tindikalikali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 4,855
- 1,117
Wana jf, kuna msichana ambaye nimekuwa naye toka 2008, mazingira yalitukutanisha wakati huo nikiwa na maumivu ya kuachwa. Niliamua kuwa naye nikiamini pengine moyo wangu uliovunjika utabadilika na kupenda tena. Kadri siku zilivyokwenda ndivyo nilivyobaini kwamba simpendi., nilijivika ujasiri wa kumwambia lakini hakunielewa. Mpaka muda huu nnavyoandika haya, nimegandwa mithili ya ruba, nashindwa jinsi ya kumwacha. Jamani sipendi kuendelea kudanganya, nafsi yangu inanisuta kwa sina malengo yeyote kwake.