwa ndogo vile vile.

Wanje hakukosea kukemea hipocrisy, amekosea kutetea rushwa ndogo.

Hivi kumbe Wenje amewataka polisi waendelee kula rushwa au? Maana sijakuelewa hapo

kiranga nimesoma post zako,kimantiki upo sahihi ila hiyo mantiki kuna wakati haifanyi kazi inabidi njia mbadala kutumika,natafuta namna kuweka sawa hili mkuu,wenje hajakosea kwa mazingira halisi ya bunge.

kiranga nimesoma post zako,kimantiki upo sahihi ila hiyo mantiki kuna wakati haifanyi kazi inabidi njia mbadala kutumika,natafuta namna kuweka sawa hili mkuu,wenje hajakosea kwa mazingira halisi ya bunge.

Kusema rushwa ndogo inaruhusiwa mpaka rushwa kubwa imalizike unaweza kuku excuse?

Rushwa ndogo inaishia wapi na kubwa inaishia wapi?

Rushwa ndogo na kubwa ni sawa kwa milionea na mtu wa kima cha chini?

Unapimaje kujua hii ndogo na hii kubwa?

Kiwango gani cha shilingi kinatenganisha rushwa ndogo na kubwa?

Na vipi kama rushwa na hela ndogo inaleta madhara makubwa ya kijamii -nimetoa mfano wa polisi na hospitali mtu kufa kwa kukosa shilingi 2,000 ya rushwa- hii ni rushwa kubwa au ndogo?

Na vipi kama mtu anaona anaweza kumbutua muwekezaji anayejipendekeza kumpa dola milioni moja, bila taifa kupata madhara makubwa, hiyo ni rushwa ndogo au kubwa ?

Mpaka 2013 kutakuwa na mabadiliko makubwa sana ya kisiasa ndani ya Tanzania. Moto uliowashwa si rahisi kuuzima na kilichoanza kuungua ni lazima kiteketee. Ni furaha kuona watanzania wanafungua macho na kutoa pamba masikioni kwa lengo la kuona, kusikia na kuelewa kwamba UHURU halisi wa Watanzania walio wengi (97%) ulikuwa bado haujapatikana. Tanzania ilipata uhuru toka kwa wakoloni weupe 1961 na kutawaliwa na wakoloni weusi ambao mpaka sasa bado wapo madarakani. Lakini cha moto wanakipata. ALUTA ........................

Kwa hiyo Wenje anasema nini sasa? Ni halali kwa wadogo kula rushwa kwa sababu wakubwa wanakula rushwa?

Kwa minajili hii anatuambia kwamba na yeye anakula rushwa kwa sababu mawaziri wanakula rushwa?

Kama hali rushwa, kwa nini anasema "hawezi kutumia nguvu nyingi kupigia kelele polisi wapunguze rushwa" ?

Anaelewa kwamba "two wrongs do not make a right"?

Kwamba wrong is wrong, even if the entire Tanzanian population is doing it.

Wabunge wetu wanaelewa kwenda kwa principle au ni bendera kufuata upepo?

Hawa ndio wanamageuzi wenyewe hawa? Wanao excuse rushwa kwa sababu mkubwa anakula rushwa?

Really?

Wenje anataka kero za wananchi wa kawaida zifugwe eti kwa sababu Mawaziri wanakula rushwa?

Kama tuna uwezo wa kukamata traafic police wanaoomba rushwa, tuwaachie kwa sababu mawaziri wanakula rushwa?

Huyu ndiye mbunge wetu msomi huyu?

Hivi alikuwa anamsema Lusinde hajasoma, yeye kasoma nini? Alichosoma kimemsaidiaje mpaka sasa kiasi anaweza kutoa kauli za kipumbavu kama hizi?

Mkuu, nilifikiri ukikopi alichosema Wenje ungesoma kuanzia paragraph ya kwanza ya maneno yake uliyokopi?!

Kijana jasiri uyu no wonder alimwangusha mbunge wa magamba kama sikosei Masha!

Hakika tutashinda, mwisho wa ccm umefika!

Tatizo ni je, hata kama mwisho wa CCM utafika, hilo litabadilisha lolote la msingi kwa wananchi?

Wazambia walimtoa Kaunda na kumuweka Chiluba na chama chake, baadaye wakajuta.

My point is, kuchoka kwetu sana na CCM kusitufanye tukubali yeyote atakayekuja, hata watu ambao wanatamka wazi kwamba tufumbie macho rushwa ndogo wakati tunapia vita rushwa kubwa.

Najaribu kuwa objective na kuangalia issues bila ushabiki wala chuki, naona kama vile kutoitaka CCM kunaweza kuwafanya watu wengi kusema "bora mwingine yeyote lakini si CCM". Kusema hivi ni hatari kwa sababu wanamapinduzi wengi walioingia serikalini kwa gia ya mabadiliko, kwa kuwa hawakumulikwa vya kutosha, wameishia ku abuse trust ya watu.

I am not saying CHADEMA ata abuse, but with comments kama hizi za kutetea "rushwa ndogo" one certainly has to wonder.

Mkuu, nilifikiri ukikopi alichosema Wenje ungesoma kuanzia paragraph ya kwanza ya maneno yake uliyokopi?!

Unaweza kuandika treatise ya kurasa 1500 nzuri sana. Ukakosea mstari mmoja tu.

Critics wako wakichukua mstari huu mmoja tu uliokosea wakasema umesema hilo watakuwa hawajakosea.

Unaweza kuingia mkataba mzuri sana, lakini mstari mmoja tu ukabadilisha maana nzima ya mkataba.

Wenje kasema vizuri mostly, lakini hii habari ya kutetea "rushwa ndogo" whatever that is, kachemsha na inabidi a retract hiyo statement.

Huwezi kuwa mkulima unapalilia shamba, halafu ukasema mimi nangoa vichaka vikubwa tu, hivi vijani vidogo naviacha.

Hivyo vijani vidogo vya leo ndio vichaka vikubwa vya kesho.

Tatizo ni je, hata kama mwisho wa CCM utafika, hilo litabadilisha lolote la msingi kwa wananchi?

Wazambia walimtoa Kaunda na kumuweka Chiluba na chama chake, baadaye wakajuta.

My point is, kuchoka kwetu sana na CCM kusitufanye tukubali yeyote atakayekuja, hata watu ambao wanatamka wazi kwamba tufumbie macho rushwa ndogo wakati tunapia vita rushwa kubwa.

Najaribu kuwa objective na kuangalia issues bila ushabiki wala chuki, naona kama vile kutoitaka CCM kunaweza kuwafanya watu wengi kusema "bora mwingine yeyote lakini si CCM". Kusema hivi ni hatari kwa sababu wanamapinduzi wengi walioingia serikalini kwa gia ya mabadiliko, kwa kuwa hawakumulikwa vya kutosha, wameishia ku abuse trust ya watu.

I am not saying CHADEMA ata abuse, but with comments kama hizi za kutetea "rushwa ndogo" one certainly has to wonder.
Mkuu hapo red Wenje alimaanisha kuwa Viongozi wa Chama (CCM) na Serikali watoe Bolt machoni mwao ndiyo waanze kutoa vibanzi machoni mwa Askali, Nadhani ieleweke hivyo!

Back
Top Bottom