Eti kunatofauti gan kat ya MTU na BINADAMU mana dah!

MUREFU

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,331
350
WanaJF ninaomba mnisaidie mana 2libishana sana na pia huwa nimeshasikia weng wakisema au ku2mia maneno haya kat ya MTU na BINADAMU lakn wanavyoyatumia inakuwa kama kunautofaut ninaomben msaada wenu plzz?
 
Mtu ni aliyeumbwa na Mungu kwa mfano wake( roho sio moyo), binadamu ni yule tunayemuumba chumbani(damu na nyama) aka nafsi
 
Kuna mtu mwenye utu na mtu asiye na utu. Lakini wote hao ni watu.

Kinachowatofautisha ni ufahamu unaoitwa Utu!

UTU NI UBINADAMU! Hakuna myama au kiumbe kingine chenye utu au ubinadamu.
 
Mtu ni aliyeumbwa na Mungu kwa mfano wake( roho sio moyo), binadamu ni yule tunayemuumba chumbani(damu na nyama) aka nafsi

mh! Awap czan labda ila cnauhakika mana binadamu anaumbwa chumban kivp mbona umeniacha hapo
 
Kuna mtu mwenye utu na mtu asiye na utu. Lakini wote hao ni watu.

Kinachowatofautisha ni ufahamu unaoitwa Utu!

UTU NI UBINADAMU! Hakuna myama au kiumbe kingine chenye utu au ubinadamu.

kidogo i get somethng now broo kidogo
 
Binadamu (Bin Adam) ni kiumbe/mnyama (biological being) ambaye ana sifa unazozifahamu na anatofautiana na wanyama wengine kwa kuwa ana akili na utashi mkubwa kuliko wao (wanyama wengine). Binadamu anatambulika kisayansi kama Homo sapiens. Kiingereza binadamu anaitwa Human being. Pia huitwa man bila kujali jinsia ikimaanisha kinachotajwa ni u-kiumbe wake na si jinsia yake.

Mtu ni binadamu kwa maana ya nafasi (si cheo) katika jamii (social being), linganisha na biologivcal being hapo juu. Nitatoa mfano tofauti lakini unaorandana kimtazamo. Dunia ni sayari kwa maana ya tufe linalozunguka jua wakati ulimwengu maana yake mi mabara na watu wake (tafsiri zingine zinasema ulimwengu ni universe, mimi nazungumzia world), vivyo hivyo binadamu ni product ya uumbaji (kama earth) wakati mtu ni product ya binadamu na mahusiano na wengine (world).

Wakati mwengine lugha ya picha (figurative language) humtaja binadamu kama mtu mwenye tabia au roho nzuri, mfano Marijani Rajabu aliimba,

"Duniani sasa imani imekwisha,
...........
...........
Penye watu kumi binadamu mmoja."

Kifupi,
Ukimtaja binadamu unazungumzia kiumbe, ukimtaja mtu unazungumzia mwanachama wa jamii/jamaa (society) ya binadamu.
 
WanaJF ninaomba mnisaidie mana 2libishana sana na pia huwa nimeshasikia weng wakisema au ku2mia maneno haya kat ya MTU na BINADAMU lakn wanavyoyatumia inakuwa kama kunautofaut ninaomben msaada wenu plzz?

hayo maneno hayana tofauti ni neno lenye maana moja

MTU ni kibantu asilia, Lugha nyingi za kibantu zinatumia hilo neno MTU, NTU, MUNU
BINADAMU ni neno la kiarabu tulilolitohoa na likaingia kwenye kiswahili, na maana ya hilo jina ni BIN ADAM , yaani tu wenye nasaba na Adamu (mtu wa kwanza kuumbwa kwa wenye kuamini hivyo), ni kama sawa na wanaposema Sayyid BIN Sayyid (Yaani huyo ni Sayyid mwenye nasaba na Sayyid (Babayake))
 
dah! Mnakuja vzur hebu endeleen kunisaidia mana ndo ninaanza kufunguka kwambal
 
Back
Top Bottom