Maundumula
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 7,553
- 3,070
Muulize kwanini anaajiri ma Expert uchwara kutoka India wakati vijana wa kitanzania wapo mitaani hawana ajira?
Mkuu zomba hili swali nimelielekeza kwa Mohammed Dewji inawezekana hizo sababu zipo lakini si kwa waTanzania wote nadhani hata wewe utakubaliana na mimi.
Nafarijika Mohammed Shossi amekupa like kubwa lakini kasahau juzi alikuja na bandiko lake kwamba wakati wa zoezi la kitambulisho cha uraia alinyanyaswa kwasababu ya rangi yake leo anafurahia waTanzania weusi wanavyonyayaswa na Mohammed Dewji wametengewa vyoo vichafuu, michango yao ya NSSF haipelekwi, mishahara ya waTanzania weusi ni chini sana huku wahindi wenzao wahindi wakilipwa mishahara mara tano hadi kumi zaidi.
Yafaa Mohammed Dewji anapowaomba kura wananchi wa Singida awaambie ajira zake ni za kibaguzi na ataoa sababu hizi hizi alizotoa Zomba.
Sasa Mkuu Ngongo labda nikuulize swali,
waTanzania weusi wanavyonyayaswa na Mohammed Dewji wametengewa vyoo vichafuu, michango yao ya NSSF haipelekwi, mishahara ya waTanzania weusi ni chini sana
Sasa Mkuu Ngongo labda nikuulize swali,
Wametengewa vyoo vichafu kivipi? ... Kwanini wasivisafishe? Tukubali au tusikubali usafi wa vyoo vya jumuia nchini mwetu ni wa hali ya chini sana, hata sehemu ambazo zina maji.
Michango ya NSSF haipelekwi? Yaani umenikata hela za NSSF halafu??? Peleka pay stub mahakamani.
Hili namjibia:
Kwa sababu:
Wafanya kazi wa Kitanzania wengi ni wavivu, wezi, waongo, hawaishi kufiwa na kuomba ruksa za kwenda kuzika, hawaishi kuumwa, hawaishi kuwa na kila sababu za kutokuhudhuria kazini. Watu wa India wanajuwa dhiki ya maisha na vipi kupata kazi ni kugumu na wao huchapa kazi na hawana visingizio kama Watanzania.
Inapaswa Watanzania wanaotaka maendeleo ya haraka wabadilike.
Oops, nilisahau:
Hawaishi kukopa (kujichotea) makazini, hata iwe ni viongozi wa vyama vya siasa.
Mkuu, umeweka chumvi nyingi sana. NINA WASIWASI KAMA WEWE NI RAIA WA TANZANIA, LAZIMA UTAKUWA MHAMIAJI, TENA HARAMU AU UNA ROHO MBAYA. Hayo yapo kwa sababu sisi ni watanzania na tunaishi hapa na ndugu zetu. huwezi ukaacha kujumuika na jamii yako inapofikwa na misiba. mbona hata hao maboss wanapo pata misiba ya ndugu zao huko kwao nje huwa wanasafiri kwenda kujumuika na ndugu zao??? BEFORE WEALTH, THERE IS HUMANITY. cha msingi, ni kuweka utaratibu wa matukio gani hasa mfanyakazi apewe ruhusa ya kutohudhuria kazini, WATANZANIA NI WAELEWA NA WANA UBINADAMU SANA.
Katika kipindi cha Makutano Jumamosi ijayo mgeni atakaeongea na Fina Mango ni mbunge wa Singida Mjini Mheshimiwa Mohammed Dewji atakaeongea masuala mbalimbali ikiwepo maisha yake binafsi, ya kisiasa na kibiashara.
Kama una swali lolote ambalo ungependa Mheshimiwa Dewji alijibu tafadhali uliza na litasomwa hewani siku ya kipindi kuanzia saa tisa mchana kupitia 92.9FM Dar, 93.3FM Dodoma, 98.6FM Arusha/Moshi, 101.7FM Dodoma.
Karibu
Ile ya wiki iliyopita ya Mo Dewji mlifanikiwa?sijaona follow up kama ilivyokuwa ile ya Zitto.
Alijibu maswali yote ikiwa ni pamoja kutolea ufafanuzi kiwanja kilichokua na mgogoro
Alijibu maswali yote ikiwa ni pamoja kutolea ufafanuzi kiwanja kilichokua na mgogoro
Alijibu maswali yote ikiwa ni pamoja kutolea ufafanuzi kiwanja kilichokua na mgogoro
Alijibu maswali yote kabisa?najua ile ya Zitto kulikuwepo na follow up thread yenye link ya mahojiano hayo.Je unaposema maswali yote,una maana maswali yote uliyoyachagua ama ni maswali yote yaliyoulizwa na members humu kwenye ile thread?je kuna uwezekano wa sisi ambao hatukupata nafasi/uwezo kusikiliza kuyapata maswali hayo endapo uliyachagua?
Hili ni bandiko langu la mwisho lenye maswali yenye kuhusiana na mahojiano yaliyopita endapo utanijibu haya.Hili litasaidia kupisha wenye maswali kuhusiana na wageni wako watarajiwa.
Natanguliza shukran...